Wapi nitapata kazi ya malipo ya 5000 kwa siku?

Inapatikana wapi ?
 
Najaribu kufikiri hii inakuwaje, mimi nimefanya kazi za saidia fundi ujenzi miaka ya 97/98 kama kupandisha tofali, kuchanganya cement au kusuka nondo nilikuwa napata elfu tano au zaidi kwa siku.

Leo hii saidia fundi bado anapata hela ile ile au inakuwaje?
 
Uhitaji wa kazi kwa watu ni mkubwa...idadi ya vijana waliohitaji kazi miaka hiyo ya 97/98 sio sawa na sasa hivi.... Leo hata ukienda kuomba kazi hiyo ya kutumia nguvu bado watakulingia na usiipate!. Ila miaka hiyo inawezekana mlikuwa mnatafutwa.
 
watu wanaongea kirahisi rahisi sana,eti nenda kiwanda cha bia mara Coca-Cola,mara nenda ilemela kule kwenye viwanda vya samaki eti kazi za kumwaga!!!.Nyie watoto wa mama hamjui mziki wa ajira,hizo kazi zenyewe za viwandani zinahitaji connection na malipo ni kiduchu kazi mlima na kuzipata ni kwa kubahatisha sana
 
We dogo unamatatizo ya akili kweli ivi ukienda pale pepsi nyakato hupati kazi hara bila connection acha uzembe wewe kila siku kunajazi na lazima wachukue vibarua, siku nyingine nitakukata vibao kwenye uzi uvivu wako peleja huko
 
Nenda kwa wakala wa kusajiri lain muombe akure code upige kazi,utapata zaidi ya hiya hela,
 
Ile Siku Usiku Niliona Thamani Ya Boom Kwa Kipindi Kile Ilikuwa Sijui 5000/7000 Kwa Siku Nikasema Serikali Inatupa Kiasi Kikubwa Sana Kisa Kuingia Darasani Tu.
[emoji23][emoji23][emoji23] bahati mbaya ni wachache sana wakiwa chuoni wanaweka akiba ya pesa au kuwekeza ktk biashara. Wengi wao huishia kumiliki simu na pisi kali tu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…