Wanawake walivyoishusha hadhi dhambi ya uzinzi kuwa sawa na dhambi maarufu Afrika ya Uongo

Ugoni ni baada ya kufumaniwa , mfano mimi na pisi yangu najipigia sitaki ndoa hizi za kizungu na kwa binti nafahamika utaniitaje mzinzi?
Ndoa sio za kizungu, zipo hata kabla ya dini. So wewe utaonekana muhuni tu na kama ni mmoja muda mrefu kisheria anakuwa mke wako japo wewe unaona unajipigia
 
Dhambi ya uzinzi imeshushwa hadhi sana na wanawake. Ugumu wa maisha na tamaa zisizona breki zimepelekea wana wa kike kuwa cheap kila siku zinavyokwenda.

Zinaa imeshuka hadhi na sasa imekuwa dhambi kama uongo. Dhambi ya uongo ndio nyepesi kufanyika sana afrika maana maisha yetu yamekaa kisiasasiasa na ujanjaujanja.

Sasa hivi mtu akila tunda kimasihara au kwa kusudiana sio habari ya kujivunia bila kujali ni mke wa mtu, msomi, mwasasiasa, mzungu, mchina, mchungaji au ustaadhat hatushangai ni kawaida kabisa.

Ushauri:
Jitahidi kushughulika na mambo ya maana sio kifukuzia wakina mama au dada maana kwa sasa ni sawa na kuwinda kuku wa kisasa broiler kwa mishale na na mabomu.

Zinaa sio kitu cha kujivunia au kujipongeza. Ni afadhali uokoe Muda kwa kutafuta utakayemvumilia uoe kisha uendelee na harakati nyingine za maisha.

Ni hayo tu.
Unafikiri hao wanaogawa hawana wazazi? Je wakulaumiwa ni wazazi au ni watoto?

Kiujumla nafikiri kushuka kwa thamani ya wanawake kumesababishwa na kulegalega kwa mfumo wa malezi ambao wahusika wakubwa ni wanaume kukimbia majukumu ya kulea.

Kiuhalisia wazazi wa kike wanaweza kukuza watoto lakini hawawezi kulea, jukumu la kulea ni la wanaume.
 
Kwa mtazamo wa Mwenyezi Mungu dhambi zote ni sawa.

Ila kibinadamu Zinaa imepewa hadhi kubwa sana. Ndio maana makanisani unaweza kudanganya hadi unakufa wanakuangalia tu ila siku ukijichanganya ukazini na ukawa wazi lazima wakule kichwa na kukuona kama shetani.
Hii ni sehemu ambayo watu mnatia akili zenu mfukoni na kukubali unachokiona wazi kabisa kuwa hakiingii akilini.

Ukisema kwa Mungu dhambi zote ni sawa unamaanisha Mungu ataadhibu sawa kosa la mauaji na kosa la kijana aliyeiba mkate. Huku ni kumshutumu Mungu kwa ukosefu wa uadilifu wakati sote tunajua hakuna mkamilifu zaidi yake.

Watoto wako tu nyumbani huwezi kuwaadhibu sawa kwa kila kosa, yapo makosa utamsema/kumkosoa na yapo makosa utamuadhibu, na katika hayo kuna mengine utampa adhabu kali kuliko mengine!

Nyie endeleeni tu kutii amri za dola ya kirumi.
 
Aliesema usiue ndiye aliesema usizini.

Kwa hiyo aliesema usizini ndiye aliesema usisema uongo,

Dhambi ni ile ile na moto ni ule ule
 
Ulo sahihi dhambi haziwezi kuwa sawa hata kidogo maana hata hao wachamungu wanatenda dhambi ila dhambi wanazotenda wao si sawa na wanazofanya wasio na hofu na mungu
 
Aliesema usiue ndiye aliesema usizini.

Kwa hiyo aliesema usizini ndiye aliesema usisema uongo,

Dhambi ni ile ile na moto ni ule ule
Usijiongopee ndugu yangu dhambi haziwezi kuwa sawa hata mara moja, kwa hiyo anayeua watu na anayeiba shambani kwa mtu kwa kuwa alishikwa na njaa ambayo ingepelekea kifo wataadhibiwa sawa??
 
