Hapana mkuu, hii sio kodi ngeni na si dhambi kukusanywa. Shida inakuja ni namna gani inakusanywa.
Kama swala ni kusolve Foleni za walipaji, mbona umeme na maji tunalipia kwa njia ya simu, bank na hata application za simu.
Kwahiyo sidhani kama dhamira yao ni kusolve hilo tatizo la foleni bali kuna motive nyingine nyuma ya hili.
Ila swala la msingi hapa kwanza linaloanza kuleta utata ni uhalali wa matumizi ya haya makusanyo ambayo yanakusanya kwa expense ya furaha na amani ya raia wasio na maisha yenye uelekeo.
Tusijivike aibu ya uzalendo kushindwa kuhoji nini kinaendelea. Raia hatutaki kutoa kodi sababu huwa haziendi pahala husika na kuishia kutuumiza tu kwenye kulipia.
Sasa nadhani badala ya kuwajibika kulipa ni vema tuwajibike pamoja kama wananchi kuhoji hela zinakwenda kutumikaje na wapi zinaenda.....
Au unasemaje mkuu?!