Wapare mara nyingi wakienda kwao husema wanaenda Upareni

Wapare mara nyingi wakienda kwao husema wanaenda Upareni

Sawa [emoji3] kwa sehemu nimekuelewa,

Lakini kwa tafsiri nyingine ni tabia ya ukorofi.

Ya kutaka kuendeleza ligi ya mivutano badala ya kutafuta namna ya kumaliza jambo peaceful.

Mnapenda cases.

Hebu pata picha Eti mtu akauze ng’ombe ili ashinde case ya kuku ? [emoji15]

Nyie ni noma aisee! [emoji4]

unajua mambo mengi ya wapare huamuliwa kwa mashauriano. na mashauriano hayo mara nyingi huwa marefu sana mpaka watu wafikie muafaka. na mara nyingi muafaka ukishafikiwa wote walioshiriki ktk shauri hilo hufungwa na maamuzi hayo.

mimi nimeshuhudia hata suala la ndoa za kipare; majadiliano ya posa, wazee wakisimamia taratibu hatua kwa hatua. kwa mfano mahari ya kipare inahusisha matoleo ya mbuzi na ng'ombe. na kuna taratibu za kipi kitangulie. sasa wazee huwa wakali kwelikweli ikiwa mtoa mahari atakiuka hatua ktk suala hilo. ukiacha suala la mali zilizoko ktk mahari kuna suala la mahali ambapo mahari inatakiwa itolewe au ipokelewe. kwa mfano, mpokea mahari anatakiwa aende kwenye boma la mtoa mahari achague yeye ng'ombe anaowataka.

kwa mtu ambaye anashuhudia kwa mara ya kwanza anaweza kudhani anashuhudia mahakama ikifanya kazi. maana zoezi zima huhusisha vijana wenye kumbukumbu nzuri ambao huelezea suala zima toka lilipoanza mpaka lilipofikia. halafu wako wazee ambao ni wajuvi wa mila na taratibu na hao hutoa muongozo, au huingilia kati kunapotokea ukiukwaji wa mila za ndoa.

binafsi naamini makuzi hayo ndio husababisha wapare kuwa na "dna ya kupenda kesi."🤣
 
barabara hii mnayoiona kutoka Same kwenda milimani Chome ilichimbwa na wananchi wa wilaya ya Same kwa utaratibu wa kujitolea. utaratibu huo wa kazi za maendeleo za kujitolea unaitwa "msaragambo."

serikali ya mwalimu nyerere ilikuja kuwapa sapoti wananchi kwa kutoa baruti za kupasua muamba mkubwa ili barabara iweze kupitika. Mwalimu Nyerere alipotembelea Same na kuona wananchi wakijituma ndipo alitamka kwamba , " wapare ni wachina wa tanzania. "

 
Nasikia Nyerere alienda upare akakuta watu wote wafupi Kama watoto wadogo kumbe ni watu wazima akawauliza nyinyi wazazi wenu wako wapi wakajibu sisi ndio baba zao na sisi ndio mama zao yakimaanisha wao ndio baba na mama yaani watu wazima daaa wapere wafupi sana
Stori za vijiweni hizoo... Kwanza alipigwa na butwaa kukuta kuna vafumwa walioendelea kushinda yeye...
 
Kwetu Upareni kaka kitovu changu kiko huko mahali panaitwa Store Mombasa
Mwaka huu naenda upareni kwetu, Usangi.

Nimemisi sehemu za upareni kwetu kama , chekereni, store Mombasa, Mchali, Kikweni.
 
Asipo kuelewa basi ana tatizo la afya ya akili
Katika hili unawasingizia bure wapare. Mambo ya kichawi, kishirikina, kutambika au kitamaduni kwa wapare yamebakia mambo binafsi sana ya mtu mmoja mmoja kisiri huku yakipingwa mnoo na jamii za wapare.

Hao jamaa kwa sehemu kubwa sana waliwahi kufikiwa na dini (Ukristo na Uislamu) mapema sana na elimu (shule) kusambaa kote, wengi wamestaarabika mnoo. Hata pombe za kienyeji ni nadra mnoo kukutwa zinanywewa huko upareni, ni mila walishazikaa kitambo.

