Jana nilipokea simu kutoka kwa rafiki angu mmoja (wa kike) akaniita
CONTROLA naomba uje home nisaidie kufunga TV yangu ukutani, nikamtania nikamwambia ''naona umejikakamua umevuta flat, au siyo?'', akanichekea pale basi.
Nikamalizia mambo yangu then nikaenda nikamkuta anaangalia TV. Kweli ilikua ni TV kali sana, Samsung, iko very clear safi kabisa! Basi nikachukua drill langu toboa ukuta andaa matundu then nikafunga bracket, kwisha. Ikafika hatua ya kuchukuwa TV kufunga.
Zile chuma ambazo ndio unazivesha pale ukutani, kwakuwa mtoto wa kike muoga muoga akaniambia
CONTROLA njoo ibebe mwenyewe hii TV nisije idondosha bure, nikaenda kwenye meza kuibeba. Asalaleeee! Jamani eeeeeeh, nasema hivi, kama huna hela ya kununua TV, tulizana.
Aseee nimebeba ile TV siandiki uongo ile TV nina uhakika zaidi ya asilimia 100 haijafika nusu kilo, naongelea 500 grams. TV ni nyepesi hata pasi yangu nyumbani ikiwa haina maji sio nyepesi hivyo kwakweli.
Ikabidi nimuulize hii TV umenunua wapi? akanijibu ''Dodoma.Tena imeni-cost, hivyo ibebe kwa umakini'' Nikamuuliza ''Shilingi ngapi?'', akaniambia ni 470,000. Ilikua ni inch 32. Basi sikumuhoji sana nikampongeza kwa kununua TV yake mpya, akanilipa changu, nikasepa.
Aisee kwa ambao mnawaza kwenda madukani kunua hizo flat TV,waombeni hao wauzaji hata mzibebe muone uzito wake. Nimeulizia ulizia kwa watu wangu niambiwa LG flat, inch 32 Samsung (Chinese products) Mtaa wa Congo zinapatikana kwa dollar 100 hivi (kitu kama 230,000) ila kuna maduka Congo TV wanauza mpaka 200,000 inch 32.
Ndio yaleyale ya Tecno kashajua Wabongo wanataka smartphone zenye display kubwa, kaenda kafyatua mi Tecno ina screen kama kiganja.
Ununuzi mwema wa TV.