Wapiga kura tusichague wacheza kamari uchaguzi ujao, watoto wetu wanaathirika

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Kamari zimetapakaa hadi kwenye vitongoji vya vijijini kila mahali penye umeme nchini. Redio zote kuanzia za umma na watu binafsi zote ni kamari tu. Kijijini nimeshuhudia kijana kauawa kwenye dubwi kwa kugombea TSH 4000 tu wakati wakibishana juu ya nani amekula, ni za nani.

Wanafunzi wanabet hata ada za shule, na dereva wa bodaboda wanabeti pesa ya hesabu ya tajiri. Wakulima wanabet pesa walizopata baada ya kuuza mazao na mifugo.

Vijana wanabet hata siku na muda wa kazi, bila shaka uchumi utashuka sana kama hatua kali hazitachukuliwa kuhusu kamari.

Tusichague wagombea ambao ni maarufu kwa betting, wataliangamiza taifa, tuwaogope kama ukoma.
 
CC: kwa Mgombea wa Kinondoni
Epukeni influencers wa kamari kuwa role models wa vijana kwa kuwaacha waende bungeni. Tutajenga kizazi cha hovyo kabisa.
 
Kwahiyo asipochaguliwa ndo anaacha kazi ya kamari
 
NRNE
 
Mngekua mmezikataa baiskeli ndio tungeweelewa lkn madam mnazo mpaka mmezipindisha mataili ya mbele ma nyuma october lazima mtick
 
Kwanamna hii mchango chanya kwa taifa utsonekana,ila uchaguzi wenyewe unakupa hiyo fursa ya kufanya uamuzi huo?Endapo ungeoelewa ile maana yaNRNE ingeeleweka vyema zaidi
 
Issue ya kamari ni very controversial, on one hand wanasiasa wanapitisha Sheria ya kuruhusu kamari na kukusanya Kodi, on the other hand wanashauri tusicheze kamari
 
Kama akina Babalevo
 
Kwanamna hii mchango chanya kwa taifa utsonekana,ila uchaguzi wenyewe unakupa hiyo fursa ya kufanya uamuzi huo?Endapo ungeoelewa ile maana yaNRNE ingeeleweka vyema zaidi
Mpaka sasa hujangundua bado kuwa NENR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…