Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
WAPENDA HAKI HATUTAMCHAGUA DIAMOND PLATNUM
Na, Robert Heriel
Katika Tuzo za BET Diamond ni moja ya Wasanii wanaowania Tuzo hizo.
Wapenda haki, wanaharakati na Wana mtandao wote kuanzia Facebook, Instagram, JamiiForums, na Twitter Kama tulivyokubaliana hatutampa Kura Diamond Platnum na hatashinda tuzo hizo Kwa sababu ameshindwa kutumia nafasi yake vizuri kuilinda, kuijenga na kuitetea jamii yake.
Diamond hajawahi kutetea jamii ya Watanzania.
Utekaji na mauaji yalivyopamba Moto Diamond alikuwa wakwanza kutoa kibao chenye ujumbe usemao " Acha Nikae kimya" maudhui ya wimbo ule yalilenga kuhafifisha na kutia uoga jamii isipige kelele kuhusiana na vitendo hivyo vya udhalimu.
Diamond ni tofauti kabisa na Wasanii wa Nigeria Kama kina P Square, Burns boy, Davido n.k ambao mara kadhaa walijitokeza kuungana na jamii kuipinga serikali pale inapokosea mpaka kuandamana kabisa.
Diamond hawezi chaguliwa na watu wote walioenda shule, waliostaarabika, wapenda haki na wanaharakati.
Kwa hapa Nchini waliojaribu na wanaojitahidi kutetea haki na kutetea jamii ni kina Ney wamitego, Roma mkatoliki, Profesa Jay miongoni mwa wengine.
Diamond ni Aina ya wanamuziki wanaoiona jamii Kama jamii ya vibushuti sio ajabu ndio maana nyimbo zake nyingi hasa za siku hizi niza vibushuti, zinalenga watu wenye Low IQ.
Diamond Kama angenoga Kama angeimba nyimbo Kama za kipindi kile mathalani "nimpende Nani" ukimuona" Nitampata wapi" lakini sio hizi za Jeje na mfano wa zile za nyoka pangoni.
Kama tulivyokubaliana Kura asipate.
Ili iwe funzo Kwa Wasanii wa kizazi kinachokuja.
Msanii ambaye ni kioo cha jamii badala aungane na jamii yeye anaungana na serikali. Ajabu hii.
Hii ipo katika nchi yetu pekee.
Hata Marekani wenye muziki wao Wasanii wao huwa upande wa wananchi.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi