Wanawake ni kama watoto akikupenda anakuiga kila kitu. Kuna muda anataka hadi mavazi avae kama wewe utakuta umerudi amevaa flana yako, au pensi yako, mara boxer yako, mara apulizie pafymu yako au apake lotion yako ili mradi tu afanye unachofanya.
Ataanza tumia maneno kama yako, atataka kukaa pale unapopenda kukaa sebuleni, ataanza kuwa curious na simu yako anataka aone unatazama nini sana mtandaoni na ukimruhusu usishangae akaacha simu yake anataka gusa yako muda wote hata kama ni za kufanana.
Huyu wakwangu ananiiga hadi tabia ya kuamka usiku kula maana nina hiyo tabia. Kuna hali inakuja unapata kama njaa usiku wa sasa sita au saa nane so naamka nakunywa aidha maziwa, juice na bite yoyote ili kutuliza ile njaa. Hiu hali inanikuta sana kipindi cha baridi.
Sasa kameshakuwa na hii tabia hadi kameshakuwa kazoefu nyoko zake. Kakiamka namwambia alete tu tulie chumbani.
Raha sana kupendana halafu mkawa na tabia kufanana. Mnakuwa kama mtu fan wake.
Sasa ukute umekutana na mtu tabia ni kushoto na kulia. Humo ndani ni full kukunjiana sura na minuno isiyo na sababu na kufanyiana criticism zisizo na maana.