Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja

Huu ni uchonganishi, samahani uchochezi.
 
Well said ndugu Pasco. Lakini nani ataitisha hiyo kura ya maoni? Maana mtu mmoja aliwahi kusema "usiitishe kura ya maoni kama una uhakika wa kushinda."

Nionavyo mimi ni kwamba kwa sasa mtu anayetakiwa kuanzishwa na kusimamia jambo hili hana uhakika wa kushinda. Kwa hali ya Zanzibar ilivyo sasa, kuanzisha kura ya maoni kuhusu muungano ni sawa na kufukua makaburi. Acha tu "makaburi yapumzike".
 
Tukimaliza Zanzibar nataka kura ya makabila.
Ni lini makabila yetu yalikubaliana uwepo wa Tanganyika?
Mkataba wa makabila kuunda Tanganyika uko wapi?
 
Mwenye maamlaka ya kuitisha kura ya maoni ni serikali . Serikali ya CCM kwame haiwezi kuitisha kura ya maoni kuhusu Muungano. Ni hapo tu gharama za Muungano zitakuwa too costly ndipo Tanganyika itaachia Zanzibar. Too costly maana yake umwagikaji wa damu ya wanzibari hadi mataifa makuu kuinglia kati. East Timor ni funzo kwa wanzibari.
 
Wananchi wa Zanzibar hawana haki ya kujiuliza kuwa wanataka muungano au hawataki kwa kuwa hata huu Muungano ulipoundwa hawakuulizwa kama wanataka Muungano au hawataki.
Anayebisha atafute muda asome historia.

Waingereza waliamua kuingia Euro na sasa wanaamua kutoka. Hii ni tofauti ya Zanzibar na Muungano wa Tanzania
 
Twisted logic. Every man has God given right to determine his destiny. CCM ipende isipende.
 
Dahhhh Pasco I hope kuna mtu kutoka serikalini
Atasoma na kufikisha huu ujumbe wako mahali
Hoja nzito.
 
Mko poa tu kwa vile nyie ndio watawala. Uongo muungano haukuumizini msingekuwa wakali kwa wazanzibari wanaoukataa Muungano. Zanzibar ina Katiba yake na hakuna katiba supreme dhidi ya nyengine. Neno zuri la kusema Katiba zinakinzana
Huo "utawala" wa Tanganyika juu ya Zanzibar haumsadii chochote Mtanganyika na wala hauwezi kutuhadaa tusione mzigo tunaoubeba.

Watanganyika tusikubali ka Zanzibar haka katukwamishe mambo yetu, kametunyima Katiba Mpya haka, tumekwama kupitisha masuala yetu muhimu ya kitaifa kwa sababu ya "muundo wa Muungano." Mbona tuliweza kujivua brainwashing nyingine za Nyerere kama Azimio la Arusha na Chama kimoja, kwa nini hili li ndumba la Muungano tunashindwa na mwenyewe ashakufa? I don't understand this baloney for the life of me.

Nyerere alisema nchi kubwa zinaungana sisi tunataka kutengana, well, Nyerere has been proven wrong in Europe, Waingereza wamesema miungano sio yote ina manufaa, miungano ya kijinga jinga ya wadogo kuungana na kuwanyonya wakubwa haina faida.

Barack Obama alivyokwenda UK kuwaasa wabaki EU, Boris Johnson akamwambia, wewe Obama, there's no way in hell America ingekubali kubanwa kwenye ki muungano kama hiki cha kuamuliwa mambo na nchi nyingine, noooo way! Which is true, US inashadadia Mahakama ya the Hague lakini yenyewe haimo!

Tanganyika, sio Zanzibar, sisi Tanganyika hatutaki Muungano, I don't give a monkey's what Zanzibar thinks, na hatuwasubiri Wazanzibar waamue au watuamulie, sisi Tanganyika tumechoka kunyonywa, tunataka kujitoa!
 
Twisted logic. Every man has God given right to determine his destiny. CCM ipende isipende.

It's a wrapped logic, which is in fact leaving the Zanzibaris and Tanganyikans ( if they exist) in the middle of nowhere to decide their fate.
God given right is universally accepted and doctrinally true however millions are denied those rights by those who rule over them.
 
Tanganyika, sio Zanzibar, sisi Tanganyika, I don't give a monkey's what Zanzibar thinks na hatuwasubiri Wazanzibar waamue au watuamulie, sisi Tanganyika tumechoka kunyonywa, tunataka kujitoa!
Huo ni Ubunuwasi wa kutufanya wazanzibari tuzidi kuendelea kukuroma wakati Tanganyika inazidi kula uroda! Janja hiyo imepitwa na wakati. Zanzibar tunataka nchi yetu
 
Ni kweli, lakini kama wananchi hawakuhusika hasa upande wa Zanzibar ambao ulikuwa hauna kiongozi aliechaguliwa na wananchi wenyewe kinyume na bara inatafsirika kuwa Zanzibar ni koloni la bara. HIvyo kudai uhuru kuutoka kwa mkoloni huyu mweusi si kosa na ni haki.
 
Mungu apishe mbali
 

Upo sahihi Kabisa.
Ukipita kwenye vikao vya raia huko Unguja( JAWS CORNER IN PARTICULAR) watu wanaelewa vizuri Sana juu ya Muumgano huu lakini hawana namna ya kuitisha hicho kinachoitwa "kura ya maoni" ili kuamua hatma Yao.
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…