sio kwetu tu dunia ya tatu, lakini hata Trump alishikishwa adabu baada ya kuandamana bila kujali tume ilifanya vizuri au la, sembuse akina Lisu wa Tanzania? Trump kaambiwa asishiriki siasa milele kwenye nchi iliyokamaa kwa demokrasia. Ndugu zangu hakuna nchi nyingiine itatuambia sisi aina ya demokrasia ya kufuata mbali na sisi wenyewe kuamua aina ya demokrasia kwa kuzingatia our local context, utamaduni, mila na desturi zetu. Katika utawala wowote jambo na kazi kubwa mtawala ni kuhakikisha kuwa waliowengi wako hai na salama baaasi, yaliyobaki ni nyongeza (secondary) tu. Ndio maana China inauambia ulimwengu kuwa robo ya watu wote duniani wako China na kazi yake ya msingi ni kuhakikisha kuwa watu hao (wachina) wanapata mahitaji yao ya msingi kwa maisha, sio demokrasia ya kutenda na kusema. Hebu fikiria kama Wachina wakipewa uhuru mpana wa kusema na kutenda kama tunaoutaka sisi hapa kungekalika?