Wapinzani anzeni upya, Rais Samia ni mpya pia

Sehemu kubwa ya hotuba ilikuwa haiwahusu wahutubiwa! Ulaya hamna maandamano baada ya uchunguzi wala mikutano ya kisiasa baada ya uchaguzi, kwa sababu wanaamini tume zao nazo zinaaminika, kisemwacho na tume ni sahihi, ilitokea Marekani baada ya tume kuboronga watu waliandamana. Hivyo watu wakidhulumiwa lazima walalamike, sasa kutaka watu uwadhulumu na wakae kimya, hapo nashangaa!
 
An old wine in a new glass. Teh!
 
Mama anataka kuongelewa lugha ya kimama anasahau anatawala nchi na jambo la utawala limekaa kibaba zaidi. Hatutoongea sauti kutokea puani kamwe. Alisikika mwanachadema mmoja
 
sio kwetu tu dunia ya tatu, lakini hata Trump alishikishwa adabu baada ya kuandamana bila kujali tume ilifanya vizuri au la, sembuse akina Lisu wa Tanzania? Trump kaambiwa asishiriki siasa milele kwenye nchi iliyokamaa kwa demokrasia. Ndugu zangu hakuna nchi nyingiine itatuambia sisi aina ya demokrasia ya kufuata mbali na sisi wenyewe kuamua aina ya demokrasia kwa kuzingatia our local context, utamaduni, mila na desturi zetu. Katika utawala wowote jambo na kazi kubwa mtawala ni kuhakikisha kuwa waliowengi wako hai na salama baaasi, yaliyobaki ni nyongeza (secondary) tu. Ndio maana China inauambia ulimwengu kuwa robo ya watu wote duniani wako China na kazi yake ya msingi ni kuhakikisha kuwa watu hao (wachina) wanapata mahitaji yao ya msingi kwa maisha, sio demokrasia ya kutenda na kusema. Hebu fikiria kama Wachina wakipewa uhuru mpana wa kusema na kutenda kama tunaoutaka sisi hapa kungekalika?
 
Mkuu KATIBA ni haki ya kila mtanzania SIO fadhila za Rais wa nchi,na katiba hii inatuletea madikiteta na viongozi wasiowajibika kwa watu but kwa no 1,always katiba inadaiwa sio kupewa
 
Mama anataka kuongelewa lugha ya kimama anasahau anatawala nchi na jambo la utawala limekaa kibaba zaidi. Hatutoongea sauti kutokea puani kamwe. Alisikika mwanachadema mmoja
Anaesema hivyo hakumuona mzazi wake wa kike (mama yake), labda mama yake alikufa akiwa mdogo, au mama aliwakimbia watoto wakiwa wadogo. Sisi kwetu tumezaliwa wanaume 5 lakini hatukuwahi kusema kwa ukali na mama eti kwasababu ni mama (mwanamke), tulikuwa tunatii na kuheshimu. Ndiyo maana demokrasia yetu na mambo yetu lazima pia yafuate tamaduni zetu. Mfano, kwa kawaida, desturi na mila zetu, akina mama wana huruma na kusamehe zaidi kuliko wanaume, hivyo Rais wetu kwakuwa ni mwanamke sintashangaa kuona watu wengi wanaoonewa (awimo mbowe) wakipata ahueni sana chini ya utawala wake. Lakini kauli za ubabe, za kupaza juu, za kejeli, za mkato kwa Rais mwanamke inaweza kutafsiriwa kama kumtweza kama mwanamke sio kama Rais.
 
Tena huyu Maza alikuwa Tulia katika bunge hilo la katiba
 
Mkuu KATIBA ni haki ya kila mtanzania SIO fadhila za Rais wa nchi,na katiba hii inatuletea madikiteta na viongozi wasiowajibika kwa watu but kwa no 1,always katiba inadaiwa sio kupewa
Ni kweli kabisa unachosema, lakini sasa ni miaka 60 tangu tupate uhuru, mbona hiyo Katiba unayoitamani wewe ije haipo? Mbona kejeli, nguvu na jaziba za kuleta katiba (UKAWA) hazijafanikiwa kuandika katiba mpya hadi sasa? Hii ni kuonyesha kuwa tugeukie mazungumzo (dialogue) zaidi na nia njema kuliko ncha ya upanga katika kuleta katiba mpya.
 
Nimekupata!
 
