Wapangaji waijulishe TRA kuwa nyumba si zao ili TRA isifanye kosa kuwatoza kodi ya jengo

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
21,741
Reaction score
26,735
Ili kuondoa mgogoro kati ya mwenye nyumba na mpangaji TRA iwatake wapangaji wapeleke namba zao za mita na kuiwezesha TRA iwaondoe kwenye kulipishwa kimakosa. Hata hivyo tatizo litabaki pale mwenye nyumba na mapangaji wanatumia mita moja ambapo mwenye nyumba atalazimisha wapangaji walipe kodi ya jengo.
 
Yani kuhangaika kote Huku ni kwasababu ya 1000 tu kwa mwezi?
Tunalalamika mno vitu vya kipuuzi ndio maana tukiwa na malalamiko ya msingi serikali haiyatilii maanani maana imetuzoea ni wapayukaji hovyo.
Huyo mpangaji atakayegombana na mwenye nyumba kwasababu ya 1000 atakuwa juha
 
Mpangaji kumiliki mita ya LUKU😂😂only in Tanzania....tuwe serious!ngoja wenye nyumba wapandishe kodi ya kufidia hayo makato ya 1000/= kwa mwezi. Hiyo system ya makato iwekwe pia kwenye ukusanyaji wa takataka na ulinzi wa sungusungu...wabongo bhana!kodi ya barabara (road licence)ambayo ilitakiwa ilipwe na mmiliki wa chombo imewekwa kwenye mafuta na unalipa hata kama chombo si chako ..Watu kimyaaa!!
 
Urahisi ni kwa mpangaji na mwenye nyumba wakubaliane namna ya kuifidia hiyo kodi ya nyumba toka katika malipo ya pango anayolipa mpangaji. Unakata tsh 10,000 yako toka katika kiwango cha pango cha baba mwenye nyumba maisha yanaendelea
 
Mpangaji kumiliki mita ya LUKU😂😂only in Tanzania....tuwe serious!ngoja wenye nyumba wapandishe kodi ya kufidia hayo makato ya 1000/= kwa mwezi. Hiyo system ya makato iwekwe pia kwenye ukusanyaji wa takataka na ulinzi wa sungusungu...wabongo bhana!kodi ya barabara (road licence)ambayo ilitakiwa ilipwe na mmiliki wa chombo imewekwa kwenye mafuta na unalipa hata kama chombo si chako ..Watu kimyaaa!!
Sh.50 ni way low kulinganisha na 1000-10,000. Its likely you dont feel the pinch wangeweka hio 50 kwenye kila sehemu it would make a lot of sense kuliko kuweka %
 
Yani kuhangaika kote Huku ni kwasababu ya 1000 tu kwa mwezi?
Tunalalamika mno vitu vya kipuuzi ndio maana tukiwa na malalamiko ya msingi serikali haiyatilii maanani maana imetuzoea ni wapayukaji hovyo.
Huyo mpangaji atakayegombana na mwenye nyumba kwasababu ya 1000 atakuwa juha
Wewe ni tajiri na haujui kuna watu mchana huu hawatakua na sh. 1,000/= ya kununua unga wa dona wale na watoto wao. Kumbuka unapotoa sh.1,000/= kununua umeme utakatwa hivyo utapata uniti pungufu zaidi na kusababisha mzunguko wa kununua umeme uwe karibu karibu. Ni vizuri kama wewe ni tajiri pita pembeni waachie masikini walilie ugali bila mboga.
 
Kwa kweli..
Watanzania wengi wana mentality kuwa serikali ikifanya hivi basi wapinge tuu..
 
Wewe ni tajiri na haujui kuna watu mchana huu hawatakua na sh. 1,000/= ya kununua unga wa dona wale na watoto wao. Kumbuka unapotoa sh.1,000/= kununua umeme utakatwa hivyo utapata uniti pungufu zaidi na kusababisha mzunguko wa kununua umeme uwe karibu karibu. Ni vizuri kama wewe ni tajiri pita pembeni waachie masikini walilie ugali bila mboga.
Elfu moja ukiigawa kwa siku 31 unapata ngapi ili upate kwa siku wanachukua kiasi gani?
Acheni lawama za kijinga.
 
