Wanawake walivyoishusha hadhi dhambi ya uzinzi kuwa sawa na dhambi maarufu Afrika ya Uongo

Boss kwa maelezo unayotoa hapo kwanza kabisa inaonyesha wew ni muislamu.

Basi sasa wakati unatoa maelezo kama hayo ungekuwa una rifaa kutoka kwenye Quran tukufu, maana tutajuaje kama unatunga stori tuu. Tupe mafungu ya Quran tukufu na sisi tufatilie kama mim nilivotoa kwenye mafungu ya Biblia

Asante.
 
Yah sasa mtoa mada kasema Uzinzi umekua kama kudanganya kwa kutoa kauli kama hiyo inamaanisha Kudanganya kama ni dhambi fulani ambayo yeye binafsi ameshaizoea sana na ni ndogo sana.

Ndo tunamwambia dhambi zote ni sawa. Aliesema usizini ndiye aliesema usiseme uongo. Kwa hiyo moto utakuwa ni ule ule
 
Bongo uongo ni jambo la kawaida na uzinzi ulikuwaga ni kitu cha ajabu sana.
Kwa ulaya uzinzi ulianza kuwa kitu cha kawaida miaka mingi iila uongo ni jambo la ajabu.

Development ya zinaa duniani kwa sasa uzito wake kwenye jamii zetu za kibongo unakaribia au umevuka ukawaida wa uongo na umbea.
 
Na hapo sijaelewa vizuri maana ya kunijibu maana mimi nimesema moto ni mmoja na nimetoa maelezo yangu hapo chini kuwa itakuaje kulingana na Maandiko ya Biblia.

Sasa wakati huo na wew ungetoa maelezo yako kwamba labda kwenye Quran tukufu inasema kutakuwa na moto zaidi ya mmoja.

Hapo naona umeelezea namna hukumu itakavokuwa, sasa baada ya hiyo hukumu wale waliohukumiwa mauti ya pili au kuangamia milele watauliwa na nini?

Tupe maandiko ndugu tujifunze
 
Mmh hapo kwenye dhambi kuwa jambo la ajabu na kuwa jambo la kawaida mimi naona ni kwa mtu mtu binafsi

Maana kwa mtu ambaye unamfata Muumba wako kila siku na upo thabiti inakuaje dhambi ya kudanganya ikawa ya kawaida na kuzini ikawa ajabu.

Mimi naona vyote vitakuwa ni ajabu tuu maana haujavizoea

Ila mim naamini ukawaida unakuja kwenye mazoea, ukizoea dhambi fulani inakua ya kawaida kwako.
 
Mkuu dhambi si ni kila mtu na msalaba wake? Kulikoni tena dhambi ipi kushushwa hadhi na nani?
 
Ha ha ha ha
 
Moto umeitwa majina tofauti tofauti katika Quran kutokana na sifa husika zilizoongelewa, either ya hao watakaoingia motoni (Allah atuepushe) au kutokana na msisitizo wa sifa iliyokusudiwa ya huo moto. Majina hayo ni pamoja na Jahim, Jahannam, Laza', Sa'ir, Saqar, Hutama na Hawiya. Kuhusu uwepo wa levels tofauti tofauti za moto hiii aya chini inatunesha dalili hiyo:-

(Quran 4:145) Indeed, the hypocrites will be in the lowest depths of the Fire – and never will you find for them a helper.

Hii ni moja katika ishara ya kuwepo viwango tofauti ya adhabu ndani ya hiyo adhabu ya moto yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…