Kwa zama hizi, kwa mkoa wa Kilimanjaro, huenda wachaga ndio wanajihusisha zaidi na mila za kishirikina (kutambika) kuliko wapare. Mpaka leo hii ni kawaida kwa koo za kichaga kukaa chini (bila woga au usiri) kufanya matambiko wakati kwa wapare koo itakayojulikana kufanya hicho kitu itatengwa (itaepukwa, watu hawatakuja kuoa au kuolewa hapo nk)
 
We muongo. Hakuna mpare anasema kwa ni Moshi. Wilaya za Wapare ni Same na Mwanga
Huwa hawataki kutaja hasa maeneo waliyotoka, yaani Chome, Mwanga, Ugweno na Usangi.

Ukiwauliza wanasema kwao Moshi [emoji23]
 
Yule sio mpare ni mkaguru na jina lake halisi anaitwa Emmanuel ila bosi wake aliemtoa kwao kibaigwa ndie mpare anaitwa kadege ,,,,ila wengi wamezoea kumuita mshana kwasababu ndivyo alivyoandika dukani kwake huyo mzee kadege sasa mzee kadege alipomchukua Emanuel dhumuni amsaidie kazi za shamba baadae akaja kugundua kuwa Emmanuel huwa wakati wa baridi huwa anashikwa sana na pumu sasa kutokana na mzee kadege kumpenda sana Emanuel akaamua amuweke dukani hapo ndipo jina la mshana likaanza kutrend kwasababu wengi walijua mzee kadege ni baba yake......kwasasa Emmanuel ni dalali hapo tandika double cabin na hapo anatambulika kama kalulu japo sijajua hili jina kalipataje ila jamaa ninachomsifu ni muaminifu mno
Mshana Jr
 
Katika hili unawasingizia bure wapare. Mambo ya kichawi, kishirikina, kutambika au kitamaduni kwa wapare yamebakia mambo binafsi sana ya mtu mmoja mmoja kisiri huku yakipingwa mnoo na jamii za wapare.

Hao jamaa kwa sehemu kubwa sana waliwahi kufikiwa na dini (Ukristo na Uislamu) mapema sana na elimu (shule) kusambaa kote, wengi wamestaarabika mnoo. Hata pombe za kienyeji ni nadra mnoo kukutwa zinanywewa huko upareni, ni mila walishazikaa kitambo.

Kwa zama hizi, kwa mkoa wa Kilimanjaro, huenda wachaga ndio wanajihusisha zaidi na mila za kishirikina (kutambika) kuliko wapare. Mpaka leo hii ni kawaida kwa koo za kichaga kukaa chini (bila woga au usiri) kufanya matambiko wakati kwa wapare koo itakayojulikana kufanya hicho kitu itatengwa (itaepukwa, watu hawatakuja kuoa au kuolewa hapo nk)
Umefika Ugweno kweli wewe? Maeneo ya Mriti, Vuchama Ngofi, Fumbua ng'ombe n.k

Je Kaseni na Sungo?

Mkuu acha kabisa, wenyeji wa huko wenyewe huwa hawarudi makwao na kuishi mpaka leo, wakienda ni kuzika tu na kurudi siku hiyohiyo
 
Watu wa makabila mbali mbali walioko mijini ama mbali na nyumbani (sehemu ya asili yao) mara nyingi wakitaka kusema wanarudi kwao watataja jina husika la mji ama sehem anayotoka.

Mfano kwachaga atasema naenda moshi. Muhaya atasema naenda bukoba, mngoni atasema ashuka zake songea nk.

Ila inanishangaza kwa Wapare. Mara nyingi sana utaskia naenda Upareni. Au atamuuliza mtu "hivi lini unapandisha upareni" na wakati wana sehemu zao km Usangi, Ugweno, Chome, Same nk.

Ni mazoea ama kuna sababu maalum?

View attachment 2443480
Kwa sababu Moshi ni ya wachaga.
 
Back
Top Bottom