Wapalestina Gaza wagaragazwa wenzao wanaangalia tu. Huu ni unyama

Hata sijui unaongea nini na wakati Palestine inakaliwa kimabavu na Israel. Unaongea vitu gani mkuu? Ebu pitia ulichoandika kwa utulivu uone kama kina make sense.
 
Na huyo aliye na nguvu Si naye kapewa Kama Mimi na yuko wa kuziondosha hizo nguvu? Mbona tembo huuliwa na chura
. Juzi hapa tuliona ulimwengu. mzima ukiwa katika taharuki, wenye nguvu wakifunga miji na kuwafungia ndani watu wake na maelfu kufariki kwa kitu kidogo hata gram moja hakifiki lakini kinaogopwa dunia nzima
 
Mkuu Acha kutowa povu hujalazimishwa kuwa mu islam amekwambia wenzio kutokana na mambo yanayo endeleya Gaza wamepata fursa ya kujifunza uislam ni Nini ,lakini sio lazima Uwe mwislam
Mimi siyo muislam na sina mpango wa kusilimu, lakini nakuhakikishia matendo ya Isarael yanapelekea wengi sana kufanya hivyo.

Hata USA wanaongeza waumini.
 
Mkuu Acha kutowa povu hujalazimishwa kuwa mu islam amekwambia wenzio kutokana na mambo yanayo endeleya Gaza wamepata fursa ya kujifunza uislam ni Nini ,lakini sio lazima Uwe mwislam
Nani amekwambia mimi ni Mu-islamu au Imani yangu inakuhusu wewe nini ? Nadhani jifunze kusoma tena na kuelewa point yangu kubwa ni to each his / her own uamuzi wa mtu yoyote ni haki yake hata wote wakiamua kuwa mashetani all the best to them (unless umani zao zitaleta shida kwenye uhuru wa wengine sioni tatizo)
 
ulisema Idf inapata kipigo huko Gaza , imekuwaje tena useme wao ndo wanaonea hamas?
Sio kama wanawaonea Hamas ila wanaonea watoto, wanawake na wagonjwa na wanafunzi

Kama wangekuwa wanawapiga Hamas ingekuwa sawa lakini Hamas wapo na wiki iliyopita waliongea nao na kubadilishana mateka

Nahisi Kuna kitu kipo nyuma ya pazia katika hi vita
 
Jambo kubwa unalopaswa kulifahamu ni kuwa, kwa kadri ambavyo Hamas na makundi mengine ya Palestina yanavyoleta chokochoko dhidi ya Israel ndivyo ambavyo Israel inaongeza udhibiti wa hayo maeneo ili kuzima hizo chokochoko.
Kwa mfano, mwisho wa hii vita ya Gaza ya sasa huenda itapelekea 90% ya maeneo ya Gaza kuwa chini ya umiliki wa Israel milele!

Nani wa kulaumiwa?
Ujinga wa vikundi vya kigaidi ndani ya Palestina ndio vinazaa haya.

HASIRA ZA MKIZI FURAHA YA MVUVI.
 
Ile dini hawajitambui
Kwahiyo Ile vita ya dini ya Kiislam na Kiyahudi?

Au sijaelewa?

Kama ni vita ya kidini inaamana nchi zote za kiislam zikielekeza siraha zake Israel Kuna kiumbe kitakacho bakia pale?
 
Bado Israeli anapiga kirafiki sana, anatoa mpaka taarifa na vipeperushi. Kule Ukraine tuliona Mrusi anaangamiza miji na wala sikukuona ukianzisha mada za namna hii ila ulikuwa mshabiki mkubwa wa Urusi. Sasa kwa kutulia uone vile shoo inapigwa, Netanyahu aliposema hili litakuwa ni eneo la ukiwa hakuwa anatania.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Mabomu yanakoelekea ndipo Hamas walipo.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Hii vita ikiisha, ndani ya miaka 20 amani itatamalaki ukanda wa Gaza.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna kitu kilichopo nyuma ya pazia, kila kitu kiko wazi.
Kambi na makundi ya Hamas yapo katikati ya makazi ya watu huku wakijificha katika makundi ya watoto na wanawake. Hakuna namna risasi ya askari wa kiisrael au kombola la Israel litamfikia hata askari mmoja wa Hamas bila kukutana na wingu la wanawake au watoto wasiopungua 20.

Hamas sio wajinga kukaa kihasara hasara. Jamii inayopiganiwa na Hamas imekubali 100% kulipa hiyo gharama ya kuwaficha wana mgambo wa Hamas. Kinachowapata watu wasiokuwa na hatia huko Gaza kwa sehemu kubwa ni matunda wanayovuna kwa kuwahifadhi Hamas.
 
