Wapare mara nyingi wakienda kwao husema wanaenda Upareni

Wapare mara nyingi wakienda kwao husema wanaenda Upareni

mleta mada kasema wengi wanasema Upareni yaani Paris sasa wewe umeshamuona mpare anaenda Upareni alafu aseme anaenda Moshi
labda ukuta anaenda Moshi kweli pia Moshi kuna kipi cha ajabu hadi wajipendekeze wewe mama
Moshi Kuna wapare ambao ni nyumbani kabisa, mfano Moshi vijijini Kuna wapare, wakamba, wamasai, na wakahe although wachaga ndo dominant
 
Watu wa makabila mbali mbali walioko mijini ama mbali na nyumbani (sehemu ya asili yao) mara nyingi wakitaka kusema wanarudi kwao watataja jina husika la mji ama sehem anayotoka... Mfano kwa mchaga atasema naenda moshi... Muhaya atasema naenda bukoba, mngoni atasema ashuka zake songea nk.
Ila inanishangaza kwa wapare... Mara nyingi sana utaskia naenda upareni... Au atamuuliza mtu "hivi lini unapandisha upareni" na wakati wana sehem zao km usangi, ugweno, chome, same nk...

Ni mazoea ama kuna sababu maalum?

View attachment 2443480
Mimi naenda Usukumani Krismas ya mwaka huu 2022, Upareni nitaenda mwakani 2023
 
Tunaenda upareni, kama hutaki acha.
Hahaaa. Kati ya makabila yenye maendeleo na yenye watu wachapa kazi ni watani wetu Wapare. Nikiwa na mpare mahali najua nipo na jembe sina wasiwasi. Wapare endeleeni kuijenga Same mjini inakuwa kwa kasi na kupendeza ila tu serikali yetu inatuangusha kwa kushindwa kupangilia miji yetu. Siku si nyingi na nyie mtasema, 'naenda Same..."
 
Naam tuna mauzoefu wa mengi na hatupaparikii ile kitu sana.
Tunajua kufanya maamuzi sahihi nk nk
Mshana Jr
giphy.gif
 
Mkuu niko Arusha but ni mhamiaji tu.
So sina vimelea vya Arusha na sitokuwa navyo.
Napenda utani sana lkn mimi siwezi kuua hata sisimizi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Usitishwe na fujo zangu...maisha halisi mimi ni mtu na nusu[emoji1787][emoji1787][emoji1787]...
Nimejipigia debe kidogo
Inna

Hahaha, kujipigia promo muhimu, ukisubiri Inna akupigie promo utachelewa sana. Halafu huoni hata mimi nina utani mwingi tu, bila kufurahi maisha hayaendi

Aah sasa kama sio AR ni wapi mzee wa uhamiaji?
 
Back
Top Bottom