Wanawake washaurini(kuwasaidia) binti zenu kutafuta mume kuanzia wakiwa miaka 17-25

Wanawake washaurini(kuwasaidia) binti zenu kutafuta mume kuanzia wakiwa miaka 17-25

Ila naona mambo yako tofauti na zamani naona miaka18 ya enzi zile ni saw na 22 ya sasa Kwa kweli wapo wanawake wengi juu ya 25 hawana watoto na wanaoforce huzalia nyumbani
 
Ramadhan Kareem!

Dada zangu, wadogo zangu wakike, pamoja na kina Mama, elimu hii ni muhimu Sana.
Dunia ya sasa imefikia pagumu Sana, hasa kwenye kipengele cha ndoa.
Maneno yenye hekima kubwa sana na wenye masikio wasikie maneno haya toka kwa Taikoni wa Fasihi[emoji848]...
 
Mila za Afrika za kuaminisha watoto, hasa wa kike, kwamba kuolewa ndio kitu cha muhimu kuliko vyote katika maisha yake ni za kipuuzi.

Ndugu mliofanikiwa kupata mwanga wa elimu, ukiwemo wewe mtoa mada, msaidie kupiga vita imani hii ya kishenzi, na sio kuipigia chapuo.
Kwa hiyo wewe unapinga swala la ndoa, unataka waoto wazaliwe nje ya ndoa na kulelewa nje ya familia? au nyinyi ndo wale ma single mother.....au wale wanaoamini mtoto unaweza kwenda kumnunua au kutengenezewa maabara.
 
Ila naona mambo yako tofauti na zamani naona miaka18 ya enzi zile ni saw na 22 ya sasa Kwa kweli wapo wanawake wengi juu ya 25 hawana watoto na wanaoforce huzalia nyumbani
Na hiki ndo mtoa mada anajaribu kutahadharisha, binti anapopindukia miaka 25 uwezo wake wa kupata ujauzito unaanza kupungua na akija kuolewa ndo purukushani za kusaka mtoto zinaanza.........na huenda kipindi cha nyuma haikuwa tatizo sana lakini kufuatana na mabadiliko ya vinasaba na kimaumbile na mfumo mzima wa maisha hasa kwenye aina ya vyakula inapelekea tatizo kuwa kubwa.
 
Mwanamke wa miaka 18-24 ukimuoa unajitaftia mabalaa tu! Labda ukaolee Muheza huko kijiji cha Amani, ila sio hawa mapaka wa mjini ambao wanasomea IFM ama UDSM ambao wanazurura kwenye ma Bar na ma Club kila weekend untanyooshwa!


😀😀😀😀

Wanawake wanatabia ya kuangalia wanaume wa kuwanyoosha
 
Mila za Afrika za kuaminisha watoto, hasa wa kike, kwamba kuolewa ndio kitu cha muhimu kuliko vyote katika maisha yake ni za kipuuzi.

Ndugu mliofanikiwa kupata mwanga wa elimu, ukiwemo wewe mtoa mada, msaidie kupiga vita imani hii ya kishenzi, na sio kuipigia chapuo.


Sasa bila ndoa unafikiri Mwanadamu anatofauti ipi na mnyama?

Kinachomfanya mwanamke aendelee kuwa wathamani ni uwepo wake ndani ya ndoa,
Hii itamfanya alindwe, aonewe wivu, achungwe, ajaliwe, athaminiwe, aogopwe, ajivunie n.k.
Mambo hayo wanawake ndio huyapenda.

Labda tujidanganye lakini nature siku zote haiongopi.

Ndoa Kwa mwanamke ni muhimu Sana nao wanalijua Hilo.
 
Sasa bila ndoa unafikiri Mwanadamu anatofauti ipi na mnyama?

Kinachomfanya mwanamke aendelee kuwa wathamani ni uwepo wake ndani ya ndoa,
Hii itamfanya alindwe, aonewe wivu, achungwe, ajaliwe, athaminiwe, aogopwe, ajivunie n.k.
Mambo hayo wanawake ndio huyapenda.

Labda tujidanganye lakini nature siku zote haiongopi.

Ndoa Kwa mwanamke ni muhimu Sana nao wanalijua Hilo.
Hilo la mwanadamu kuwa tofauti na mnyama, tuliache kwanza, kisha twende taratibu;

Ni kwa nini mwanamke kuwa thamani ni uwepo wake ndani ya ndoa? Kwani mtu kuwa na thamani maana yake ni nini?

Kwani mwanamke hawezi kuwa na mchango au msaada katika jamii asipokuwa kwenye ndoa? Wanawake waliowahi kuwa na wadhifa na kuitumikia jamii, ili hali hawana ndoa, wapo wengi tu sioni ulazima wa kuwataja, hawana thamani kwenye jamii?

Wanawake walioko kwenye mashirika kama vile ya dini, hawanaga ndoa, lakini wanaanzisha vituo vya kusaidia watu, kulea watoto yatima n.k, hawana thamani kwa kuwa hawako kwenye ndoa?

