Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kucheleweshwa kwa zoezi la vikosi vya Israel kuingia Gaza kuna watu wanaamini kuwa ni woga wa Israel kupata kipigo kutoka kwa vikosi vya wanamgambo wa Hamas na wenzao huko Gaza kama ilivyokuwa huko nyuma. Hapana safari hii ni zaidi ya uwoga.
Nia safari hii ni kuwamaliza wapalestina kwa wingi kuliko safari nyingine yoyote ile kwani wakiuliwa Hamas wachache wanazaliwa wengine wanaoendeleza vita. Mbinu hiyo sasa imeweza kufanyika mbele ya walimwengu wote. Marekani na Israel wanajua wanachofanya ndio maana badala ya kutoa amri ya kusitisha vita kila siku kuna ahadi za kwenda kesho yake badala ya leo.
Jumuiya ya waarabu wanaona kinachofanyika lakini nguvu yao kubwa ni kukataa tu kukutana na Rais wa Marekani aliyepanga kukutana nao badala ya kutoa tamko kali la kufunguliwa mpaka na kupeleka mahitaji na kuiamrisha Israel ifungue maji kwa wote bila masharti.Na hiyo nayo imekuja baada kuuliwa kwa wagonjwa na madaktari kwenye shambulio la anga kwenye hospitali hapo jana ambapo watu 500 wameuliwa kwa sekunde chache tu.
Urusi ilipojitoa kwenye mkataba ya usafirishaji nafaka kati yake na Ukraine umoja wa mataifa ulitoa malalamikio na shutuma kali kwa Urusi na kutamka kuwa ni ajabu kuwa Urusi inatumia chakula kama silaha.Hiyo ilikuwa ni kwa vile mahjitaji ya ngano na bidhaa nyengine zinazoambatana nazo ni kwa ajili yao wao.
Kwa upande wa Palestina wanajua kuwa maji kwanza ni muhimu kuliko hata chakula na bado hakuna tamko la kuiambia Israel kuwa iache kutumia maji kama silaha.
Kinachoendelea ni kama kutokea kichaa mwenye nguvu akamkaba koo mnyonge fulani katikati ya barabara penye watu wengi kama pale mtaa wa sikukuu Kariakoo na kila mmoja akapita zake bila kuwaamua hata kabla ya kuuliza ugomvi wao.Akifa mnyonge yule bali hukumu na ghadhabu za Mwenyezi Mungu zitawaenea wote walioshuhudia na wakapuuza.
Hatua wanazochukua waarabu na waislamu kwa ujumla ni hafifu sana kulingana na uzito wa ukatili wanaofanyiwa wapalestina.Wakiona wanakula na kunywa na kupata usingizi mnono wanawasahau wenzao.inashangaza kumekuwa na uungwaji mkono wa wapalestina nchi za Ulaya ,Marekani na kwengineko kuliko nchi za kiarabu ambazo ni jirani zaidi na Palestina kunakotokea unyama huo.
Watu wa Ulaya na kwengineko wanajua hakuna maisha ya furaha kwa watu 90 kuishi kwenye nyumba moja isiyo na huduma kamili za kibinadamu na kila muda wakiangalia angani kusikiliza kombora ambalo linaweza likwawaangamiza wote kwa pamoja.
Waarabu wajitayarishe na mabalaa yatakayowakuta wao wenyewe kwa uzembe wao.Hii dunia ni kitu kidogo sana kwa Mwenyezi Mungu.