Wanunuaji TV kuweni makini huko madukani, Mchina sio mtu mzuri kabisa

Wanunuaji TV kuweni makini huko madukani, Mchina sio mtu mzuri kabisa

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,167
Reaction score
24,129
Jana nilipokea simu kutoka kwa rafiki angu mmoja (wa kike) akaniita CONTROLA naomba uje home nisaidie kufunga TV yangu ukutani, nikamtania nikamwambia ''naona umejikakamua umevuta flat, au siyo?'', akanichekea pale basi.

Nikamalizia mambo yangu then nikaenda nikamkuta anaangalia TV. Kweli ilikua ni TV kali sana, Samsung, iko very clear safi kabisa! Basi nikachukua drill langu toboa ukuta andaa matundu then nikafunga bracket, kwisha. Ikafika hatua ya kuchukuwa TV kufunga.

Zile chuma ambazo ndio unazivesha pale ukutani, kwakuwa mtoto wa kike muoga muoga akaniambia CONTROLA njoo ibebe mwenyewe hii TV nisije idondosha bure, nikaenda kwenye meza kuibeba. Asalaleeee! Jamani eeeeeeh, nasema hivi, kama huna hela ya kununua TV, tulizana.

Aseee nimebeba ile TV siandiki uongo ile TV nina uhakika zaidi ya asilimia 100 haijafika nusu kilo, naongelea 500 grams. TV ni nyepesi hata pasi yangu nyumbani ikiwa haina maji sio nyepesi hivyo kwakweli.

Ikabidi nimuulize hii TV umenunua wapi? akanijibu ''Dodoma.Tena imeni-cost, hivyo ibebe kwa umakini'' Nikamuuliza ''Shilingi ngapi?'', akaniambia ni 470,000. Ilikua ni inch 32. Basi sikumuhoji sana nikampongeza kwa kununua TV yake mpya, akanilipa changu, nikasepa.

Aisee kwa ambao mnawaza kwenda madukani kunua hizo flat TV,waombeni hao wauzaji hata mzibebe muone uzito wake. Nimeulizia ulizia kwa watu wangu niambiwa LG flat, inch 32 Samsung (Chinese products) Mtaa wa Congo zinapatikana kwa dollar 100 hivi (kitu kama 230,000) ila kuna maduka Congo TV wanauza mpaka 200,000 inch 32.

Ndio yaleyale ya Tecno kashajua Wabongo wanataka smartphone zenye display kubwa, kaenda kafyatua mi Tecno ina screen kama kiganja.

Ununuzi mwema wa TV.

UPDATES:

UPDATES:




Tv ambazo niliziongelea hapo JUU nyepesi mithili ya TISSUE nimezileta na ninaziuza,sijaleta nyingi nimekuja na Piece 3 tu Brand name ni LG, zipo 3 na TV zote ni mpya mpya mpya..Unapata ikiwa ndani ya box lake na Remote yake.

Brand new narudia tena TV ni mpya ni mpya,Sina haja ya kutaka kujua ubora wa TV wala uwezo wake kwahiyo naomba nisiulizwe maswali ya ubora wa TV hizi maana mimi sio muuza TV hizi TV nimezinunua kwa hasira walionipa hwa member kwa comment zao na kujifanya wao wanajua sana kuliko wengine

wakwanza huyu hapa

Wewe jombaa ni kiazi sana.
Kwa hio siku hizi vitu original vinapimwa kwa uzito?
Waweke mawe?

Huyo jamaaa yeye ni mjuaji wa TV sasa nataka afahamu kuwa TV copy zipo alifikia kuniambia ninachoandika ni CHAI

Hii ni chai

kibaraka mwingine huyu hapa alijitia mjuaji tv na anauza TV sasa leo TV ninazo njooo ununue kwa 270,000 sio mtu mwingine TV ninazo mimi zipo 3 na ni mpya mpya mpya,Mnapenda sana kujitia mnajua vitu Bogus kabisa,tena wewe ukija uje na 50,000 yangu ina maana wewe TV ntakuuzia kwa 320,000...maana tv nauza 270,000 + 50,000 uliyosema unanipa naomba uje na 320,000

Wewe ni liongo mimi nauza tv kkoo, huwez pata tv 32inch kwa 200,000 kama unapajua njoo nionyeshe nakupa 50,000 bure. Kingine andiko lako lina chumvi kibao. Na tv unayotumia nna uhakika ni ya miaka ya 2002 huko li lcd lizito.

