Wanunuaji TV kuweni makini huko madukani, Mchina sio mtu mzuri kabisa

UZI Haukuwa wa biashara mkuu ndio mana sijaweka picha "makusudi kabisa"

unaiogopa kwanini sasa wakati mlikua mnanikatalia hamna TV za namna hii?

Unahisi sio mchina katengeneza hii TV? nikutoe wasi wasi tu TV ni mchina pure

ila kama ni mchna OG au mchina kanjanja mimi hapo ndo sijui nishaitwa ngosha tena.
 

Huyo fundi kakushauri hivyo kwa sababu 1 kubwa TV za MO electro ndani wanasema zina stabilizer sjui (mi sijui) umeme wa tanesco ukirudi TV haiwaki direct itatulia kama sekunde kadhaa umeme ukiwa sawa ndio TV inawaka kile kitaa pembeni kwa chini.

Tofauti na hzi tv zingine umeme ukirudi wa tanesco tv inawaka pale pale haina kusubiri kwahiyo kuungua tv za MO inavyosemekana ni ngumu kuungua.

ila tukirudi kwenye PICHA asee tv za MO picha zake nikiipambanisha na hii tv ninayoiongelea kwenye hii thread Picha ya MO inasubiri,Picha ya tv ya mo sijaielewa kabisaaaaaa.
 
we wabishie wataalamu TV wakiona comment yko hamna rangi utaacha kuona

Humu ndani kuna wataalamu hao,ukiwambia kitu wabishi tena wabishi haswa.

Wameniambia mimi nimezoea kutumia tv za chogo flat screen niwaachie wao.

Namimi nimewaachia wao,nimeleta TV nimewatangazia Nauza hawataki kununua.
 
Mkuu wangu PETER PIERE nasemaga JF ina watu ila naamini watu walioko JF wanahesabika

waliobaki sijui niwaeke kundi gani,unachosema nakubaliana na wewe wengi humu wanatumia COPY

halafu wanajiweka kwenye kundi la watumia TV mimi sibishani nao tena nilichojifunza ni kwenda nao hvyo hvyo

wamedai hamna TV nimezileta nimewatangazia Kununua hawataki wote wameniacha THANK GOD tv zimeisha
 
Katika pita pita zenu huko mkikutana na huu uwanja wa inch 42 unauzwa bei ya kitonga msije sema hamkutonywa

Brand name : MAISHA

Kwa kweli Awamu ya 5 ataekosa Flat TV ndani kwake hatokaa amiliki Flat tena (natania tu)



 
Je uzi wako ni fursa ya kutangaza biashara? Siuelewi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuweka flat screen ndani brand ya MAISHA, sijui ABORDER, bora ninunue chogo nikae nalo ndani.
Siungi mkono hoja kwamba ili kitu kiwe original sharti kiwe kizito. Hapa wabongo tunakamatika kinoma.
Ndo maana mchina alitukamata na simu za lain mbili kipindi cha 2009 hadi 2014. Mchna na simu zake za OKING, TECNO, NOCKLA( Sio NOKIA) alikuwa anaweka mifuniko ya betri mizitoooooo. Ukibeba siku unajimwambafai kuwa nina simu orijino nzitooo kumbe mfuniko wa betri ndo mzitoo.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚.

Nunua hisence, panasonic, sony, lg, Tcl inch 32 smart tv sio akina MO, maisha takataka toka china.
Mm hata tv za star times sizielewi kabisa
 
Wewe weka no,tukupigie umekomalia pm,pm pm,mimi sjawahi kufika pm weka na kapicha sasa.
 
Hivi ni nini kimempata huyu CONTROLA..? Kapotea sana jukwaani zaidi ya kawaida.
Nipo mkuu,sema siku hizi nasoma sana kuliko kuchangia

mambo tu yananikalia shingoni naogopa kuandika andika

shaka ondoa kabisa nipo salama na asante kwa kunikumbuka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…