RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖Mhadhara (59)✍
Je, wajua?
Wanawake wengi wanakuwa na siku za kununa bila sababu. Bila shaka unaishi na ndugu yako wa kike, mfanyakazi mwenzako wa kike, mkeo, mchumba, au mpenzi wako na huwa kuna siku anaamka amenuna bila sababu (yaani hayuko sawa kama siku zote).
Kama tabia hiyo inajirudia kila mara usiwe na shaka, usidhani kuwa hakupendi, na wala usimfikire vibaya kuhusiana na hiyo tabia. Ni kwa wanawake wengi (hasa wanapoingia kwenye maisha ya majukumu) huwa kuna siku inawatokea wananuna bila sababu. Si kwamba siku ya kununa inafanana kwa wanawake wote, kila mmoja ana siku yake ya kununa na humtokea bila yeye kutarajia.
Wapo wanawake ambao kila wiki wananuna mara moja, wengine kwa wiki mbili au tatu wananuna mara moja. Na kuna wengine kila mwezi wananuna mara moja. Hivyo kama unaishi na ndugu yako wa kike, mkeo, mpenzi, mchumba, au mfanyakazi na ana tabia hii unapaswa kumzoea na kumvumilia.
Right Marker
Dar es salaam