Huyu nae aliniita mimi Ngosha,sawa mimi ni ngosha i hope umeridhika Na ngosha mimi nauza TV hizo hapo juu mpya sh.270,000 Tsh.

CONTROLA Nikisema mtaona napenda ukabila
Ila bila kumung'unya maneno wewe mleta ni ngosha.
Ubora wa kitu unapimwa kwa uzito? Unazungumziaje uzito wa laptop na desktop computer?

Wasalimie Misungwi

Huyu sikumuelewa alikubaliana namimi au alikua ananipinga ila sielewi nataka tu ufahamu mr trabomeka siandikagi thread za kutunga tu yani za kimazingaombwe...Tv nch 32 mpya nauza 250,000 usiniulize nimenunua sh ngapi mpaka niuze 250,000 ila fahamu tu kuwa CONTROLA hafanyi biashara isiyo na faida.

🤣🤣🤣🤣 wee jamaa vipi? Teknologia kila diku inabadilika vitu potable na visivyotumia umeme mwingi ndio vinapewa kipaumbele.


Huyu nae naweza kusema alikurupuka kuniita mshamba nataka ufahamu ushamba sio tatizo ila kuuziwa kitu kisicho bora na ukajiona mjanja huo ndio USHAMBA wenyewe sasa nataka leo uje uniungishe mimi mshamba nina inch 32 LG mpyaaaaaaaaaaaa nauza 270,000 Tsh.


Mleta mada mshamba toka chato ai ikungulyabashashi

Huyu aliniita HAMNAZO oukeiiii nataka kuona wewe mwenye nazo TV ziko hapa nauza 270,000 mpyaaa nauza 270,000 haya wewe ulienazo njooo chukua TV nimekuja nazo kama sampo tu nikiona mnanunua ntawaletea nyingi mpka JF wote muwe na Flat tv ndani mwenu....

we jamaa hamnazo ndo wale w simu nzuri lazima iwe kubwa.

Nikweli sina pesa na kweli mimi ni maskini kapuku bin mlalahoi, ktka kujikwamua na huu umaskini wangu naomba uje uniungishe TV zipo 3 hii inaitwa ROUND ONE (MAJARIBIO) mkizimaliza naenda wafatia mzigo sasa


Ukiona hivyo huna pesa

The one and only member ninae mkubali kimya kimya haya naomba niungishe boss RRONDO nimeleta mzigo ambao uliniambia BOX si lakuangalia cha muhimu ni Control tu,sawa boss sikupingi kabisa ila naomba nisaidie kijana wako nimekuja na TV 3 mpya ndani ya mabox zilo sealed ni inch 32 LED TVmpyaaaaaaaaaaaaaaa Naziuza 270,000 kwa moja
hapo kwenye 270,000 tayari nina faida ya kula ndani hata wiki mbili imagine that boss


TV ina tatizo gani? Kinachotakiwa ni control. Mkuu box linakuharibu.

Huyu ni mtu wa mwisho kum quote ambae amediriki kuniita MUONGO sawa hupendi waongo ila nakuhakikishia tukipimwa damu mimi na wewe damu yangu itakua imezidi yako kwa asilimia 300 kwa jinsi ninavyochukia mtu muongo na mbishi asie na research,wewe ni mbishi na kwa kua umejisema hapa wewe ni mfanya biashra wa TV unanunua tv k.koo bei ya jumla 400,000 mimi naomba leo uje uchukue zangu zipo 3 mpya mpya mpya kwa 270,000 yani nakupa ni wewe tu kwenda kuuza.

