Wapalestina Gaza wagaragazwa wenzao wanaangalia tu. Huu ni unyama

Wapalestina Gaza wagaragazwa wenzao wanaangalia tu. Huu ni unyama

Hizo nchi za kiarabu hata zikiungana zote bado zitabaki sio chochote wala lolote kwa hizo nchi za wazungu.

Tukubali kuwa wazungu walishatangulia kitambo na bado anatuongoza huku mwendo wao ni wakukimbia wakati sisi tunaoongozwa mwendo wetu ni wakutembea.

Huyo Irani sio chochote kabisa na misaada anayoitoa kwa waarabu wenzake ni ile misaada ya kijambazi ambayo haitawaendeleza wenzao badala yake inawatengenezea uhasama na chuki dhidi ya nchi zingine kitu ambacho kinakuja kuwapelekea wapokee kipigo cha mbwa mwizi kama Palestina
Waarabu wakiungana wiki tu hutasikia NATO EU wala upuuzi gani
Iran hua inawaspoti wanyonge daima safi sana Iran
 
Unashindwa kupata mantiki ya maandiko kama haya.Hatupo kwa ajili ya kulia lia kama unavyodhani.
Hii habari unahusu ubinadamu na unyama
Tukishindwa kuonesha ubinadamu wetu basi tunaweza kugeuzwa wanyama kabisa na si sisi tu bali na nyinyi pia mtaumia au tuseme tutadhurika sote kwa pamoja.
Asante mkuu nimekuelewa.
 
Kwenye andiko lako mkuu, limenihudhunisha sana mkuu, hata hivyo, Wayahudi waachwe tu wasichokozwe tena na ili amani iendelee kutawala

Hao majamaa, walishapitia madhila mengi mno katika historia yao, kunyanyasa, kuuwa na kutokuwa na huruma, wanaweza na ndivyo walivyo, wao wanaimani kali saana kushinda itikadi zote za imani duniani

Na lingine, hayo majamaaa, kwa tekinolojia yako juuu sanakulikoni watu wote duniani
Nashukuru kuwa umenielewa na kuungana na mimi katika huzuni.Nilipokuwa nikiandika hicho kipande katikati yake nilisimama nikalia halafu ndio nikapata nguvu kuandika.
Nilijenga hisia za wale watu wazima walivyovamia bekari iliyopigwa bomu kwa makusudi ili watu wasile na wakaokota mikate iliyokuwa tayari na wengine kuondoka na vifaa vilivyobaki kwenda navyo huko waendako.Nilijenga hisia kuwa hata hicho walichookota huenda wasiwahi kukila na wakapigwa bomu wakafa.
Nikaangalia ule msururu wa akinamama na watoto wao ambao hata katka shida hiyo huwa wanajisitiri kulinda imani ya dini yao na wengine wakiona watoto wao wameshakufa wanapiga kelele lakini zinakwenda wapi.Sikuweza kuendelea nikalia tena.
Hapo mwisho ndio tumetofautiana mimi na wewe.Mimi siamini kuwa Israel inabaki pale kwa teknolojia.HIzi teknolojia za kisasa ndizo zitakazowafanya wawaheshimu binadamu wenzao.Teknolojia za coding na hacking na AI hakuna atakayekuwa mwamba huko tuendako.
kinachowafanya vile vile wabaki ni roho mbaya kutokana na dini yao ambayo imeshapitwa na muda hata kuliko ukristo.Kama wao wanakumbuka madhila waliyopata kwanini hawakumbuki madhila ya wenzao.Wamekataa kata kata kuundwa taifa la wapalestina watakaloishi nalo jirana.Wanafikiria roho zao peke yao.Kwa hali hii makundi kama Hamas ambayo hata wafanye nini hawataweza kuyamalizan ndiyo yaakayoifanya itie akili na kujua kuwa wao pia ni binadamu na si wateule wa Mungu.
 
Watu waliokuwa na utajiri na familia zao mara wanajikuta wamebaki wapweke na hata mikoba ya akiba zao imewapotea na wanajikuta omba omba na waokotaji kwenye magofu ili wapate cha kula bila kuchagua ubora.
Funzo kubwa sana....Mwenyezi Mungu usiwapite watu wako vitani....Mwenyezi Mungu tunaomba endelea kuilinda Tanzania🙏
 
U
Inashangaza sana kuwa binadamu sasa wamekuwa na roho za kinyama sana kwa sababu wanyama ndio ambao mwenzao akiliwa wanakuwa na msaada mdogo sana japokuwa kwa umoja wao wangeamua wangeweza kumuokoa.

