Wanawake wenzangu njooni tuzungumze kidogo

Wanawake wenzangu njooni tuzungumze kidogo

Najua kikao ni cha wanawake ila kama mfanya usafi wakati nafuta vioo nimeshindwa kujizuia itabidi niseme jambo.

Haya mambo ya changamoto za kisasa za kimahusiano yanasababishwa na vitu vingi sana lakini haiondoi ukweli kuwa nguvu ya mahusiano kudumu ni matokeo ya jitihada za watu wawili tu waliopo katika uhusiano huo.

Kama unataka usiwe topic au kituko cha mahusiano katika umri huo jitafakari sana uliishi vipi kipindi chako cha miaka 16 hadi 26.

Huu ndio umri utakao amua hatima yako ya kimahusiano huko miaka 30 kwenda uzeeni.

Kama ulidanga huo umri then jiandae na matokeo after 30 kwasababu kila unachofanya katika umri huo kinakuja kukuletea malipo yake hata kama ilikuwa ni kwa usiri. Unaweza kuwa ulikuwa unapiga matukio yako kwa kificho sana. Ila siku isiyokuwa na jina kuna yule mshenzi mwenzako atakutafuta na ndipo siri zitajulikana.

Hizi story za usivumilie "this n that" au "usiogope kuachana" ni katika kujitetea tu ila kiuhalisia hapo umeshaanza kulipia hesabu yako.

Maisha baada ya 26 kuelekea 30+ ni maisha ambayo wanawake huwa mnataka kurekebisha makosa na uzembe wenu mliotenda at 16 to 26 prime age. Hautafanikiwa. Shetani akishakupaka shombo lake hakuna sehemu utatoboa kimahusiano. Hapo subiria tu kama MUNGU atakupa neema yake aje kijana mwenye huruma akupe hifadhi ila shida viburi na ujuaji wenu ndivyo vinawakosesha hata hiyo neema ya MUNGU mkishafika huo umri.

Hiki kizazi watoto wa kike sijui nani aliwapa huu mfumo wa maisha mnayoishi. MUNGU awatetee.
 
Mwenzenu kapiga double
 

Attachments

  • IMG-20250204-WA0024.jpg
    IMG-20250204-WA0024.jpg
    174.6 KB · Views: 2
Theresa49 umemaliza yote, umeongea maneno kila mwanamke ayashike yamkae kichwani. Huwa watu husema atabadilika tukioana, jidanganye ni zaidi yake inakuwa. Hapo hana cha kupoteza tena, hii mada imekuja wakati muafaka.

Jana kilitokea kitu, nikasema Mungu ahsante ulijua kuniepusha na huyu jini ningekuwa nalia kila siku. Wadada kingine, ukiona mtu kafanya jambo na roho yako, haimtaki tena, ondoka utakuja kumshukuru Mungu, using'ang'anie mtu.

Tulia, Sali/Swali, tafuta pesa yako, enjoy life, Mungu atakuletea wako, hata kama una miaka 60 ndiyo furaha yako itaanzia hapo itakuwa tu.
 
umeharibu huko sasa unataka ku
Ladies habarini za asubuhi, leo utani na masihara ya ushangazi naweka pembeni kidogo.

Nakusihi, tafadhali usikimbilie kuolewa na kuzaa. Chonde chonde, naona kuna nyuzi nyingi humu za kusakama wanawake wa over 30 na kuwaambia namna thamani zao zinavyoshuka kadri umri unavyozidi kwenda.

Hiyo ni perspective ya upande wa wanaume, ila kwetu kama wanawake, hakuna kosa kubwa utakalojutia kama kukimbilia ndoa na kuolewa na mtu ambaye si sahihi. Chukua muda kumfahamu mwenza wako na jitahidi kuolewa na mtu mnayeendana kimaadili, kiutashi na mwenye mapenzi ya kweli ili mkipata watoto wasiteseke. Kisaikolojia, inaathiri sana watoto kukua kwenye dysfunctional homes, nyumba ambazo wazazi hawana maelewano, upendo wala wababa hawashiriki kwenye malezi ya watoto wao. Kuna tafiti za kutosha kwenye hili na wengine waliotoka kwenye hizo nyumba za magomvi tunawaona humu kwenye mitandao wanavyobehave.

Usiogope kumuacha mwanaume kwa hofu ya kutopata mwingine, kama unaona dalili na tabia zisizofaa kabla ya ndoa, jua zitaongezeka mara 10 baada ya kuoana. Tunasikia visa kila siku vya wanawake wenzetu wanavyoteseka, ila tumenormalize sana madhila ya mahusiano mpaka yamekua mambo ya kawaida tu. Baadhi yetu tukiambiwa tutaje wanawake watano kutoka kwenye familia zetu au tunaowafahamu kwa ukaribu wenye furaha kwenye ndoa zao, tunaweza tusiweze.

Maisha yamebadilika, fanya uamuzi ambao ni bora kwako na uzao wako na si kwa sababu utaonekanaje kwenye jamii kama hujaolewa.

Ni hayo tu, nawasilisha!

CC:
Bantu Lady jannelle realMamy Joannah leo dada Qashy Lilith Lamomy

PS:
Yes, nimeishi kwenye ndoa na nina watoto. No, sitajibu maswali zaidi kuhusu maisha yangu binafsi.

📌Chukua nyuzi kama unaona inakufaa kama haikufai, achana nayo 📌.
umeyaharibu huko sasa unataka kutuharibia watoto wetu, we huna tofauti na mchawi. pambana na hali yako usitafute wafuasi ktk upuuzi huo
 
Hukuona uzi wake kutafuta mtu wa kumkojoza?? Hadi aliandika email yake watu wakaanza kurusha kamba, yeye yuko desperate alaf anashauri wenzie wasiharakie mahusiano!! Atasema matani, matani gan na email alikua anazijibuu?
Single women hawapendi kuona wanawake wengine wanakuwa na mahusiano sababu wanajua kuwa hiyo hali inaweza waua kwa upweke ndio maana wanapambana kutwa kucha kuharibu mitazamo ya wanawake wenzao na kutoa ushauri wa kupotosha wanawake.
 
Watu wanaoweka presha Kwa wanawake humu ni wale ambao maisha yao ya mapenzi ni vuruguvagara ndoa zao zipo kichwa chini miguu juu either wanamkosi kwenye mapenz Kila wanapogusa wanakula vya kichwa Sasa wanaona sehem yakuja kujifariji ni humu JF Ili wapooze mioyo Yao wanaanza kutoa habar negative kuhusu wanawake yaan mtu unaona kabisa huyu Kuna kichwa Cha chuma kimemkuta ndo maana anakuja kutoa povu
Kamwe Sito pelekeshwa na maneno ya humu ndan yaan hata wakitumia viongozi wa dini au vtabu vya din maneno yaoo sio sumu hayaui mtu
pole sana dada
 
umeharibu huko sasa unataka ku

umeyaharibu huko sasa unataka kutuharibia watoto wetu, we huna tofauti na mchawi. pambana na hali yako usitafute wafuasi ktk upuuzi huo
Wameitwa wanawake na wewe umetokea na ID yako inasema jina lako ni Nicholas, halafu unaandika vitu havieleweki. Nani amekuvuruga mapema yote hii?
 
Back
Top Bottom