Wapi nitapata soko la kuuza mkaa mbadala? Ujuzi wa kuzalisha ninao, mwenye kujua soko anijuze tafadhali

Njoo uone mkuu au nipigie 0711756341 nimezalisha kidogo natumia nyumbani! Kwasasa nina kilo elfu 1000 zipo tu sijui hata pa kuzipeleka!
Kiufupi ni kama ka kiwanda maana nimeunganisha na mota za umeme kuchanganyia!
Nitoke Morogoro au Igunga kufuata mkaa wa buku. Hakika nitakuwa qualified inmate wa Mirembe.

Sambaza mkaa wako kwenye maduka na supermarkets kwa kuwawekea wholesale price ili sisi tununue rejareja.
 
Nitoke Morogoro au Igunga kufuata mkaa wa buku. Hakika nitakuwa qualified inmate wa Mirembe.

Sambaza mkaa wako kwenye maduka na supermarkets kwa kuwawekea wholesale price ili sisi tununue rejareja.
Samahan mkuu sikujua kama uko mbali!
 
wateja wako wa kila siku ni hawa

i.wauzaji chips hakikisha una zungukia sehem zote zinazo uza chips huwez kukosa oda kila siku
ii. tembelea vyuo mbali mbali zile canteen za vyuo hua wanapendelea matumiz ya mkaa mbadala kuliko huu wa kawaida
iii. tembelea migahawa mikubwa na midogo maeneo ya manzese magomeni kkoo mpaka posta
bila kuwasahau mama ntilie na mabar yaliyo jazana kila kona hapa mjini

Sent from my SM-G950U using JamiiForums mobile app
 
Asante kwa ushauri
 
Samahan mkuu sikujua kama uko mbali!
Tupe majibu. Mtu akitokapoint A kufuata mkaa point B, anarudishiwa gharama za nauli?

Majibu yalenge mkaa unapatikana vipi. Katila majibu epuka neno NJOO UUFUATE na fananizi na hayo
 
Weka picha mkuu,

Anzia mbande kisewe mpaka mvuti..chanika na E.t.c
 



Jambo zuri, ila kuna tu NGO tujanja njaja tunajidai tunasaidia local community wanauza sana, kwa hiyo sio jambo jipya sana.

Jaribu kutafuta watu wa mazingira mkae nao, ongea nao, share idea, uone kama watavutwa na huo uwekezaji.

Ila si kitu kipya, nafikiri back in 2010 hiyo NGO walikuja oficin kuomba tuwafadhili, tukawafadhili, usiwaze kwamba ni jambo jipya, unaingia kwenye soko la ushindani.

Ila kila la heri, determination compete with anything
 
Je una constant supply ya material ya kutengenezea huo mkaa mbadala?
 
Peleka sample mashuleni kama atlas... Kuna kipindi walikuwa wananunua ule anaozalisha mchina wenye tundu katikati
 
Tupe majibu. Mtu akitokapoint A kufuata mkaa point B, anarudishiwa gharama za nauli?

Majibu yalenge mkaa unapatikana vipi. Katila majibu epuka neno NJOO UUFUATE na fananizi na hayo
Mkuu nazani hatukuelewana sahivi nipo kwenye kujua soko ili nijue nauzaje
 
👏👏👏
 
Mkaa halisi unauzwa wapi? Je tatizo ni soko au watumishi hawana uelewa wa bidhaa yako? Watumishi wa mkaa wako popote pale.
 
Mkuu nazani hatukuelewana sahivi nipo kwenye kujua soko ili nijue nauzaje
Poa nimekupata.

Ukishapata soko ukaanza kuutengeneza tujulishe point of sales za mkaa wako.

KWa sasa hivi tunakupa nafasi ujadiliane na maafisa masoko wa humu😄
 
Upo wapi mkuu!?
 
Unaelekea kupiga ela Kama utawekeza kwenye marketing mkaa wako uingie kwenye mzunguko. Serikali ishatoa projection by 2025 tuepukane na matumizi ya mkaa na kuni, jaribu kuset standard ya bei yako ya mkaa isizidi matumizi ya gas each item for a month, utatoboa uswahilini wanaamini ukipika ubwabwa kwenye gas unakuwa sio mtamu kama wa kwenye mkaa.
 
Asante kwa ushauri ndugu angalau napata mwanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…