Kinachotokea Gaza kinalingana sana na unyama.Kiwango cha vifo vya wapalestina na kujeruhiwa ni kikubwa sana na huenda haijawahi kutokea katika dunia tangu kuumbwa kwake.Kule Hiroshima na Nagasaki wajapani walikufa wengi kwa mpigo lakini kutokana na aina ya silaha iliyotumika hata watu hawakuona mateso yale kiasi kwamba wangelaumiwa kwa kutokutoa msaada kwa wenzao.

Pale Gaza hali ni tofauti sana kwani Israel ni taifa lenye silaha nyingi za kisasa ikipigana na Hamas ambao ni wanamgambo silaha yao kubwa ikiwa ni RPG na makombora yanayoruka hewani kwa mfumo wa kizamani.Silaha nyengine inayowasaidia na kuwasukuma mbele Hamas ni kujua madhila yaliyowakuta wazazi wao na wenyewe ambayo wameona hakuna njia nyengine isipokuwa ni kufa huku wakijitetea badala ya kufa kitandani.

Muhimu tunachokizungumzia hapa ni vile ambavyo Israel inapiga na kuua na kujeruhi wanawake na watoto mpaka wagonjwa na kuvunja majumba yao waliyojenga kwa shida.

Wengine waliobaki hai mwanzoni walitakiwa wahamie kusini,maskini wengi wakatiii amri hiyo,lakini hii ilikuwa kama kuwacheleweshea adhabu zao au kuwapunguzia kwa wakati huo kwani hawakuwachwa huru moja kwa moja kutokana na mashambulizi hayo.

Baada ya muda sasa Israel imekuja kusini na kuwataka hata wale walio katikati nao wazidi kuelekea kusini mpakani na Misri.Maskini wapalestina wa rika zote wametii japo haikuwasaidia chochote kwani makombora yanaendelea kupigwa na kuuliwa kwa idadi kubwa kila siku.

Watu waliokuwa na utajiri na familia zao mara wanajikuta wamebaki wapweke na hata mikoba ya akiba zao imewapotea na wanajikuta omba omba na waokotaji kwenye magofu ili wapate cha kula bila kuchagua ubora.
Katika hali hiyo ya kusongamana kwenye kambi za wakimbizi au kwa ndugu waliobaki na majumba bado wapalesina hao wanatakiwa hapo walipo waende mashariki au magharibi ili itoe nafasi ya kuvurugwa muda mfupi ujao.kwa kisingizio kuwa hapo walipo kuna Hamas.Maskini wote wanatii na kukimbia bila kutaka kufanya mjadala kuwa hawajawaona hao Hamas.Wanafanya hivyo kwa kujua kuwa ikisemwa hivyo kinachofuata ni makombora ya kusambaratisha kila kitu.

Wakipata amri kama hizo ama kwa vipeperushi au namna nyengineyo wapalestina hukimbizana kwa miguu au kwa gari za punda ambazo wachache wamebaki nazo. Hata hivyo wale wanaochelewa kidogo hupatikana viungo vyao tu vilivyotapakaa baada ya kufa kwa mabomu.

Muhimu zaidi tunachotaka kukieleza ni kuwa huo ukatili unaofanyika unafanywa mbele ya macho ya walimwengu wote wa makabila na dini zote. Ukiondoa hisia za kidini basi kiubinadamu tu basi isingepaswa kufanyika mbele ya binadamu wengine.

Kama ni lawama basi tukisema tulaumu hizo lawama zitaanza kwa watu wenye imani moja na wapalestina ambayo ni uislamu na ambayo ni dini karibu ya raia wote wanaoizunguka Palestina na Israel kwa ujumla.Hiyo ndiyo dini ya viongozi wa nchi hizo.

Matendo ya kuuliwa na kuchomewa majumba waislamu wala hayapo na hayajaanza Palestina na Gaza yake pekee.Hayo yamefanyika sana India,Myamar na China.Japo kuna mengi yangeweza kufanyika kuokoa hali zile lalini kule yawezekana ikasemwa ni mbali na hata hayakuwa yakioneshwa wazi wazi.

Haya yanayofanyika Gaza katikati ya ndugu zao na bila kuchukua hatua yoyote ile hakuna namna ya kuyaelezea isipokuwa ni unyama ambao umeingia ndani ya mioyo ya binadamu.

Kuna wenye nyoyo za kinyama ambao wanaweza wakaleta maneno ya kejeli kwa kisingizio kuwa piga Hamas haoo! eti kwa vile walishambulia oktoba 7.Ukiondoa hisia za kinyama na mtuj akabaki na ubindadamu wake basi kwa kuangalia historia hakuna sababu ya kuilaumu Hamas kwa kushambulia na wala haipasi kuwalaumu kwa kutokuwa tayari kusalimu amri.

