Mshangazi dot com
JF-Expert Member
- Nov 19, 2011
- 1,345
- 3,503
Ladies habarini za asubuhi, leo utani na masihara ya ushangazi naweka pembeni kidogo.
Nakusihi, tafadhali usikimbilie kuolewa na kuzaa. Chonde chonde, naona kuna nyuzi nyingi humu za kusakama wanawake wa over 30 na kuwaambia namna thamani zao zinavyoshuka kadri umri unavyozidi kwenda.
Hiyo ni perspective ya upande wa wanaume, ila kwetu kama wanawake, hakuna kosa kubwa utakalojutia kama kukimbilia ndoa na kuolewa na mtu ambaye si sahihi. Chukua muda kumfahamu mwenza wako na jitahidi kuolewa na mtu mnayeendana kimaadili, kiutashi na mwenye mapenzi ya kweli ili mkipata watoto wasiteseke. Kisaikolojia, inaathiri sana watoto kukua kwenye dysfunctional homes, nyumba ambazo wazazi hawana maelewano, upendo wala wababa hawashiriki kwenye malezi ya watoto wao. Kuna tafiti za kutosha kwenye hili na wengine waliotoka kwenye hizo nyumba za magomvi tunawaona humu kwenye mitandao wanavyobehave.
Usiogope kumuacha mwanaume kwa hofu ya kutopata mwingine, kama unaona dalili na tabia zisizofaa kabla ya ndoa, jua zitaongezeka mara 10 baada ya kuoana. Tunasikia visa kila siku vya wanawake wenzetu wanavyoteseka, ila tumenormalize sana madhila ya mahusiano mpaka yamekua mambo ya kawaida tu. Baadhi yetu tukiambiwa tutaje wanawake watano kutoka kwenye familia zetu au tunaowafahamu kwa ukaribu wenye furaha kwenye ndoa zao, tunaweza tusiweze.
Maisha yamebadilika, fanya uamuzi ambao ni bora kwako na uzao wako na si kwa sababu utaonekanaje kwenye jamii kama hujaolewa.
Ni hayo tu, nawasilisha!
CC:
Bantu Lady jannelle realMamy Joannah leo dada Qashy Lilith Lamomy
PS:
Yes, nimeishi kwenye ndoa na nina watoto. No, sitajibu maswali zaidi kuhusu maisha yangu binafsi.
📌Chukua nyuzi kama unaona inakufaa kama haikufai, achana nayo 📌.