At least wewe umeongea point, nimekuwa muungaji mkono sana wa mada za huyu jamaa juu ya haya mambo, ila sasa naanza kushtuka. Inawezekana jamaa anawachukia wanawake.
Kusema kwamba ndoa ndio jambo la maana kuliko yote katika maisha ya mwanamke, ni kupigia debe unyanyasaji, utumwa, ukatili na mateso wanapitia wanawake kisa tu kulinda ndoa, maana jamii imemuaminisha kuwa ndio kitu cha thamani kuliko chochote.
Ni kusababisha wanawake wanaojiweza, wasomi, wenye nyadhifa na mchango katika jamii wajione hawana maana yeyote, kama hawajaolewa. Hii ni imani ya kikatili, yenye lengo la kutweza na kudhalilisha utu wa mwanamke.
Waungwana wote tunatakiwa kupiga vita imani hii ya kishenzi. Cc
Nyumisi