Wanawake wasomi na wenye ujuzi mbalimbali, maspeshalisti wengine madaktari, hawana thamani kwenye jamii kama tu hawako kwenye ndoa? Na huyo mwanamke alie na ndoa, ana uspesho gani kumshinda asiye na ndoa? Kwa sababu tu anampikia mumewe au ni nini? Yaani ni nini kinachompa uthamani akiwa huko kwenye ndoa?

Na ni nani aliesema kwamba uthamani na utu wa mwanamke ni ndoa, kama siyo jamii hii hii ya watu, tukiwemo mimi na wewe?

Hawa wanawake wanaonekana kupenda ndoa, lakini uhalisia ni kwamba wengi wanavumilia tu kwa kuogopa watu kama wewe ambao watawaona hawana thamani wakitoka kwenye ndoa!
Ndugu yangu ROBERT HERIEL , huwa unafurahia sana ukiona wanawake wanakuwa desperate, wanapata depression, wanateseka na kuhaingaika kwenda kwa waganga, kukesha kwenye maombezi ya upepo wa kisurisuri wakitafuta ndoa, kwa sababu wanaogopa jamii itawaona hawana thamani, kisa tu hawana ndoa?

Ningeomba tuwaonee huruma wanawake kwamba nao ni binadamu, tupige vita imani hii ya kishenzi. Cc Nyumisi
 
Oa mwanamke mwenye umri wa atleast 25 yrs mpaka 29 hapo!
At least wewe umeongea point, nimekuwa muungaji mkono sana wa mada za huyu jamaa juu ya haya mambo, ila sasa naanza kushtuka. Inawezekana jamaa anawachukia wanawake.

Kusema kwamba ndoa ndio jambo la maana kuliko yote katika maisha ya mwanamke, ni kupigia debe unyanyasaji, utumwa, ukatili na mateso wanapitia wanawake kisa tu kulinda ndoa, maana jamii imemuaminisha kuwa ndio kitu cha thamani kuliko chochote.

Ni kusababisha wanawake wanaojiweza, wasomi, wenye nyadhifa na mchango katika jamii wajione hawana maana yeyote, kama hawajaolewa. Hii ni imani ya kikatili, yenye lengo la kutweza na kudhalilisha utu wa mwanamke.

Waungwana wote tunatakiwa kupiga vita imani hii ya kishenzi. Cc Nyumisi
 
Kwa hiyo wewe unapinga swala la ndoa, unataka waoto wazaliwe nje ya ndoa na kulelewa nje ya familia? au nyinyi ndo wale ma single mother.....au wale wanaoamini mtoto unaweza kwenda kumnunua au kutengenezewa maabara.
Ndugu zangu, muwe mnajitahidi basi kusoma kilichoandikwa.

Mimi sijapinga ndoa na wala siwezi kupinga kwa kuwa NI HIARI YA MTU, nimeandika kwa herufi kubwa.

Ninataka ndoa iwe ni hiari ya mtu, kuaminisha jamii kuwa ni kitu cha thamani kuliko vyote ni kujaribu kufanya ndoa iwe ni jambo la lazima. Sijui kama unanielewa kama ulishindwa kuelewa post ya mwanzo.

Kama unadhani umuhimu wa ndoa ni kulea watoto, sikubishii, hayo ni maoni yako. Lakini wengine wanaweza kuwa na maoni tofauti juu ya umuhimu wa ndoa. Nimekuita kwenye post zingine zilizofafanua hili jambo, kama utapenda kunielewa ninachozungumza!
 
Yaani hujapata ujumbe bado mkuu. Akili ni zaidi ya komputa. Una feed data nyingi Sana yenyewe inatoka na jibu moja tu as a information.
Ishu ni kuwa mabinti watafute wenzao kabla umri haujaenda na sio kukimbia na wazee kisa Cha kuwapa mahitaji
Nimemuelewa sana mshikaji Ila tatizo lipo kwenye uhalisia wa Mambo hasa kwa apande zote mbili

Mfano kitu kinaitwa uvumilivu

Mkuu kwa Rika la vijana wengi 18 - 25 au mpaka 29 wengi hawajajipanga na kuweza kumudu mahitaji ya familia na jamii
Hapa uvumilivu unahitajika kwa upande wa kike

Kwa age ya 18 - 25 hapa mwanamke huhitaji kuonekana ni mrembo na huhitaji kuenda na fashion ya dunia

Mkuu nakuuliza swali kabla sijaendelea
Ni Mara ngapi umesikia kuhusu wanawake wa Sasa kuiweka pesa mbele kuliko future za familia zao

Utasikia Hana hela wa Nini mimi

Mchumba anataka kusuka,kuvaa, outing, na baadhi ya vitu ili kuendana na utamaduni wa jamii ya Sasa

Ukizingatia jamaa ni jobless

Mi nashauri vijana wajiimarishe kiuchumi ili kuweza kumudu familia zao sikuizi wanamke wanaolewa kupunguza ukali wa jua kuwawakia
 
Back
Top Bottom