Wapenzi mkikaa pamoja kwa muda mrefu kuna kitu mtafanana, je wewe umefanana nini na mpenzi wako?

Wapenzi mkikaa pamoja kwa muda mrefu kuna kitu mtafanana, je wewe umefanana nini na mpenzi wako?

Wanawake ni kama watoto akikupenda anakuiga kila kitu. Kuna muda anataka hadi mavazi avae kama wewe utakuta umerudi amevaa flana yako, au pensi yako, mara boxer yako, mara apulizie pafymu yako au apake lotion yako ili mradi tu afanye unachofanya.

Ataanza tumia maneno kama yako, atataka kukaa pale unapopenda kukaa sebuleni, ataanza kuwa curious na simu yako anataka aone unatazama nini sana mtandaoni na ukimruhusu usishangae akaacha simu yake anataka gusa yako muda wote hata kama ni za kufanana.

Huyu wakwangu ananiiga hadi tabia ya kuamka usiku kula maana nina hiyo tabia. Kuna hali inakuja unapata kama njaa usiku wa sasa sita au saa nane so naamka nakunywa aidha maziwa, juice na bite yoyote ili kutuliza ile njaa. Hiu hali inanikuta sana kipindi cha baridi.

Sasa kameshakuwa na hii tabia hadi kameshakuwa kazoefu nyoko zake. Kakiamka namwambia alete tu tulie chumbani.

Raha sana kupendana halafu mkawa na tabia kufanana. Mnakuwa kama mtu fan wake.

Sasa ukute umekutana na mtu tabia ni kushoto na kulia. Humo ndani ni full kukunjiana sura na minuno isiyo na sababu na kufanyiana criticism zisizo na maana.
 
Kumbe huku wote mmeoa
Sasa ile timu kataa ndoa ipo wapi??

Za kuambiwa changanya na zako

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ukiwaiga walimwengu unaweza ingia choo cha kike. Wengine wanatolea to stress hapa ila huku uraiani wanapendana na wanaishi vizuri. We unafanya masihara kulala kama panga store.
 
Mi mweusi tiii ye Mweupe peee Nahis itatuchukua karne kufanana... Ila tabia kama kufiri kwa haraka na kuchukua maamuzi naona na yeye anaanza kuwa kama mim
Wewe na yeye ni kama mimi na yeye, hatuwezi fanana mionekano, ila tabia tumeanza kuendana, mfano mimi nimeanza kuwa mpole, ukali wote na machachari vinafifia kadri siku zinavyozidi kusonga.
 
Mapenzi raha nyie! Binafsi naona ni kitu kizuri sana kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu. 😍
Sasa na alivyo na career yake hutokaa uamini anavyodeka!

Kuna siku sijui aliniudhi nini nikakasirika sikumwambia kama nampenda, akanitumia VN analalamika mpaka kesho nikiisikiliza nacheka sana!
 
Kufanana sura kwangu Itakua ngumu.Alinifanya nikaaanza kusikiliza nyimbo za wasabato japo yeye sio msabato ila katoka kwenye familia yenye wasabato wengi.Kabla sikuwai kua mpenzi wa hizo nyimbo.Kwenye chakula jamani mi nilikua mpenzi Sana wa kande,mwenzangu hapendi sa hivi napika hiki chakula mara moja moja Sana,na nikipika ye nampikia chakula kingine.
 
Kuna Jamaa kama ww nakula mke wake dar asee nakiri wamefanana kuongea kabisa
 
Sie twafanana maamuzi, analo fikiria yeye na Mimi hilo hilo.
 
Back
Top Bottom