Dhambi ya uzinzi imeshushwa hadhi sana na wanawake. Ugumu wa maisha na tamaa zisizona breki zimepelekea wana wa kike kuwa cheap kila siku zinavyokwenda.

Zinaa imeshuka hadhi na sasa imekuwa dhambi kama uongo. Dhambi ya uongo ndio nyepesi kufanyika sana afrika maana maisha yetu yamekaa kisiasasiasa na ujanjaujanja.

Sasa hivi mtu akila tunda kimasihara au kwa kusudiana sio habari ya kujivunia bila kujali ni mke wa mtu, msomi, mwasasiasa, mzungu, mchina, mchungaji au ustaadhat hatushangai ni kawaida kabisa.

Ushauri:
Jitahidi kushughulika na mambo ya maana sio kifukuzia wakina mama au dada maana kwa sasa ni sawa na kuwinda kuku wa kisasa broiler kwa mishale na na mabomu.

Zinaa sio kitu cha kujivunia au kujipongeza. Ni afadhali uokoe Muda kwa kutafuta utakayemvumilia uoe kisha uendelee na harakati nyingine za maisha.

Ni hayo tu.
Mweee ebu wacheni zenu bwana mbususu tamu maana na mihangaiko yote ya kusaka pesa pasipo kula mbususu fofauti tofauti ni nini? That life is just struggle?
 
Usijiongopee ndugu yangu dhambi haziwezi kuwa sawa hata mara moja, kwa hiyo anayeua watu na anayeiba shambani kwa mtu kwa kuwa alishikwa na njaa ambayo ingepelekea kifo wataadhibiwa sawa??
Ndio Moto utakaokula ni moto mmoja ndugu. Kila mtu ambae hajatubu dhambi zake atachomwa.

Kama unaona kuna adhabu nyingine kwa mwenye dhambi labda wale waiba kuku na wasema uongo watakua na adhabu yao na wauaji ndo watachomwa moto haiko ivo ndugu. Wote ni moto tuu
 
Labda nikuelekeze kwa kifupi kwa kupitia maandiko.

Kwanza kabisa ieleweke sote tukifa tunaenda kwenye udongo. (Maana sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi)

Soma mwanzo 3:19
"kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi."

Kisha itakapofika kiama (kurudi kwa Yesu) hapo Yesu anakuja kuwachukuwa walio wake kwanza (watafufuliwa kwanza/ufufuo wa kwanza) kumbuka wenye heli wakishafufuliwa watu wengine ambao hawakutubu dhambi zao watabaki ardhini (hawatufufuliwa), kisha itapita miaka 1000 wenye heli wakiwa mbinguni na wenye dhambi wakiwa ardhini (kifungo cha shetani) Yesu atarudi tena na mji mpya (Yerusalem mpya) hapo ndo utakuepo ufufuo wa pili ( wa wenye dhambi) na wakishafufuliwa watajaribu kuuvamia Yerusalem wauchukue ndipo huo moto utawala wote.

Huo ndio moto ninao ongelea mimi ndugu
Soma kitabu cha Ufunuo kuanzia sura ya 20 pale

"
5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.
6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
UFUNUO 20:5-9

UKisoma kwa umakini hapo unaona moto ni mmoja unaowala wenye dhambi wote ndugu
 
Hapa ndo ambapo hujalewa na bila shaka ndo kwanini jamii nyingi zenye imani kama yako maovu ni mengi kwakuwa watu wanakuwa wameshakata tamaa juu ya kuiepuka dhambi. Hakuna mtu asiyetenda dhambi, ila hutofautiana ni aina ipi ya madhambi mtu hujikuta amefanya.

