Wapare mara nyingi wakienda kwao husema wanaenda Upareni

Wapare mara nyingi wakienda kwao husema wanaenda Upareni

Hao wachaga wana mini cha ajabu cha kutufanya tujipendekeze kwao?Actual kama kusoma hata sisi tumesoma Wilaya ya Mwanga IPO kwenye Wilaya kumi bora zilizotoa ma Profesa nchi hii!
Hiyo Moshi yenyewe imeshaathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi hakuna lolote Sikh hizi.Wenyewe wanakimbilia mikoa mingine MF Mwanza,Shinyanga n.k Msituletee hizoo bwana!
Ndo muache sasa kusema mnaenda moshi. Hapawahusu.
 
kabila letu ni Vaathu/ Vaasu, au Vamp'hare; lugha ni Chasu / Chathu. pia kabla ya kuwa jamii iliyounganika kama kabila, Wapare walikuwa jamii ndogondogo zenye asili ya makabila mengi kama Wakamba, Wataita, Wazigua, Wagweno, Wachaga, n.k.

Hakuna jamii / koo ya Wapare ambao waliwahi kupigana vita na Wachaga. In fact kuna koo za Wapare ambao kazi yao ilikuwa kutengeneza silaha zinazotumika katika vita baina ya jamii za Wachaga. Wapare kuishi milimani sababu yake ni kukimbia magonjwa toka maeneo ya tambarare, na kujilinda kutokana na mashambulizi toka kwa jamii nyingine haswa Wamaasai / Wakwavi, na Wazigua.
Nikumbushe vita ya kavambughu na nkhoma ya mkwavi.
 
Yule sio mpare ni mkaguru na jina lake halisi anaitwa Emmanuel ila bosi wake aliemtoa kwao kibaigwa ndie mpare anaitwa kadege ,,,,ila wengi wamezoea kumuita mshana kwasababu ndivyo alivyoandika dukani kwake huyo mzee kadege sasa mzee kadege alipomchukua Emanuel dhumuni amsaidie kazi za shamba baadae akaja kugundua kuwa Emmanuel huwa wakati wa baridi huwa anashikwa sana na pumu sasa kutokana na mzee kadege kumpenda sana Emanuel akaamua amuweke dukani hapo ndipo jina la mshana likaanza kutrend kwasababu wengi walijua mzee kadege ni baba yake......kwasasa Emmanuel ni dalali hapo tandika double cabin na hapo anatambulika kama kalulu japo sijajua hili jina kalipataje ila jamaa ninachomsifu ni muaminifu mno
Duuh! Mshana Jr hii ni kweli

Sent from my SO-01K using JamiiForums mobile app
 
Hao wachaga wana mini cha ajabu cha kutufanya tujipendekeze kwao?Actual kama kusoma hata sisi tumesoma Wilaya ya Mwanga IPO kwenye Wilaya kumi bora zilizotoa ma Profesa nchi hii!
Hiyo Moshi yenyewe imeshaathiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi hakuna lolote Sikh hizi.Wenyewe wanakimbilia mikoa mingine MF Mwanza,Shinyanga n.k Msituletee hizoo bwana!



Ndiyo kila mtu ahivunie kwao na sio kwa wenzie!

Kila mtu ashinde matches zake!

Semeni mnaenda Mwanga au Thame [emoji4]
 
Jamaa inasemekana kuwa very complicated and complex!

Wanaweza kuuza ng’ombe kwa kesi ya kuku [emoji38]

Pata picha ni watu wa namna gani?!
 
Jamaa inasemekana kuwa very complicated and complex!

Wanaweza kuuza ng’ombe kwa kesi ya kuku [emoji38]

Pata picha ni watu wa namna gani?!
mwisho wake atakushinda kesi na utamlipa kuku pamoja na ng'ombe. maana ya huo utani ni kwamba mpare hakubali haki yake ichezewe hata siku moja.
 
Maneno ya wenye husuda kali hayo [emoji3] thibitisha wizi wao ni upi? [emoji2369]
wapare wanawapenda sana jirani na watani zao wachaga. mimi wazee wangu walinihusia kwamba mahali ambapo hakuna mpare,mchaga, au msomali, hakuna pesa kwa hiyo niepuke kuishi hapo.🤣
 
Nasikia zamani wapare waliulizwa na Mwalimu JK kwamba ninyi wananchi hadi sasa hivi kuna kitu gani mmefanya cha maendeleo ili serikali iunge mkono juhudi zenu? Wakajibu eti "TUMEJENGA MAHAKAMA" (kwa lafudhi ya kipare)..

Nyerere aliwakuta Wapare wanachimba barabara kwa njia ya kujitolea inaitwa "msaragambo." Moyo huo wa kujitolea na uchapakazi wa Wapare ulimfanya Nyerere atamke kwamba, " Wapare ni Wachina wa Tanzania. " Mpare ni mchapakazi na haogopi ushindani, ndio maana anaishi popote pale Moshi, Iringa, Tanga, Arusha, hata nje ya Tanzania.
 