Lawama kubwa itabaki kwa unyama ulioingia ndani ya nyoyo za binadamu wa karne hizi zinazokariibiana na kiama.Kwa hali hiyo kama litatokea la kutokea kwa unyama wa binadamu basi asilaumu hali ya tabia nchi wala nini isipokuwa abaki kujutia na kulaumu nafisi yake aliyoibadilisha na kuwa ya kinyama.

View attachment 2833477 View attachment 2833479 View attachment 2833489 View attachment 2833481 View attachment 2833485 View attachment 2833487 View attachment 2833488 View attachment 2833491
Umeandika vizuri sana ndugu kwa hili pia nakuunga mkono Ila kinachotokea pale ni mgogoro wa aridhi sio mgogoro wa kiimani kama ilivyo kwa waislamu wa china, India au mymar sema ni vile tu wenzetu mmegoma kumtofautisha waarabu na uislam,
Ila kiukweli kwakinachoendelea pale kati saiv hata television nimeacha kuangalia habar za middle east nashindwa kuvumilia kuangalia watoto wanavyosafa halafu Dunia imekula buyu as noting ah gwan
 
Mwenye akili ya kibinadamu wala hachanganyikiwi.Kwa sasa tunazungumza habari ya hisia za kinyama.
Kama ni kipigo basi Israel haiwezi kukiepuka na kama hakikutolewa na binadamu na majirani zake basi kitatoka kwa yule ambaye pigo lake ni la ajabu na sio la ukatili kama ule wa Gaza.
Sasa hueleweki. Inawezekana umechanganyikiwa. Mpaka sasa israel tumewapiga au bado? Nijue moja
 
Kwanini hata sasa Hamas wasisalimu amri tu ili kuokoa maisha ya wapalestina kuendelea kupotea?

Mleta mada anza kuwaza katika angle hiyo ikiwa kweli unawapenda wanawake na watoto wanaoteketea Gaza.
 
Kesho wakija wanaoitwa Pro Palestinians wakifadhiliwa na watu wasiopenda Israel wataacha kuwa magaidi ? Ndio maana nikakwambia ukipigana vita na Jeshi unajua nani wa kumaliza ukipigana vita ambavyo ni ideology, unapigana na invisible enemy kwahio mabavu ni last resort sio mzuizi...;

Mfano Osama waliopiga Ubalozi wa Tanzania na Kenya hata Osama walikutana nae ?; Watu wanaopigana kwa Jina la Muumba wao Je ni kweli Muumba wao anahitaji msaada ?; Hivyo utaona kwamba hao watu na wengine wote wakikemea kwamba Kumaliza Raia mmoja haina justification ya aina yoyote au sababu hawa wanataka Taifa lao Huru la Palestina wakiwapa hilo Taifa huenda wakiendelea kudai wataonekana ni wakorofi (Kama ambavyo kila mtu ali-condemn Ubalozi wa Kenya na Tanzania ulivyopigwa Bomu)
Hamas nia yao ni kuifuta Israeli. Sasa unataka wayahudi wajadili nini hapo?!
Wewe unaweza kujadiliana na mtu anaetaka kukuua?
 
Natumia fake id kama unavyotumia wewe Mpaji mungu 😛
😁 Mwisho wa siku Kuna Watu Wana nguvu kuliko ww wanaweza kukufanya chochote na hamna kitu utafanya.....njoo ubishe mfano rahis tu umepewa access ya kutumia fake Id na mtu mwenye nguvu ili uwe free kusema chochote bila kudhurika na watu wenye nguvu kuliko ww
 
Hamas nia yao ni kuifuta Israeli. Sasa unataka wayahudi wajadili nini hapo?!
Wewe unaweza kujadiliana na mtu anaetaka kukuua?
Hamas according to you (unasema kwamba wanataka kuifuta Israel) Jambo ambalo Hamas wanawaambia watu wanaotaka kuwa-recruit tunataka kuwapa Taifa lenu ambalo lipo occupied..., Sidhani kama HAMAS wangesema tuungeni tufaifute Israel wangepata watu (Au wale watoto wanaozaliwa sasa hivi na nyumba zao kupigwa mabomu usiku na mchana ukiwauliza adui ni nani unadhani watakwambia nini au kesho wataenda kujiunga na hao the lesser of the two evils (according to where they stand)

1701790055890.png

Yaani hapo wewe kama recruiter wala hauhitaji maneno mengi..., Now tell me nani anataka kumfuta nani ?
 
