Katika nyakati ambazo Wapinzani wanatakiwa wawe makini basi ni nyakati hii.
Ni nyakati ya wapinzani kaucha jazba na kuwa wastaarabu sana na wenye kujenga hoja bila MIHEMKO.
Kwa sababu sasa hivi sio kwamba CCM ni saafi saaaaaana laa hasha, sababu ni kuwa mama anacheza karata zake kwa utulivu na ustaarabu.
Mama ni mtu anayeheshimika na Watanzania wa rika, vyama na dini zote, Watanzania wote wanamjua kwamba ni mtu mstaarabu na mtu mwenye staha ya maneno.
Hivyo mtakapojifanya wazalendo sana, mtakapojifanya mnakuja na maneno ya jeuri kwa sababu ya uhuru wa kuongea basi mtajiharibia kwa Watanzania wengi sana.
Mama anaongea kwa ustaarabu wewe unakuja na kauli za kifedhuli hoja yako haitaonekana kitakachoonekana ni hizo kauli zako mbovu.
Mukitaka mumuweze mama sasa hivi basi mnnatakiwa muwe humble kuliko nyakati zote kwa sababu sasa hivi tuna Rais wa aina nyingine kabisa.
Ushahidi ni kwa Mdude anavyojifanya shujaa na maneno yake Watanzania wengi wanamuona hana adabu kwa sababu ya rais aliyekuepo sio wa dizaini hizo.
Sio kwamba CCM imesafika saaana bali huyu mama ni mtu muungwana, hivyo lazima mufanye siasa za kiungwana sana.