Wanywa pombe kali huwa mnajiuliza swali hili mkiwa mnakunywa?

Aliyekuwmbia situnzi afya yangu kisa pombe ni nani!!?...
Pombe ni sumu, pombe kali ni sumu. Acha pombe, acha kuwatajirisha wenye kampun za pombe huku wewe ukiiacha familia yako kwenye mateso makubwa sababu ya kunywa pombe ama kufa kwa pombe.
Soda sio sumu!?? Vidonge sio sumu!?? ..... Bugia soda acha nibugie gambe .... Afya yangu ni dhamana yangu kama wewe na afya yako ......
 
asilima kubwa matajiri huzaliwa hawana pesa wachache huzirithi na hata hao pia hutumia akili kubwa kuzikuza, sasa point ya utafutaji pesa huanzia chini ukianza tuh visungura kwa kigezo hiki ndio kiwango changu wacha nilewe nakuhakikishia hutafika wine,na ukifika kiwango cha mvinyo wa bei ghali hutopata muda wakunywa au pengine ukapata huo muda mara moja kwa mwaka tena kwa kiwango kidogo hivyo hakuna tajiri mlevi kwani huo muda hana wakulewa
 
Je kinachodhuru mwili ni pombe pekeyake?
Tumefunzwa kila kitu kwa kiasi.. Chochote kikizidi kiwango ni sumu
Walokole/wasabato Wana shida sana ..... Yanajiona tayari yameshafika mbinguni Kwa kutokunywa pombe tu ... Na wazima wa afya Kwa kutokunywa pombe tu ..... Madhambi na masumu ni mengi mno duniani humu ...ila wao kila siku kufungua Uzi pombeee pombeee ....
 
Unataka kumuona tajiri akiwa barabarani amelewa chakari?
 
Muda Fulani msongo na kukata tamaa ya kufanikiwa zaidi hupelekea Hali hizo, but Mimi binafsi kuacha pombe kazi ipo, nahofia kopoteza kundi kubwa la marafiki


Kwa mfano leo wewe na mimi tumekufa, lakini wewe umekufa huku maini yako bado mazuri sana, na mimi nimekufa huku yangu yana matobo kisa pombe, MAINI YAKO MAZIMA HUKU UKIWA UMEKUFA YANA FAIDA GANI TENA?
Mhhh we jamaa noma
 
Wewe unafikiri wenye viwanda vya Coca-Cola na Pepsi hawana majumba na magari?
Bure kabisa wewe
 
Umaskin mkubwa sana mkuu..
Ila wenye kampun hizo za pombe wanaendelea kua matajiri, juzi kuna mmoja kanunua gari ya milioni 700 na wako huko.kwenye mitandao.wanayaonesha mafanikio yao makubwa
Hili jambo hua linanikasirisha sana
nakubaliana na wewe ukitaka kuwa tajiri wekeza kwenye pombe huko kuna kundi kubwa la wapumbavu
 
Usitufokee wewe jitunze uende na maini yako mazuri mbinguni
 
Muhimu diko mkali. Unaonaga wapi mlevi na hospitali tena wa hayo makali
 
Mkuu
Duniani tunapita tu.. Unataka utunze hizo figo na maini ili uende nayo wapi?
Mwisho wa siku kila mtu atakufa unataka ufe ukiwa na figo nzima ili uende nazo wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