Tumia kichwa kufikiri, kwanini nilipie sh.1,000/= wakati nyumba si ya kwangu? Wewe unaona hiyo hela ni ndogo wakati wenzako hawana sh 400/= ya kupandia daladala hivyo wanatembea kwa mguu toka Ubungo (kama unaifahamu) mpaka Magogoni (kama unakufahamu) Dar. Ukiona watu wamejipanga kwenye misikiti ya wahindi siku za Ijumaa usiwacheke, ni umasikini walioupata ndani ya Uhuru.
 
Tukiambiwa tunaishi in a shit hole country tunaona kama tunaonewa,TRA kujihusisha na kukusanya mapato ya kodi hii ambayo ni wajibu wa serikali za mitaa
 
Yani kuhangaika kote Huku ni kwasababu ya 1000 tu kwa mwezi?
Tunalalamika mno vitu vya kipuuzi ndio maana tukiwa na malalamiko ya msingi serikali haiyatilii maanani maana imetuzoea ni wapayukaji hovyo.
Huyo mpangaji atakayegombana na mwenye nyumba kwasababu ya 1000 atakuwa juha
Kwanza tu ni kuweke sawa ni kuwa wewe ni mnafiki wa wazi kabisa.

Katika swala dogo kama hili umeshindwa kujua nan adui na nani mwenzako usimame nae katika kupambania haki ambayo wewe inakuhusu.

Nadhani unakumbuka ile hadithi ya mtego wa panya ulioua kuku, mbuzi, kondoo na ng'ombe na panya ambaye ndie muhusika wa mtego akapona. Lakini panya huyo huyo aliwaonya na kuwashirikisha hawa wanyama wakubwa wamsaidie na walikataa wakiamini huo mtego wa panya hauwahusu.

Anyways kama hauifahamu hiyo story hebu nenda kaitafute uisome uielewe. Utapata ujumbe.

Wewe raia wenzako wanalalamika kunyanyaswa wewe unatetea bila hata chembe ya huruma. Mbona hauna upendo na watanzania wenzako?!

Unakuwa kama Job ndugai akikaa kwenye kiti kile cha uspika anajibu majibu utadhani yeye anamiliki hii Dunia. Acha dharau.

Kama 1000 kwako ni ndogo kuna wenzako wanaitafuta kwa shida sana na hawapo tayari kunyang'anywa hiyo 1000 kiuonevu kwa kisingizio cha sijui kuchangia kodi ya nini sijui. Ni upumbavu.

Hebu jaribu kuwa muungwana wewe.
 
Wewe ni tajiri na haujui kuna watu mchana huu hawatakua na sh. 1,000/= ya kununua unga wa dona wale na watoto wao. Kumbuka unapotoa sh.1,000/= kununua umeme utakatwa hivyo utapata uniti pungufu zaidi na kusababisha mzunguko wa kununua umeme uwe karibu karibu. Ni vizuri kama wewe ni tajiri pita pembeni waachie masikini walilie ugali bila mboga.
Umemwambia sawa kabisa
 
Yani kuhangaika kote Huku ni kwasababu ya 1000 tu kwa mwezi?
Tunalalamika mno vitu vya kipuuzi ndio maana tukiwa na malalamiko ya msingi serikali haiyatilii maanani maana imetuzoea ni wapayukaji hovyo.
Huyo mpangaji atakayegombana na mwenye nyumba kwasababu ya 1000 atakuwa juha

Kama ni hivi tutaiuliza serikali zile kauli za nchi hii ni tajiri na kusikia namba za tozo za madini zilivyokuwa zikiongezeka imeishia wapi? Mbona sasa ni kauli za tozo aka kodi za kichwa kila mahali?
 
Tumia kichwa kufikiri, kwanini nilipie sh.1,000/= wakati nyumba si ya kwangu? Wewe unaona hiyo hela ni ndogo wakati wenzako hawana sh 400/= ya kupandia daladala hivyo wanatembea kwa mguu toka Ubungo (kama unaifahamu) mpaka Magogoni (kama unakufahamu) Dar. Ukiona watu wamejipanga kwenye misikiti ya wahindi siku za Ijumaa usiwacheke, ni umasikini walioupata ndani ya Uhuru.
Lipa mkuu, hata hii mitandao unayotumia kulalamika na umeme unaochajia simu ni zao la kodi na tozo mbalimbali. Kata fedha yako kwenye Kodi ya mwenye nyumba.
 
Back
Top Bottom