Lighton
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 2,231
- 3,737
tabia ya wanawake kumtegemea mwanaume Kwa 100% imekuwa ni tabia ambaya wameifanya Kama sehemu ya maisha Yao. Unakuta mwanamke anamtegemea mwanaume, boyfriend/mumewe Kwa kila kitu.
Mwanamke wa Aina hii, anajiweka kwenye situation tofauti, either apate kila anachohitaji Kwa mumewe, apate baadhi ya anavyovihitaji, apate kidogo kuliko afadhali au akose kabisa. Tabia hii imefanya wanawake wengi kuingiwa na tamaa mbalimbali na mwishowe kuishia kwenye usaliti.
Kiuhalisia mwanaume hawezi kumtosheleza mwanamke Kwa kila anachokihitaji, labda Kama huyo mwanaume ni Malaika wa mbinguni, Ndiyo maana maandiko yanatueleza sifa za mwanamke mwema(mithali 31:10-mwisho)
Tafsiri ya mwanamke kutolewa Kwenye ubavu wa mwanaume, ni usaidizi, siyo kulea watoto tu, Bali ni kusaidia pia kazi ambazo mwanaume atashindwa kuzifanya pindi anapokuwa na ratiba ngumu.
Ule usaidizi unakuja kwasababu ya upendo, unyenyekevu kwamba Ili Mambo yaende lazima nisaidie Mambo kadhaa. Mwanamke mwenye tabia hii ni mwanamke wa mithali ni mwanamke mwaminifu Kwa mumewe au boyfriend wake.
Siku hizi kumekuwa na usaliti mwingi kwasababu, wanaume wanaona wanawake zao hawatosheki. Ni kweli hawatosheki kwasababu wanawategemea wanaume wao Kwa kila kitu.
Wanawake wa Aina hii ni wanawake wa miaka ya hivi karibuni. Kuna msemo unasema "hata uwe na pesa kiasi gani huwezi kumtosheleza mwanamke" Ni kweli kwasababu yeye mwenyewe hatosheki, kwasababu anafikiri anaweza kutosheka Kwa kila kitu.
Binadamu yoyote hawezi kutosheka, binadamu anatakiwa kuwa na malengo pamoja na kuwekeza juhudi zake kutimiza malengo yake, ni jambo la kupendeza na la faraja kutimiza malengo uliyojiwekea Kwa muda mrefu. Mama zetu wa miaka ya 50s walifanikiwa katika hili, wanawake wenye tabia ya wamama wa miaka 50s wamebaki wachache sana na wengine mpo humu.
Wafundisheni wanawake wenzenu wenye tabia hii.