Wapinzani chezeni karata zenu kwa umakini sana kutokana na Rais tuliyenaye sasa hivi

Wapinzani chezeni karata zenu kwa umakini sana kutokana na Rais tuliyenaye sasa hivi

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Posts
11,837
Reaction score
17,412
Katika nyakati ambazo Wapinzani wanatakiwa wawe makini basi ni nyakati hii.

Ni nyakati ya wapinzani kaucha jazba na kuwa wastaarabu sana na wenye kujenga hoja bila MIHEMKO.

Kwa sababu sasa hivi sio kwamba CCM ni saafi saaaaaana laa hasha, sababu ni kuwa mama anacheza karata zake kwa utulivu na ustaarabu.

Mama ni mtu anayeheshimika na Watanzania wa rika, vyama na dini zote, Watanzania wote wanamjua kwamba ni mtu mstaarabu na mtu mwenye staha ya maneno.

Hivyo mtakapojifanya wazalendo sana, mtakapojifanya mnakuja na maneno ya jeuri kwa sababu ya uhuru wa kuongea basi mtajiharibia kwa Watanzania wengi sana.

Mama anaongea kwa ustaarabu wewe unakuja na kauli za kifedhuli hoja yako haitaonekana kitakachoonekana ni hizo kauli zako mbovu.

Mukitaka mumuweze mama sasa hivi basi mnnatakiwa muwe humble kuliko nyakati zote kwa sababu sasa hivi tuna Rais wa aina nyingine kabisa.

Ushahidi ni kwa Mdude anavyojifanya shujaa na maneno yake Watanzania wengi wanamuona hana adabu kwa sababu ya rais aliyekuepo sio wa dizaini hizo.

Sio kwamba CCM imesafika saaana bali huyu mama ni mtu muungwana, hivyo lazima mufanye siasa za kiungwana sana.
 
Mimi nakuelewa mleta mada. Dhana yako ni kwamba wapinzani wakiwa wapole sana mwenyekiti wa ccm kwakuwa naye ni mpole kwa maumbile na hulka yake basi kuna siku atawahurumia wapinzani awapatie katiba mpya. Hell No! Narudia tena Hell No!.

Huyu mama kama angekuwa ni rais atokanaye na mgombea binafsi au angetokea CHADEMA basi katiba angetupatia ndani ya siku 100 za utawala wake. Lakn kwakuwa anatokana na kundi la walafi wa madaraka la CCM, kamwe msitegemee.

Hawa walafi wa CCM ndiyo waliombadilisha JK daikika za mwisho kabisa za mchakato wa kupata katiba mpya 2014. JK alikuwa na dhamira ya dhati kabisa ya kutupa katiba mpya lkn manyang'au hawa wakamwabia wee!
 
Mm nakuelewa mleta mada. Dhana yako ni kwamba wapinzqni wakiwa wapole Sana mwenyekiti wa CCM kwakuwa naye ni mpole kwa maumbile na hulka yake basi kuna siku atawahurumia wapinzani awapatie katiba mpya. Hell No! Narudia tena Hell No!
Lakini mkuu katiba mpya akitaka kufanya huo mchakato ni hisani yake tu na wala sio lazima yeye kufanya.

Unadhani kwa nini katiba mpya isiwe hisani yake endapo ataamua?
 
Lakini mkuu katiba mpya akitaka kufanya huo mchakato ni hisani yake tu na wala sio lazima yeye kufanya.

Unadhani kwa nini katiba mpya isiwe hisani yake endapo ataamua?
Atazuiwa na wahafidhina wa chama chake. Hawa ndiyo hawataki kusikia ishu ya katiba mpya.

Na mama lazima awaogope wahafidhina maana wanaweza ku-,tamper na safety and securiity ya rais.
 
Katika nyakati ambazo wapinzani wanatakiwa wawe makini basi ni nyakati hii.

Ni nyakati ya wapinzani kaucha jjazba na kuwa wastaarabu sana na wenye kujenga hoja bila MIHEMKO...
Sasa ngoja waje uone utasikia sukumagang. Wakati huu ushauri ni wa msingi sana.

Huu ndio wakati wa kula na kipofu Ila watakuja kujimwambafai mpaka wamkere aamue kuwa liwalo na liwe wakati mwenzao ameshika mpini wao wameshika makali, akivuta tu wameumia.
 
Kwa m
Mm nakuelewa mleta mada. Dhana yako ni kwamba wapinzqni wakiwa wapole Sana mwenyekiti wa ccm kwakuwa naye ni mpole kwa maumbile na hulka yake basi kuna siku atawahurumia wapinzani awapatie katiba mpya. Hell No! Narudia tena Hell No!...
Kwa matusi ya vijana wa CHADEMA? Wacha tuendelee hivihivi tu aisee, kila ukishauri unaishia kutukaniwa mpaka wazazi.