Acha. uongo mimi ni mfanyabiashara nanunua Tv kariakoo tena kwa bei ya jumla. Lg na Samsung hazipungui laki 4. Tena hiyo ni bei ya jumla . sembuse huyo dada yako aliyenunua rejareja. Mtu muongo simpendi.


Namalizia kwa kusema mnaweza ona TV nilizipondea lakini leo nimezileta,unaweza ukajiuliza why Je siogopi hasara? yes jibu ni kwamba HASARA naogopa ila nimepiga hesabu zangu kua kwa watu wa JF na huku makazini kwngine wapnda miteremko nadhani zikishndkana kuuzika ntaziuza kwa bei niliyonunulia nina uhakika 20000% zitauzika so hela yangu itarudi tu.

Ndugu zangu mawasiliano yangu yanapatikana PM nitakuelekeza mzigo nimeupeleka wapi wewe utaenda uchukua nina vijana wa kuweza kukuletea mzigo Sehemu ya kukutania mtakutana UBUNGO so kwa wakazi wa Dar ukihitaji kuletewa TV utaweza kuja hadi ubungo stand ya mwendo kasi pale ndani utapokelewa na kijana atakupa TV yako.

TV zipo 3 bei ya kila tv ni Tsh 270,000 ONLY ukubwa wa tv ni inch 32 LED TV.

Bei haipungui hata kidogo naomba tuvumiliane eneo hili la bei usije pm kuanza niambia nikupe punguzo,sijaweka picha Makusudi kwakua huu uzi haukua wa biashara nimeamua tu kuja waambia wabishi kua wasipende kubisha bisha pasipo kua na uhakika wa wakibishacho.


warranty na HIZI TV ni 5minutes

ukishaichukua ukinipa mgongo tusitafutane

yani sitishi mtu ila nasema ukweli na ndivyo nilivyo

Tukimaliza biashara wewe pambana na hali yako

Usije sema sijakwambia hapana THREAD nimeandika kila kitu.



UPDATES
UPDATES
UPDATES


Asanteni wana JamiiForums Hakika nimewapenda kupitia kuniona Ngosha Kupitia niona wakuja lakini leo kwa mara ya kwanza mmenifanya niingize Pesa ambayo sikutegemea wala kuwaza kama nitaingiza siku 1 kwa masaa machache sana..

TV nilizotangaza 3 zimeisha zote Japo hamna mteja alietoka JamiiForums ila nashukuru kwa challenge zenu nmejifunza kitu na asanteni kwa kunipa FURSA nyingine.

Naingia rasmi kwenye hii biashara,Ntakua naleta TV za namna hii kila kwa yeyote atakae hitaji nakaribisha ORDER wewe weka order kimya kimya PM then tv ikifika nakucheki kimya kimya,ukijitangaza humu Shauri lako.

Asanteni endeleeni na ubishi Mungu atupe uhai tu ila kila mzigo ntaoleta Nitaanza u post humu JF.
 
Kuna baadhi ya vitu uzito humaanisha uimara au ubora wa kitu, lakini tukija kwenye vifaa vya electronics kila siku wanajitahidi ziwe na uzito mdogo zaidi.

Sikatai kuwepo kwa vitu fake, nnachopinga ni kulinganisha uzito na ubora wa kitu.

Mfano laptop nyingi sasa hivi zinakuja na battery ndogo sana tena ipo ndani hauitoi kirahisi, vilevile hard disk nazo ni ndogo mno. Hiyo yote kupunguza uzito na ukubwa.

Kwa TV inategemea iwapo ina power supply ndani au ni zile zenye adapter nje kama laptop, ikiwa ni hizo zenye adapter nje kuwa nyepesi ni kawaida.
 
The Monk,
mkuuu hiyo tv inatumia power cable ya namna hii

two-pin-ac-power-cord-cable-laptop-radio-cd-player-charger-ariful99-1712-14-Ariful99@5.jpg


huo waya tu naweza uvuta nikaukata hauna adapter yani kama unavyoona huu waya ndio ile tv sasa
 
Back
Top Bottom