Wanawake wanaocheza michezo na vicoba wananufaiaika zaidi kuliko wanaume wanaobeti, Je ni muda wa wanaume kujitafakari kuhamia Vicoba ?

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Kote kuna "risk" za uso zipo ila uhalisia haujifichi, Kwenye vicoba kuna "Uwezekano / probability" kubwa kuzidi betting

Betting ni janga kubwa sana hapa nchini kwa wanaume, watu wanakula sana za uso hadi huruma, lakini ndio wanazama kabisa uraibu inakuwa ngumu kuacha kama ilivyo ulevi wa pombe ama uvutaji wa sigara, mtu anaweza kubeti mwaka mzima milioni lakini ni siku moja ama mbili tu kaotea elf 80 atajiona mwamba mpaka basi. Wengi huwa wanadanganya wanashinda ila uhalisia wanakula sana za vichwa, inabidi wadanganye tu ili kuondokana na aibu,

Tukija kwa wanawake nao kuna michezo yao huwa wanacheza na vicobba, na huku wapo wanaokula za uso ila kuna nafuu maana huwa ni kawaida kuona kuna wanaonufaika na kufanya maendeleo, ni kawaida kuona wanawake wa huku wananunua kiwanja, mashamba, magari, kuoata mitaji, n.k. wala si habari za kustukiza kama ilivyo kwenye kubeti.

Je ni Muda umefika kwa wanaume kukubaliana na uhalisia kwamba waachane na betting wahamie vicoba ?
 
Wanawake wanaocheza vicoba ndio wanao ongoza kugawa utamu. hii ni kwa mujibu wa sehemu ninayoishi. Huko kwingine sijui.
Mkuu suala la kugawa utamu ni mtu tu, hata mke wako muda huu unaandika hivi anaweza kuwa gesti yupo na mchepuko wake.
 
Mkuu suala la kugawa utamu ni mtu tu, hata mke wako muda huu unaandika hivi anaweza kuwa gesti yupo na mchepuko wake.
Duuh kwa bahati mbaya sina ndoto za kuwa na mke, alafu nipo lodge na kibinti pia. What a coincidence???!!
 
Kikoba kinafanya ujifunze njia nyingi za kutafuta pesa sababu kuna ujasiriamali ambao huwa unafundishwa huko ndani ya kikoba...

Hata wafanyakazi wanacheza vikoba...

Kuna fursa za kupata mkopo...

Kuna faida Kila baada ya muda...

Kuna kusaidiana kwenye shida na Raha...

Sio wanawake wote wanacheza vikoba wanaowaza kama mnavyowawazia...
 
Ikifanyika research unaweza kuta wanaume wanaocheza indirectly na kunufaika na mikopo ya hivyo vikoba ni wengi sana tofauti na unavyofikiria 😁😁..
Unakuta mwanamke kashika hisa hata za watu watatu kumbe ni mume au watoto wake ndo wanahusika na ratiba ya michango na kukivunja wanaijua
 
Wanaume tunabet, mikeka ikitiki tunawapa wanawake wakacheze vikoba, mwisho wa siku watafiti wanasema vikoba vinalipa.
Wtf
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…