I've never been a fan wa CCM Ila kwa sasa it's enough hakuna uelekeo acha tujiunge na hao CCM sasa tuibe tu wanetu waishi vizuri maana upinzani haupo serious zaidi ya kutukanana mitandaoni tu na hoja zilizokosa strategy.

Nilichogundua kwa nchi hii, bado sana tunapotezeana muda tu. Heri kuiba maisha yaendelee wajinga ndio waliwao.
 
Mimi pia mzee, upinzani wetu ni majanga, waulize kama hii katiba iliyopo wamewahi hata kuisoma, hawajuhi hata kumuheshimu mwanamke, Mbowe should talk to his guys
Wanatukana tu. Now I know better. Ukiasoma comments zangu nilikuwa nasapoti sana Ila ni ujinga na kupoteza muda umri umeenda tunadeal ni vijana waiojua kuweka timeframe kwamba tufanye nini kwa muda gani ili tuwe sehemu fulani.

Yani tunaishia kutukanana tu, tunaacha kujadili strategy za muhimu ili kupata ushawishi wa namna ya kupata Katiba mpya.

Ni matusi tu. Pathetic.
 
Kwa m

Kwa matusi ya vijana wa CHADEMA? Wacha tuendelee hivihivi tu aisee, kila ukishauri unaishia kutukaniwa mpaka wazazi.

I've never been a fan wa CCM Ila kwa sasa it's enough hakuna uelekeo acha tujiunge na hao CCM sasa tuibe tu wanetu waishi vizuri maana upinzani..
Kwa hali hii ya upinzani wa Mbowe, wa kelele na matusi kama desturi yao,kumbe covid 19 wako sahihi walichokifanya kukimbilia Bungeni na kuwaacha walivyo. Na Hayati Magufuli alikuwa sahihi tu kuwabana. Hawafai.mama asiwalegezee.
 
Tatizo CHADEMA siasa zao ni zile zile za harakati as if tupo utumwani, kwa style ya mama CHADEMA wangalie sana wataishia kupiga kelele Twitter, mtaani watu hawaelewi cause mwendazake katupa funzo watanzania Sasa basi CHADEMA wasipokuwa makini wataishia kupasikia bungeni cause jamii ishapitia taabu na mateso Sasa kwa jinsi mama alivyo jamii ipo tayali kusema tunamtaka uyu uyu twende naye
 
Naaam kabisa mkuu sasa hivi hakuna namna mama anaonekana msafi,mstaarabu na muungwana achilia mbali kuteleza kibinadamu lakini anajulikana kwamba sio fedhuli wa kauli.

Na jambo hili ndio watu kama chadema wanashindwa kuelewa.

Sasa mtu anasema "hatukubali kumpa muda"

Sawa hukubali kumpa muda ndo utafanya nini sasa zaidi ya kupiga kelele ?
 
Atazuiwa na wahafidhina wa chama chake. Hawa ndiyo hawataki kusikia ishu ya katiba mpya.

Na mama lazima awaogope wahafidhina maana wanaweza ku-,tamper na safety and securiity ya rais.
Hayo ni mawazo yako mkuu.

Pia nimekuuliza kuwa unadhani kwa nini isiwe ni hisani yake mama ikiwa atataka kutekeleza mchakato wa katiba mpya ?

Kwa sababu sio lazima kwake kutekeleza mchakato huo kwa sasa,aamue kwa wema wake tu.
 
Kwa hali hii ya upinzani wa Mbowe, wa kelele na matusi kama desturi yao,kumbe covid 19 wako sahihi walichokifanya kukimbilia Bungeni na kuwaacha walivyo. Na Hayati Magufuli alikuwa sahihi tu kuwabana. Hawafai.mama asiwalegezee.
Walichofanya chadema ni wivu tu kuwavua uanachama wabunge wao.

Hii katiba tuliyonayo ndio iliwaweka akina mbowe bungeni na hii hii ndio ikawatoa bungeni.

Wakati wapo bungeni walilalamika pia kwamba kura zinaibiwa lakini hatukuona wakijivua uanachama au kuacha ubunge kwa sababu wao walikuwa wapo wanakula posho ati.

Ndo tunazema upinzani nao wanatafuta ulaji,kwa mantiki hiyo 19 wale wako sahihi maana wameusoma mchezo wa wenzao kwamba wakiwa hawajapata wanasema tususieeeeee ili wakose wote,wakipata waaaooo tupiganieeee
 
Kwa m

Kwa matusi ya vijana wa CHADEMA? Wacha tuendelee hivihivi tu aisee, kila ukishauri unaishia kutukaniwa mpaka wazazi.

