Mbogo_beichee
JF-Expert Member
- Mar 31, 2021
- 224
- 608
Boss kwa maelezo unayotoa hapo kwanza kabisa inaonyesha wew ni muislamu.Hapa ndo ambapo hujalewa na bila shaka ndo kwanini jamii nyingi zenye imani kama yako maovu ni mengi kwakuwa watu wanakuwa wameshakata tamaa juu ya kuiepuka dhambi. Hakuna mtu asiyetenda dhambi, ila hutofautiana ni aina ipi ya madhambi mtu hujikuta amefanya.
Dhambi/thawabu ni uzito wa kosa/jema ulilofanya. Chukulia thawabu ni +positive na dhambi ni -ve. Baada ya hapo pia tambua kuwa hizi dhambi zimegawanyika pande mbili, kuna dhambi dhidi ya haki ya mtu na dhambi dhidi ya haki ya Mungu kwako, mfano kutomshirikisha Mungu ni haki ya Mungu kutoka kwako wakati kuiba ni haki ya mtu uliyoichukua kutoka kwake. Mungu anasemehe tunayomkosea tukiomba toba lakini yapo mengine pia anasamehe hata bila ya kumuomba toba, as long as umejiepusha na madhambi makubwa i.e. Kuua, kumshirkisha yeye na miungu mengine n.k. Kwa upande haki ya mtu, hii utailipa tu either uilipe hapa duniani kwa kumrudishia haki yake au uilipe siku ya hukumu, otherwise huyo mtu akusamehe akiwa yeye bado yupo duniani, na akifanya hivo Mungu pia humsamehe na yeye madhambi yake kwa kiwango kikubwa zaidi ya kile alicho samehe yeye, na ndio maana tunahimizwa tusameheane. Sasa basi, Ikiwa umekufa na hujalipa haki ya mtu then yatachukuliwa mema katika mizani yako kwa kiwango cha uzani wa kosa ulilomfanyia na ataongezewa yeye katika mizani yake ya mema. Na ikiwa katika mizani yako mema yote yameisha (labda ulidhulumu wengi na hukuwa mtenda mema kwa wingi) basi yatachukuliwa madhambi ya yule uliyemdhulumu kwa uzito wa kosa ulilomtendea na utawekewa katika mizani yako.
Kwakuwa Mungu ni mwenye huruma, ikiwa uzito wa mema yako katika mizani ni mkubwa kuliko mabaya yako basi wewe utaingizwa peponi, as long as umejiepusha na madhambi makubwa ambayo yameanishwa adhabu zake na hapo ni kama umekufa hujatubia hayo madhambi.
Sasa ukubwa wa adhabu utatofautiana na uzito wa mizani yako katika mabaya yako. Miongoni mwa watakaokuwa na adhabu kali zaidi kuliko wengine ni Iblis (Lucifer) na Firauni.
Allahu aalam.
Basi sasa wakati unatoa maelezo kama hayo ungekuwa una rifaa kutoka kwenye Quran tukufu, maana tutajuaje kama unatunga stori tuu. Tupe mafungu ya Quran tukufu na sisi tufatilie kama mim nilivotoa kwenye mafungu ya Biblia
Asante.