Wapenzi wa Mazda Atenza, average fuel consumption ya 21 km/L mnaionaje?

Wapenzi wa Mazda Atenza, average fuel consumption ya 21 km/L mnaionaje?

Ingekua usiku ningesave zaidi maana barabara nyeupe zaidi.
Next uje na masomo juu ya matumizi ya visaidizi mbalimbali kama cruise control, electronic parking brake e.t.c, maana wengi huwa wanavitumia ndivyo sivyo.
 
Nilikua na safari ya Dar hadi Moro town kisha Ifakara na kurudi Dar, kwa kutumia Atenza.

Mafuta (Diesel Tsh 80k) niliweka Puma ya Survey (jirani na Mlimani City) na kuanza safari pale kuelekea Morogoro.
View attachment 3110125

Njiani sikua na vituo zaidi ya kusimama JKT Mlandizi na Cate Hotel Morogoro.

Barabara ya Dar to Moro ina magari mengi ni mara chache sana kumaintain average speed ya 75km/h kwa muda mrefu, muda mwingi nimejikuta natembea average ya 50km/h au chini, nikitumia masaa matano na nusu hadi Moro (mi sio mtu wa kibati)!

Baada ya hapo misele ya Morogoro tu mjini, ambapo niliendesha zaidi na stops and go zilikua nyingi hadi kesho yake ndio safari ya Ifakara ikaanza.

img_0518-jpeg.3110130


Barabara ya Mikumi kutokea Ifakara ni nzuri sana, haina msongamano wala speed limits nyingi.
View attachment 3110215
Kukawa na misele ya siku mbili Hapo Ifakara ambapo nilitumia gari, na kuanza kurudi Dar.
View attachment 3110143

Kufika Mikumi town nikaongeza mafuta (taa ilikua imewaka) pale Total mafuta ya Tsh 50k, na kuendelea na safari hadi Moro ambapo nili break kwa nusu saa na kuendelea hadi Dar nonstop.

Kurudi kuanzia Mlandizi nilikutana na foreni sana kwahiyo speed ilikua ndogo sana.

Average speed ya safari nzima ilikua 21 km/h ambayo ni ndogo sana na imechangiwa na town trips na speed ndogo Morogoro road (Dar - Mlandizi).
View attachment 3110146

Kwa ulaji wa mafuta, trip nzima ina average ya 21.7 km/L.

View attachment 3110147

Kwa wastani kilometa 900 hiyo feedback.

Njiani nilikua natumia sana cruise control na ndio ilisaidia nisichoke sana na nilijitahidi kupunguza vituo vingi vya kusimama.

Okay, hii ndio experience yangu, kwa wadau wa Mazda CX5 ulaji wa mafuta utafanana kiasi chake kwasababu wanashare engine, Skyactiv 2.2D
Kwa gari ya diesel ni nzruri. Na imechangiwa na foleni na matumizi yako ya mjini(Moro na Ifakara).
 
Hapo unanunua kwa Mil 12 na TRA unakuta wanataka Mil 12
Hapa ndipo Hawa watoza ushuru wanapotipiga na kitu kizito. Kisha tunaziona wenzetu wanazitumbua Kwa ma vieti, kaka unaijua vieti wewewe? Kwa msema wa Mh. Balozi Polepole enzi hizo. Mungu awalani wao na vizazi vyao vitano Kwa kutunyonya.
 
Next uje na masomo juu ya matumizi ya visaidizi mbalimbali kama cruise control, electronic parking brake e.t.c, maana wengi huwa wanavitumia ndivyo sivyo.
Aisee Cruise Control sitaweza kuendesha gari bila hii kitu.
 
Kaka hizi janja janja hutatupa mpka sasa , me nmeona za 2014 zinaisha sana na bei zake zinafika mpk 6k$ mpk dar na juzi nliamgalia nkaona 2015 grey mpk dar ni 5k$

Ukija angalia zote pamoja na kodi mpk unaishika hazipishan sana

Na ushauri wako nn kwa first time buyer
Mzee hii chuma ushavuta au ulikuwa unamchosha tuu Mwamba kwa maswali?
 
CIF kuanzia $4300 hadi 5500 kutegemea na mwaka, condition etc.

TRA nao wanataka Milion 9 hadi Million 13 kutegemea na mwaka.
Na vipi kuhusu CX5 kiongozi...?
 
Back
Top Bottom