Sawa [emoji3] kwa sehemu nimekuelewa,
Lakini kwa tafsiri nyingine ni tabia ya ukorofi.
Ya kutaka kuendeleza ligi ya mivutano badala ya kutafuta namna ya kumaliza jambo peaceful.
Mnapenda cases.
Hebu pata picha Eti mtu akauze ng’ombe ili ashinde case ya kuku ? [emoji15]
Nyie ni noma aisee! [emoji4]
unajua mambo mengi ya wapare huamuliwa kwa mashauriano. na mashauriano hayo mara nyingi huwa marefu sana mpaka watu wafikie muafaka. na mara nyingi muafaka ukishafikiwa wote walioshiriki ktk shauri hilo hufungwa na maamuzi hayo.
mimi nimeshuhudia hata suala la ndoa za kipare; majadiliano ya posa, wazee wakisimamia taratibu hatua kwa hatua. kwa mfano mahari ya kipare inahusisha matoleo ya mbuzi na ng'ombe. na kuna taratibu za kipi kitangulie. sasa wazee huwa wakali kwelikweli ikiwa mtoa mahari atakiuka hatua ktk suala hilo. ukiacha suala la mali zilizoko ktk mahari kuna suala la mahali ambapo mahari inatakiwa itolewe au ipokelewe. kwa mfano, mpokea mahari anatakiwa aende kwenye boma la mtoa mahari achague yeye ng'ombe anaowataka.
kwa mtu ambaye anashuhudia kwa mara ya kwanza anaweza kudhani anashuhudia mahakama ikifanya kazi. maana zoezi zima huhusisha vijana wenye kumbukumbu nzuri ambao huelezea suala zima toka lilipoanza mpaka lilipofikia. halafu wako wazee ambao ni wajuvi wa mila na taratibu na hao hutoa muongozo, au huingilia kati kunapotokea ukiukwaji wa mila za ndoa.
binafsi naamini makuzi hayo ndio husababisha wapare kuwa na "dna ya kupenda kesi."🤣