Mama na Magufuli ni kitu kimoja, dhambi na hukumu yao ni moja.
 
Nimekupata!
Hata Marekani na Uingereza wana shida kubwa ya Katiba zao na tume za uchaguzi. baadhi ya majimbo yanadhani kuwa yanaonewa au kubanwa au kubinyiwa haki zao kwenye muungano na wakati wa uchaguzi. Pale Uingereza Ireland inataka kujitenga, lakini hawaji kwetu kulalamika maana watajadiliana wenyewe kwa mujibu wa desturi zao na maisha yanaendelea. Hata sisi tufuate njia hii ya msalaba katika kuijenga nchi yetu ambayo ni yetu sote mpaka wale ambao hawajazaliwa bado.
 
Hata mimi nataka serikali 3, Tanganyika iache kujiita Tanzania na kuikoloni Zanzibar.
 
Hata mimi nataka serikali 3, Tanganyika iache kujiita Tanzania na kuikoloni Zanzibar.
Hiyo itakuwa sawa na mgombea uchaguzi wa Marekani aseme kama nitachaguliwa kila jimbo nitalipa uhuru wake kamili. Mgombea huyo atakufa hata kabla ya siku ya kupiga kura. Hapa Tanzania mojawapo ya mambo ambayo serikali ya CCM inalazimika kushinda uchaguzi kwa lazima ni pamoja na kulinda Muungano wa Serikali mbili. Lazima vyama vyote vya siasa viachane na agenda ya kujadili muungano na mapinduzi ya Zanzibar. Hiyo lazima kama taifa bila kujali vyama tukubali kuwa hiyo ndiyo historia yetu na hatima yetu kama taifa, kama wazee walikosea huko nyuma kuhusu muungano tukubali kuwa walikosea kwa niaba yetu sote, sawasawa na wazazi wetu walivyotuchagulia makabila, dini, na majina yetu.

Kama tunataka tupige makitimu ya hapohapo kwenye demokrasia basi vyama viendelee na agenda ya serikali 3, CCM itatafuta kila njia ya kubaki madaraki kwaajili tu ya zuia wahuni wanaotaka kuuvunja muungano na mapinduzi ya zanzibar. Serikali 3 hatakuja sasa wala kesho wala kesho na wewe na mimi tutanaiga dunia kabla serikali 3 hazijakuja kama vile Maalim Seif alivyoondoka bila mafanikio.

Kumbukeni kuwa kilichokwamisha mchakato wa kuandika katiba ni ulevi wa UKAWA na woga wa CCM wa kuvunja muungano wetu. Hata mchakato wa katiba ukianza tena aina ya muungano isiguswe hata kidogo, vinginevyo hatutafika mwisho tena.
 
kama wazee walikosea huko nyuma kuhusu muungano tukubali kuwa walikosea kwa niaba yetu sote.
Tukubali walikosea kisha tufanye marekebisho pale walipokosea. Hatuna sababu yoyote ya kuendeleza makosa yao. Mimi ninachoamini kila chenye mwanzo hakukosi kua na mwisho Wazanzibari tayari wameshaelewa wanatawaliwa na Tanganyika huu sio Muungano, tufike pahala tukaae chini tufanye Muungano wa kweli, huku kuikalia nchi yao kijeshi hakuna mwisho mzuri.
 
Kilicho
Toa mfano wa Muungano uliorekebishwa upya ukapona na kusimama tena. Na hapo unaposema wewe ndipo chanzo cha unaoitwa udikteta wa watawala unapoanzia. Vyombo vyetu vya dola, ulinzi na usalama havitakuwa na kazi nyingine kubwa zaidi ya kulinda muungano na mapinduzi dhidi ya wakora wa aina yako.
 
Mwisho wake ni wewe kuondoka duniani na kuiacha tanzania chini ya ccm. CCM inabakizwa madarakani na walevi wasioutaka muungano. Maana wanufaika na muungano wa aina hii ni wengi na watu muhimu kuliko wanaodhani hawanufaiki nao. Na hakuna Rais atakaekubali muungano ufie mikononi mwake inyeshe mvua litoke jua.
 
Rasimu ya warioba ilipendekeza serikali tatu. Ukawa ilitokana na ccm kutaka kuleta rasimu yao ambayo sio maoni ya wananchi.Mama samia alikuwa makamu mwenza wa bunge la katiba. Waliovuruga bunge la katiba ni ccm ambao walibadirisha maoni ya wananchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…