Kingsmen
JF-Expert Member
- May 4, 2020
- 279
- 213
Natarajia kuingia kufanya kazi huko nitakutafuta mkuu.Kwa uzoefu wangu niliofika kwa mda Cha kwanza hawa jamaa wapi makini sana kwa mgeni maswali ambayo watakuuliza cha kwanza unatakiwa uwe na show money isiopungua Dola 500 Cha pili unawenda wap au mwenyeji wako ni nani na huyo mwenyeji wako lazima wajue ana Kaa sehemu Gani na anajishuhulisha na nini na wakikugongea passport mda utaokuwepo kwao usije ukazidisha tarehe ya kukaa kwao ukizidisha Wana faini zao au jela na kingine hawa jamaa Wana ubinafsi sana kwa raia Mimi nilipoingia gaberon walipokagua passport yangu waliniuliza maswali mengi sana kabla hawajanigongea passport na kingine Cha muhimu sana epuka kumchukuwa mke wa mtu au x wa mtu wanawake ni wazuri sana na ukimwi ni mwingi sana na nchi nzuri sana ya kutafuta maisha hasa ukiwa unafanya biashara na biashara ambao itakayokuchomoa haraka ni biashara ya vinyago au kacha kama za huku kwetu na raia wengi hawapendi kufanya kazi ngumu maisha Yao asilimia kubwa ni ya bata