Magaidi ni hamas wakifadhiliwa na Iran
Wewe bado Una lala huja amka usingizini,unamjua gaidi kweli 11 September ulikuwa na umri gani kijana ,Nani alimuua muammar gadaf vita vya Iraq vita vya Syria vita vya Vietnam iroshima na Nagasaki vita vya wanyarwanda wenyewe kwa wenyewe chanzo unakijuwa na Kwa nini waliuwana ilikuwa ilikuwa ni préparation War ya kuingiya Congo wewe unalijuwa hili ao unaandika tu ilimradi na wewe uwandike .vijana mjifunze kungamua mambo Kwa mtazamo mwingine Ila nacho kwambia hii ni vita ya 3 ya dunia uamini usiamini maana kuna kitu kinaitwa new world order na Muda ni kama umekwisha ndo maana karibia dunia nzima kuna vita ni mpango wakupinguza watu duniani na wewe ukiwa ndani mana yake hapa hakuna alie kuwa Salama wenzako Wana maono Yao na Yale unayo yaona kwenye TV Unayo skia kwenye radio ni moja kati ya matango Pori wanayo lishwa wa vivu wa kungamuwa mambo makubwa .mzayu na mshirika wake marekani Hao ndio wanataka kuitawala dunia na kumkaribisha antichrist kuwa makini Sana Kwa kuangalia mambo.lakini Sawa Hamas ni gaidi Israël anacho kifanya kuuwa watoto wa mama na watu wazima wa sio kuwa na hatia wewe unaona ni Sawa na moyo wako unafurahia kuwa na moyo wa kibinaadam wale wanaopigwa ni watu kama wewe wanayo Haki ya kuishi na mungu yupo anaona
 
Alwaz umeandika mada yako Kwa uchungu mkubwa Sana mara nyingi huwa nasoma mada zako ila leo naona upo deep Sana.
Huu uchungu ulio nao umenikuta nami pia juzi baada ya Israel kupiga kambi ya wakimbizi kwa siku mbili mfululizo nilikuwa naangalia watoto wadogo kama wanangu jinsi wanavyokufa na kupoteza wazazi wao kwa kweli inaumiza

Kwa upande Fulani hizi shida ambazo wapalestina wanapata zinatokana na waarabu wenzao wenye nguvu Kati ya Iran na Saudi Arabia kutoelewana kiimani,kiitikadi na kisiasa, ebu fikiria hawa jamaa wangekuwa ni kitu kimoja kama ilivyo USA na nchi za magharibi hii dunia ya waarabu ingekuaje? Ni nchi Ipi ingeweza kugusa muunganiko wao kiuchumi,kijeshi na usalama?

Tatizo kubwa la waarabu ni kubaguana wao kwa wao Kwa misingi ya kiimani Kwa kifupi hawana tofauti na Sisi waafrica... angalia jinsi wazungu walivyoweza kuwagawa waarabu kiuchumi yaani zile nchi zote ambazo wazungu ni marafiki wao ziko vizuri kwa kila sekta na zile ambazo Iran anazisaidia ni vita tupu
Bro shida ina kuja sehem moja haya unayo yaona Leo ni mikakati na mipango ya muda mrefu walio panga mayahudi walijuwa iko Siku moja tutakuja kusimama na kuitawala dunia sio mwarabu tu hii kitu IPO karibia dunia nzima kuna mikataba uchwara walisha signishwa inchi kibao Kwa faida Yao na Leo hii wako natekeleza waone kama wanaweza kwenda na speed ya new world order na muda ni kama umabakia mchache.


Ukitazama vizuri utaona ni kama karibia inchi nyingi ziko na vita,na ukiusoma mchezo vizuri utagunduwa nyuma ya pazia America IPO mkuu
 
Raia wote wa gaza wana asili ya ugaidi

Wamalizwe tu
Hahahhh Afghanistan Kiko wapi Leo Israël anacho kifanya kuuwa civilian wasio kuwa na hatia ndio mwisho wake,alaf kingine hii vita haishi Leo ao kesho mkuu hata 50 years plus anavouwa raia watoto wadogo wa mama wazee ana zalisha wakina Hamas wengi na uadui mwingi hawezi kuwa salama
 
Na watu kama nyie ndio mnaupa Uislamu a Bad Name..., na kuwapa fursa ya kuwa-brush waisalamu wote kwamba wana fikra kama zako....

Ni mpuuzi pekee anayeishi kwenye dunia ambayo ni multicultural kutaka watu wote wawe kama yeye...
Mkuu Acha kutowa povu hujalazimishwa kuwa mu islam amekwambia wenzio kutokana na mambo yanayo endeleya Gaza wamepata fursa ya kujifunza uislam ni Nini ,lakini sio lazima Uwe mwislam
 
Back
Top Bottom