Ideology bila watu nayo imekufa pia. Jiulize wale magaidi wa kibiti wako wako, yaani watu wanakula na kushiba badala ya kufanya wanaanza kufuga ndevu na kuua polisi na kuteka silaha ati wanataka kuanzisha dola la Kiislam. Hawa risasi ziliwajibu, na mahandaki waliochimbia mpaka msikitini yalifumuliwa yote.
Mpaka leo kimya, gaidi siyo mtu wa kubembeleza.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Unajua kitu kinaitwa Antisemitism na unajua kilivyowagharimu wa-Israel karne hadi karne yaani kuanzia wale kina Shylock mpaka kina Rothschild kupelekea kuchukiwa ulimwenguni (Ni Hitler na prosecution yake iliyopelekea ulimwengu kugeuka na kuona kwamba hawa wadau wanaonewa) sasa the shoe is on the other foot wakionekana wenyewe ndio waonevu mwisho wa siku wenyewe ndio wa kupoteza, huwezi uka-gain land kwa kutumia mabavu na kuwaminya watu unaweza kutumia busara na hekima na ukapata zaidi (wakoloni wameweza hilo mbona kirahisi tu na sisi tunawapa Ardhi yetu kwenye Silver Platter) Narudia tena Ideology haiondolewi kwa mtutu wa Bunduki...
 
Walikwenda kulipua Kibiti nzima na kutembeza mabomu ? Sababu walichokuwa wanakifanya au kukitaka kilikuwa hakina tija na hata wanaowazunguka waliona hakina maana hao hao ndio walikuwa wa kwanza kutoa inteligensia kwamba hawa watu sio wenzetu..., Sababu hata kwa Macho ya Kaburu Mandela alikuwa Gaidi (lakini sababu alichokuwa anatetea kiliwagusa wadau wengi ) Apartheid alipata nguvu ingawa methology zilizotumika some could have been construed as terrorism...
 
Hii vita ikiisha, ndani ya miaka 20 amani itatamalaki ukanda wa Gaza.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Hii Amani iliondoka vipi hapo Gaza.., Na waliokuwepo wakati inaondoka ndio hawa ambao karibia wote wanakufa au huenda wanaozaliwa leo ni wadau wapya wenye madai kama hayo hayo ya baba zao wanaokufa leo ?
 
Al habib Mohammed Alwaz leo una lia lia baadae hamas wakirusha kombora sdoret una kuja na sired ingine ya kusifia et long live hamas 😂😂
nyie vijana wa mudi mna chekesha sana kwa kweli
 
Waarabu wa, turkey, Egypt, Lebanon, Pakistan, Yemen, saudia,Qatar, mpaka wale waarab Koko wa zenj,wamebqki kusema maneno tu kama wanaimba taarab, ilibidi wapereke jeshi kwa Siri, watumie mbinu za Iran, na Republican guard yake, watengeneze kitu kama ilivyokuwa Islamic State,
Wavamie Israel, walianzishe mpaka myahudi akimbie, maneno tu hayasaidii kitu, mzungu kuua kwake kawaida tu,
Alimtesa mwafrika kwa miaka 400!, alianza na utumwa, akaja na, ukoroni, akambeba kwa minyororo ya shingo, akaenda kumtumikisha America! Wala hajawahi, kuomba radhi, mzungu(Anglo Saxon) ni Yule Yule wa mkutano wa Berlin kuigawa Afrika! Sasa hawa wapalestina wameteseka kwa miaka 70! Wanategemea mzungu awaonee huruma! Watakawisha, kama waarab hawataungana na kukiwasha Huko, mashariki ya, kati
 
Mimi nimekujibu wazi na kirahisi kabisa. Israel hakuamka na kwenda kutwaa ardhi ya wapalestina. Kila chokochoko ya kigaidi ya vikundi vya kipalestina iliifanya Israel kudhibiti maeneo zaidi ya Palestina.

Mimi nakuuliza, kwa tukio la Hamas la 7 october, utashangaa Israeli ikiikalia kimabavu Gaza kwa 90% ?
 
Nope nina uhakika hii issue ikiisha Palestina itapata ardhi kubwa zaidi ya iliyonayo sasa.... sio kama iliyokuwa nayo miaka 10, ishirini iliyopita ila kubwa kuliko ya 7th Oktoba... And Israelite's have just added some more enemies among this Gen Z (ambao walikuwa hawapo miaka ya mapigano ya huko nyuma), Pili hio Apartheid inayoendelea huko nadhani itabidi ipungue pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…