Dhambi/thawabu ni uzito wa kosa/jema ulilofanya. Chukulia thawabu ni +positive na dhambi ni -ve. Baada ya hapo pia tambua kuwa hizi dhambi zimegawanyika pande mbili, kuna dhambi dhidi ya haki ya mtu na dhambi dhidi ya haki ya Mungu kwako, mfano kutomshirikisha Mungu ni haki ya Mungu kutoka kwako wakati kuiba ni haki ya mtu uliyoichukua kutoka kwake. Mungu anasemehe tunayomkosea tukiomba toba lakini yapo mengine pia anasamehe hata bila ya kumuomba toba, as long as umejiepusha na madhambi makubwa i.e. Kuua, kumshirkisha yeye na miungu mengine n.k. Kwa upande haki ya mtu, hii utailipa tu either uilipe hapa duniani kwa kumrudishia haki yake au uilipe siku ya hukumu, otherwise huyo mtu akusamehe akiwa yeye bado yupo duniani, na akifanya hivo Mungu pia humsamehe na yeye madhambi yake kwa kiwango kikubwa zaidi ya kile alicho samehe yeye, na ndio maana tunahimizwa tusameheane. Sasa basi, Ikiwa umekufa na hujalipa haki ya mtu then yatachukuliwa mema katika mizani yako kwa kiwango cha uzani wa kosa ulilomfanyia na ataongezewa yeye katika mizani yake ya mema. Na ikiwa katika mizani yako mema yote yameisha (labda ulidhulumu wengi na hukuwa mtenda mema kwa wingi) basi yatachukuliwa madhambi ya yule uliyemdhulumu kwa uzito wa kosa ulilomtendea na utawekewa katika mizani yako.

Kwakuwa Mungu ni mwenye huruma, ikiwa uzito wa mema yako katika mizani ni mkubwa kuliko mabaya yako basi wewe utaingizwa peponi, as long as umejiepusha na madhambi makubwa ambayo yameanishwa adhabu zake na hapo ni kama umekufa hujatubia hayo madhambi.

Sasa ukubwa wa adhabu utatofautiana na uzito wa mizani yako katika mabaya yako. Miongoni mwa watakaokuwa na adhabu kali zaidi kuliko wengine ni Iblis (Lucifer) na Firauni.

Allahu aalam.
 
Labda nikuelekeze kwa kifupi kwa kupitia maandiko.

Kwanza kabisa ieleweke sote tukifa tunaenda kwenye udongo. (Maana sisi ni mavumbi na mavumbini tutarudi)

Soma mwanzo 3:19
"kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi."

Kisha itakapofika kiama (kurudi kwa Yesu) hapo Yesu anakuja kuwachukuwa walio wake kwanza (watafufuliwa kwanza/ufufuo wa kwanza) kumbuka wenye heli wakishafufuliwa watu wengine ambao hawakutubu dhambi zao watabaki ardhini (hawatufufuliwa), kisha itapita miaka 1000 wenye heli wakiwa mbinguni na wenye dhambi wakiwa ardhini (kifungo cha shetani) Yesu atarudi tena na mji mpya (Yerusalem mpya) hapo ndo utakuepo ufufuo wa pili ( wa wenye dhambi) na wakishafufuliwa watajaribu kuuvamia Yerusalem wauchukue ndipo huo moto utawala wote.

Huo ndio moto ninao ongelea mimi ndugu
Soma kitabu cha Ufunuo kuanzia sura ya 20 pale

"
5 Hao wafu waliosalia hawakuwa hai, hata itimie ile miaka elfu.
6 Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.
7 Na hiyo miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa, atoke kifungoni mwake;
8 naye atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za nchi, Gogu na Magogu, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
9 Wakapanda juu ya upana wa nchi, wakaizingira kambi ya watakatifu, na mji huo uliopendwa. Moto ukashuka kutoka mbinguni, ukawala.
UFUNUO 20:5-9

UKisoma kwa umakini hapo unaona moto ni mmoja unaowala wenye dhambi wote ndugu
Mada imekaa katika mtazamo wa dhambi machoni petu.
Maana hata makanisa huwa yanafuta watu ushirika wakizini na kugundulika
Huwa wanafutwa kabisa ushirika wakati watu wanatoa ahadi za uongo au kuongopa wanaonekana nj kitu cha kawaida.

Mfano Paulo anawaambia wakorinto wale wazinzi wa kanisani watengwe kwa shetani. Musa aliagizwa wapigwe mawe hadi kufa. Lakini sio waongo

Msingi wa mada ni kwamba kiwango cha uzinzi kimefikia machoni pa watu kuwa kawaida karibu na dhambi ya uongo au kimevuka.
Watu wanaweza kuzini bila hata kuongea kwa kuangaliana machoni tu.
 
Back
Top Bottom