SIKU HIZI WACHAGA WANANUNUA SANA UCHAWI....WALE WA JIRANI NA KENYA WANANUNUA KWA WAKAMBA! KUNA KISA KIMOJA HUKO URU KUNA NYUMBA KUBWA TU WALIKUA WANAIGOMBANIA WANA FAMILIA IKAPIGWA JUJU MZEE! DUUU WAKATI WOTE ASUBUHI,MCHANA,JIONI INAUNGUA MOTO NA KUFUKA MOSHI MBONA WALIIKIMBIA!! (NATURE WACHAGA MWANZONI HAWAKUWA NA UCHAWI WA ASILI ILA WANANUNUA SANA PIA KULE ROMBO KUMILIKI MALI KISHIRIKINA.ACHANA NAO KABISA HAWA WATU.....HALAFU KUPENDA MASIFA KANA KWAMBA WAO HAPA TANZANIA NI BORA KULIKO JAMII NYINGINE ! WAKATI WANAJISIFU JAMII NYINGINE WANAPIGA KAZI WANASONGA MBELE.(HAKUNA MWAFRIKA BORA KULIKO MWINGINE WENGI TUNATOFAUTIANA KIDOGO TU) HASA HAWA WA KUSINI YA JANGWA LA SAHARA BURE KABISA! TUUNGANE TUJENGE TANZANIA YETU MADA ZA UKABILA HUMU TUWEKE PEMBENI!!!
Wee mpare mbona umekuwa mkali? Uchawi wa asili kwa kaskazini upo upareni na usambaani, hii ndiyo mada yetu, hayo ya kujisifu sisi hatuna, chaggas are really hustlers that's y they are everywhere in this country. Nenda masasi, kasulu, tarime lazima utamkuta shirima anapambana huko. Hii mifano yako ya wachaga wawili watatu waliouziwa uchawi na wapare/wasambaa haina tija. Ni sawa na kumkuta mmasai mmoja au wawili wanakula samaki ukasema wamasai wote ni wala samaki
 
Ilisemekana wakati fulani kuwa wapare na eneo lao watafanyiwa recategorization wawe mkoa wa Tanga au mkoa mpwa wa Koorogwe [emoji28][emoji3]

Sijui ilifikia wapi huo mpango!
 
mwisho wake atakushinda kesi na utamlipa kuku pamoja na ng'ombe. maana ya huo utani ni kwamba mpare hakubali haki yake ichezewe hata siku moja.



Sasa usumbufu wa gharama na muda wa case si bora ungefanya mambo mengine.

Halafu kushinda case huwa Inategemea [emoji3]

Ndio maana sio wote walioko gelezani ni wakosa.

Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi wapate haki zao wawe huru.
 
Sasa usumbufu wa gharama na muda wa case si bora ungefanya mambo mengine.

Halafu kushinda case huwa Inategemea [emoji3]

Ndio maana sio wote walioko gelezani ni wakosa.

Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi wapate haki zao wawe huru.

Ni maneno ya utani tu kuhusu wapare. uhalisia ni kwamba wapare ni watu wasiokata tamaa ktk kupigania haki zao.
 
Ni maneno ya utani tu kuhusu wapare. uhalisia ni kwamba wapare ni watu wasiokata tamaa ktk kupigania haki zao.


Sawa [emoji3] kwa sehemu nimekuelewa,

Lakini kwa tafsiri nyingine ni tabia ya ukorofi.

Ya kutaka kuendeleza ligi ya mivutano badala ya kutafuta namna ya kumaliza jambo peaceful.

Mnapenda cases.

Hebu pata picha Eti mtu akauze ng’ombe ili ashinde case ya kuku ? [emoji15]

Nyie ni noma aisee! [emoji4]
 
Huwa wanaenda kutambika kwa Mungu wao yuko huko mlimani.

Pia wanaenda kuongezea uchawi, wapare wote 🤣 ni wachawi eti wawe kama Msuya japo zamani walitaka wawe kama mengi.

Mpare anayebisha aje na mbuzi nimpe ushahidi.
Katika hili unawasingizia bure wapare. Mambo ya kichawi, kishirikina, kutambika au kitamaduni kwa wapare yamebakia mambo binafsi sana ya mtu mmoja mmoja kisiri huku yakipingwa mnoo na jamii za wapare.

Hao jamaa kwa sehemu kubwa sana waliwahi kufikiwa na dini (Ukristo na Uislamu) mapema sana na elimu (shule) kusambaa kote, wengi wamestaarabika mnoo. Hata pombe za kienyeji ni nadra mnoo kukutwa zinanywewa huko upareni, ni mila walishazikaa kitambo.

Kwa zama hizi, kwa mkoa wa Kilimanjaro, huenda wachaga ndio wanajihusisha zaidi na mila za kishirikina (kutambika) kuliko wapare. Mpaka leo hii ni kawaida kwa koo za kichaga kukaa chini (bila woga au usiri) kufanya matambiko wakati kwa wapare koo itakayojulikana kufanya hicho kitu itatengwa (itaepukwa, watu hawatakuja kuoa au kuolewa hapo nk)
 
Back
Top Bottom