Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja

 
Wazanzibar wengi hawajui wanataka nini. trust me. wapo hivyo.... hata wakipitisha hiyo kura ya maoni wenyewe kwa wenyewe watasalitiana. Mfano mzuri tu kwenye maoni ya katiba mpya na pia hata kwenye Bunge la Katiba utaona ni wanafiki sana. Wazanzibar wanapenda kuwa na jambo la kuzungumzia kwa muda mrefu na libaki kuwa hilo hilo. nimekaa nao nawafaham yaani hawatak jambo lishe. isipokuwa kama hilo jambo laleta madhara kwao ndo watasema bore lishe. TANGANYIKA TUTAWAUNGA TU watake wastake. Tutawaunga.
 
Na ni watu wa kubadilika badilika.

Leo wanasema wanaogopa majeshi vinginevyo wangekuwa na kura ya maoni! Walipokaa mwaka 2010 hawakuogopa mabomu! Nani aliwasumbua?

Halafu wanasema eti wanataka muungano wa mkataba

Hivi nani amewapa mamlaka ya kuamua aina ya muungano!
Kwa nguvu gani na umuhimu gani wanaweza kusema wanataka abcd

Tunajua kwa huu muungano wao ni mzigo tu.
Hawana hoja nyingine zaidi ya kutaka mablaozi na mafao tu

Utashangaa wanasema hawataki muungano, lakini wanataka mkataba

Tunasema hivi mkataba na ZNZ utakuwa kupitia EAC. Period

Wakitaka waondoke wazima wazima, na hawana sababu za kusubiri.
Wabunge wao wasije Dodoma, wamwite makamu wa Rais, na wale zaidi ya laki 6 warudi kwao tu. Muungano wasioutaka utafikia mwisho

Tumechoka na kelele za kila siku, majukumu yakiweka wanakimbia!

Ni wakati wznz sasa wazungumzie majukumu n.k. si kila siku kulalamaaa tuu , tunataka, tupewe n.k. Wakiambiwa jukumu hata dogo wanakimbia, hawawezi

Wanataka mabalozi, hawawezi kulipia wabunge wao wanaokuja Dodoma!
Wakitaka mabalozi wapewe na wizara nzima ya mambo ya nje kuhudumia.
 
Huo ni Ubunuwasi wa kutufanya wazanzibari tuzidi kuendelea kukuroma wakati Tanganyika inazidi kula uroda! Janja hiyo imepitwa na wakati. Zanzibar tunataka nchi yetu
Uroda upi, taja mmoja!

Taja kitu kimoja ambacho Tanganyika ina benefit toka Zanzibar!

UK inatokana na muungano wa England, Scotland, Wales na Ireland
Ireland haipo UK
 
Uroda upi, taja mmoja!

Taja kitu kimoja ambacho Tanganyika ina benefit toka Zanzibar!

Ireland haipo UK
1. kutumia bure miundombinu ya bahari kwa dahari -Zanzibar Channel
2.Kukitumia bure kwa shughuli za kitalii na katika uchotaji wa mafuta na gesi kisiwa cha Latham(Fungu Kizimkazi)
3. kushindwa kulipa madeni ya Zanzibar katika mgawanyo wa EAC iliokufa - orodha ni refu
 
Pasco umejitahidi kueleza vema kwenye hili bandiko lako lkn umeharibu padogo ya kuwaeleza wapige kura ya kuamua, hivi ktk hii serkali ya ccm inayo lazimisha huu muungano unategemea hata kura zikipigwa watawala wapo tayari kukubali?
 
Ahsante sana ndugu kwa kusaidia uelewa wangu, hakika umeifanya siku yangu ya jumapili kuwa ya afya na baraka tele
Ni sawa tu na kumeza dawa ya usingizi tu maanq watawala kamwe hawapo tayari kwa mabadiliko yanayo piganiwa
 
Kwahiyo huo mwiba wa kesy ni wa kujenga au kubomoa? Yeye anqchofanya ni kucheza na akili za wapiga kura wake tu ili aonekane anachangia kitu bungeni
 
Kuamua kuichagua CCM kwa zaid ya 90% kwny uchaguzi wa March 20,2016 ni ushahid tosha wanahitaji kuendelea na Serikal mbili kwny Muungano wetu.
Mtu kuwa kichaa siyo lazima uvae chupi kichwani bali ni pamoja na kuwa na mawazo dhaifu kama haya yako
 
hamuko tayari Tanganyika, Warioba alikwisha yaweka sawa haya mukayapindua mukaweka yenu. Kama nyinyi munanyonywa na mtoto keshapea unatakiwa umuachishe uangalie jengine sio umlazimishe wakati kashapea muache aanze maisha yako, msitafune huku munapuliza
 
Znz wanajitambua toka kitambo,na walisha amua,titizo lipo kwa huyu MKOLONI mweusi TANGANYIKA aliyejivika koti la TANZANIA tena mchana wa jua kali bila kuona hata JOTO
 
One day yes
Mkuu Kakke, japo heading haiendani na maudhui, lakini kelele za vitimbakwiri wa Zanzibar wanaotaka huu muungano wetu adhimu uvunjike, tumeisha wazoea.

Mabadiliko ya 10 ya katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yameitangaza Zanzibar kuwa ni nchi, na ikaitaja mipaka yake, bendera yake na wimbo wake wa taifa, nayo ikaelezwa kuwa ni dola, ina vyombo vyake vya dola, rais wa Zanzibar ni Amiri Jeshi wa Vikosi vya ile migambo ya KMKM na JKU. Zanzibar ilichokosa ni sarafu yake tuu, mabalozi wake na hati ya kusafiria.

Kwa vile Zanzibar tayari mnayo sheria ya kura ya maoni, then kwa nini msipige kura ya maoni na kuamua to walk out kwa amani?!.

Niliwahi kuashauri hapa

Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja!.

Paskali
 
Hakuna namna yoyote ile tutaweza kuicha Zanzibar ijitenge na kuwa taifa. Ni eneo muhimu sana kimkakati hasa ulinzi na usalama wetu

Sent from my Lenovo A2010-a using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…