I've never been a fan wa CCM Ila kwa sasa it's enough hakuna uelekeo acha tujiunge na hao CCM sasa tuibe tu wanetu waishi vizuri maana upinzani haupo serious zaidi ya kutukanana mitandaoni tu na hoja zilizokosa strategy.

Nilichogundua kwa nchi hii, bado sana tunapotezeana muda tu. Heri kuiba maisha yaendelee wajinga ndio waliwao.
Kumbe na wewe ume experience.

Alafu mbaya zaidi hawa wanavyama hawajui kama kuna watu ambao hatusapoti chama kwa sababu ya chama bali tunasapoti chama kwa sababu ya hoja.

Kwa maana tunaangalia hoja hatuangalii imetoka wapi,hivyo tunakuwa free minded kukosoa mtu yeyote yule bila kuangalia ufuasi wa chama.

Wapinzani ukiwakosoa wanadhani wewe ni CCM,wana mawazo mgando ya kizamani kwamba hawatakiwi kukosolewa,wanadhani kila mtu anaangalia chama.

Kwa mtindo huu wa kudhani kila anaewakosoa ni ccm ndivyo wanazidi kupoteza points zao kwa sisi wananchi ambao hatuna ushabiki,kwenye nyeusi tunakubali nyeusi na nyeupe tunakubali nyeupe
 
Lakini mkuu katiba mpya akitaka kufanya huo mchakato ni hisani yake tu na wala sio lazima yeye kufanya.

Unadhani kwa nini katiba mpya isiwe hisani yake endapo ataamua ?
Huu ni ukweli mchungu.

Watakupinga sana lakini huu ndio ukweli ndugu yangu.
 
CHADEMA wanatoa wrong approach kwa nature ya Rais tuliye naye huwezi tumia maneno makali ka enzi za jpm na Sasa Raia wakakuelewa zaidi ya kujiharibia, hafu CDM wengi Wana mchukulia Samia kiudhaifu vile ni mwanamke wakadhani niwepesi, Samia has been fair to our country na ni msikivu Sana kafanya mengi ndani ya siku 100 why provoking her na ubabe loh CDM acheni kupima maji ya kina kirefu kwa miguu, hafu mnataka kumharibia utendaji wake kwa kufanya vitu kusudi ili kumharibia Hadi kwa hisani, siku mama akigeuka na kuwa hatari kuliko jpm mtanyooka tu.
 
Kwa m

Kwa matusi ya vijana wa CHADEMA? Wacha tuendelee hivihivi tu aisee, kila ukishauri unaishia kutukaniwa mpaka wazazi.

I've never been a fan wa CCM Ila kwa sasa it's enough hakuna uelekeo acha tujiunge na hao CCM sasa tuibe tu wanetu waishi vizuri maana upinzani haupo serious zaidi ya kutukanana mitandaoni tu na hoja zilizokosa strategy.

Nilichogundua kwa nchi hii, bado sana tunapotezeana muda tu. Heri kuiba maisha yaendelee wajinga ndio waliwao.
Sikuhizi too much mihemko na matusi na hamna anayejenga hoja mbadala imegeuka genge la wahuni
 
Mimi pia mzee, upinzani wetu ni majanga, waulize kama hii katiba iliyopo wamewahi hata kuisoma, hawajuhi hata kumuheshimu mwanamke, Mbowe should talk to his guys
Wanaongelea Mambo yasiyo gusa wananchi kisa madaraka hata hii katiba ni nzuri licha ya mapungufu yake ila mbona ilikuwa inavunjwa tu vizuri na hawKufanya chochote.
 
Kwa hali hii ya upinzani wa Mbowe, wa kelele na matusi kama desturi yao,kumbe covid 19 wako sahihi walichokifanya kukimbilia Bungeni na kuwaacha walivyo. Na Hayati Magufuli alikuwa sahihi tu kuwabana. Hawafai.mama asiwalegezee.
COVID-19 wanaangalia maisha yao in the next 5 years. Hiyo ndio desturi yetu sasa na hapo wapinzani wamefikishwa na Mbowe na genge lake.

Kuna yule binti mdogo mdogo anaitwa Asia/Aisha Mohamed aliegombea ubunge wa ukonga, Nusrat Hanje wamefight kinoma lakini hola. Wakaangalia wakaona shit, liwalo na liwe lakini hapa hakuna ndoto za Chadema kuja kuongoza nchi hii. Umri unakwenda, majukumu yanaongezeka. Potelea mbali haooooo wameelekea Zak bungeni.

Wao wamebaki wasaliti wasaliti wasaliti.
 
Back
Top Bottom