Wanawake wasilalamike kuachwa, wajiangalie tabia zao

Wanawake wasilalamike kuachwa, wajiangalie tabia zao

opondo

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Posts
526
Reaction score
1,321
Nilifungua channel ya Arise and shine Mwamposa alisema ambao wanatafuta mchumba wasimame walikua wengi sanaa.

Nikawa nawaza kwanini sasahivi kundi kubwa la wanaume hawataki kuoa? Na kwanini wanawake wanalalamika hawaolewi na vijana nao wanatafuta mabinti wa kuoa na hawapati?

Kuna vitu nimeona na nimegundua mosi, wanawake sio waaminifu kabisa anaweza kua na wanaume 5 anategeshea yupi atakae muoa kwanza, na bahati mbaya hata yule alie serious anagundua michezo ya huyu binti then kinachofuata ni vilio tu na kulalamika kuachwa (hawaangalii tatizo lao la kutokua muaminifu).

Kutokusikia/kukosa utii.
Kwenye uchumba hata kama mmekaa miaka 6 usiponyesha utii na kutokusikia utaachwa tu, then wakishaachwa wanalalamika na kwenda kwa mganga kuroga mwanaume lakini yeye tatizo lake halioni.

Vijana mkitaka kuoa hakikisha umeoa binti ambae amemaliza kila kitu kwenye maisha yake, ukiona mwanamke haeleweki muache maana silaha yao kubwa hiko kwenye machozi.

Binafsi naona hakuna mwanaume anaeweza kumuacha mwanamke ambae ni msikivu na ametulia.

Niko na binti mmoja wa kinyantuzu wa bariadi naona future hiko nzuri tupo nae mwaka wa pili sasa. Vijanà ukitaka kuoa mwanamke wa kudumu sogea usukumani hapo na amini hutosumbuliwa na hawa wanawake wenye mambo mingi na ujuaji kibao na bahati mbaya wakiachwa hawajui na kutambua makosa yao kazi kulalamika na kuturoga.
 
Bandungu nimeona wanaume wengi ni wanafiki. Kwenye vikao vyetu tunakubaliana tuwagegede na no kuoa lakini mtaani mambo ni tofauti kabisaaa
🤣 Kuna wanaume huwa hawahudhurii kabisa vikao vyenu.
 
Kwa experience yangu.... wanawake wasikivu sana, watulivu sana wenye utii wa hali ya juu wife matirio kabisa ndio wanaongoza kwa kupigwa matukio na zaidi zaidi wengi wao wanazalishwa na kuachwa.
Mchezo hautaki hasira.
Na wanawake vikwekwe wengi ndio wanaolewa hao watulivu wengi bila bila.
 
🤣 Kuna wanaume huwa hawahudhurii kabisa vikao vyenu.
Ata mie nimegundua hawa ndio yakiwakuta huko wanakuja kulia lia hapa JF. Itabidi na mie nichungulie upande wa pili wanapewa nini cha ajabu mpaka kulamba asali hakutoshi wanaamua kuchonga mzinga kabisa
 
Kwa experience yangu.... wanawake wasikivu sana, watulivu sana wenye utii wa hali ya juu wife matirio kabisa ndio wanaongoza kwa kupigwa matukio na zaidi zaidi wengi wao wanazalishwa na kuachwa.
Mchezo hautaki hasira.
Afadhali utusemee.
Ukiwa wife material unapigwa matukio mpaka unabadilika halafu wanakuja kulalamika eti wanawake hawajielewi kumbe mtu kashaathiriwa mpaka kabadilika
 
Na wanawake vikwekwe wengi ndio wanaolewa hao watulivu wengi bila bila.
download.jpeg

A guide for women who are too nice 😃
 
Wanawake wanatamani Sana ndoa uenda kwa waganga na makanisani kuomba ndoa, wakishazipata tu yaani cheti na watoto uanza harakati za kuibomoa ndoa, then ndoa ikishavunjika uanza tena kulia lia kwa Mwamposa, wote kwa Mwamposa pale wengi ni ndoa
 
Nilifungua channel ya Arise and shine Mwamposa alisema ambao wanatafuta mchumba wasimame walikua wengi sanaa.

Nikawa nawaza kwanini sasahivi kundi kubwa la wanaume hawataki kuoa? Na kwanini wanawake wanalalamika

Kwanza kabisa hakuna uchumba wa miaka 6 na kama upo nyie ni wazinzi

Jua kwanza dhana ya uchumba usiite mtu mchumba ako na hujatoa posa wala mahari
Huyo ni mpenzi tu mtazamaji kama wengine… fata proces zote za uchumba kisha useme una mchumba na sio msebule

Uchumba mfupi sana ni miezi 3 wa wastani miezi 6 na mrefu zaidi ni mwaka mmoja tena kuwe na sababu maalumu…
Wanawake tumekubaliana ukizidi mwaka mmoja hakuna ndoa tunaamia kwa aliye tayari

Ni kweli sikupingi siku hizi huwezi kukuta mdada ana mwanaume mmoja hakuna kama ilivo kwenu wakaka hamuwezi kuwa na mmoja na wadada wamezinduka wanawapanga kama foleni japo sio wote

Sababu ni moja wanaume hamueleweki unaweza kumgandisha dada wa watu na usimuoe kama hivyo ulivosema unakaa na mtu miaka 6 alafu unakuja kuoa mwingine….
Sasa lazima kuwe na akiba tukiona huelewekii tunaamia kwingine

Kwanza uwe peke ako wewe baba ake [emoji1787][emoji1787][emoji1787](jokes)
Ila backup ni lazima kwa konkodi wa mapenzi na mnabalanciwa vizuri tu


Ajabu unasema watu hawaoi wakati harusi zimejaa mitaani kila siku uwe unapitiapitia page za kusherehesha haswa kwa Garab kila weekend mtu anaoa mwingine anaolewa

Umebakii wewe na wenzio msiotaka kuoa
 
Back
Top Bottom