Mkuu, hapa unaweza tukanwa mpaka kijiji ulichosoma aiseee, hahahaha
Yani ushauri wa bure tu kwamba watumie karata yao vizuri maana strategy waliyotumia hapo nyuma Rais aliyekuwepo aliwakomesha na walifyata wote. Tuliwaonea huruma sana hata siasa hawakufanya na hata mishahara hawalipwi kwa sasa wanatembeza mabakuli kuombaomba tu.
Chama hakina miradi inayoingiza pesa zaidi ya kutegemea pesa za wahisani, wahisani walibanwa akina Sabodo wakafilisiwa ikabidi warudi CCM tu. Leo tunawashauri mambo ya msingi ili kuondoa utegemezi ambao chama kikikosa uhisani basi kiendelee kuwa na pesa zake za kutoka kwenye miradi yake.
Angalia leo hata kama CCM waliiba viwanja vya mpira Ila viwanja vya mikoa vyote ni vya CCM, wenzetu ukiacha kwamba wana serikali Ila hata huko kwenye mamiradi wanayo pesa nyingi mno, mashamba, majengo ya upangishaji, vyuo nk.
Sasa jaribu kuwashauri vijana wa CHADEMA wao hawatakaa kutafakari effect ya ushauri wako watakutukana tu.
Sasa hiyo ni level ya watu wa chini sana, hiyo haiwezi kuwa siasa ambayo unategemea in 5/10 years watapewa nchi. Never.
Hatuwezi kuongozwa na wahuni, nimekuwa nasapoti sana wapinzani, Ila kwa hii, hapana nchi haiendeshwi na genge la machokoraa, lazima kujipanga.
CCM wanaona sababu wanatumia mbinu za kisiasa ya hali ya juu, unawachokoslza then wao wanakujibu halafu wanakaa kimya hawajibizani tena na wanawaacha muendelee na hilo kumbe wao wamehamia kwingine. Mnabaki na kupiga domo at the end unasikia uchaguzi umefika na hakuna aliyeweka strategy ya kushinda zaidi ya vurugu tu.
Nchi haiwezi kuendeshwa na watu wa namna hiyo. Wasipobadilika waendelee tu na siasa zao.