Uchaguzi 2020 Wapinzani mnatambua kabisa Rais Magufuli ni mtendaji, mchapa kazi na mtekelezaji mzuri. Bado hamuoni aibu kuchukua fomu za urais!

Watanzania wana akili na macho. Wanaona kwa macho Sgr itayokamilika hivi karibuni(Dar to Moro) .Wanaona kwa macho yao kuwa ndege 8 zimenunuliwa kwa cash.
Ununuzi wa Ndege kwa cash una ufisadi mkubwa ndiyo maana walimtoa CAG kafara baada ya kuhoji, SGR ina ufisadi kampuni za Naibu Bashite na wana CCM wenzako ndizo zimepewa Tenda zote muhimu pesa inazunguka inawarudia wenyewe hapo hapo ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi.
 
We utakuwa hauko sawa kiakiri.
 
Watetezi wa CCM msiwe na haraka ngoja kampeni zianze msikie maovu yote ya CCM ndipo mtajua CCM ni ile ile hawajatubu chochote.
 
Huu ushamba sijui utaisha lini. Yaan mtu analazimisha mtu mwingine awaze kama yeye. Huu ni uzuzu
 
Watanzania wana akili na macho. Wanaona kwa macho Sgr itayokamilika hivi karibuni(Dar to Moro) .Wanaona kwa macho yao kuwa ndege 8 zimenunuliwa kwa cash.
Watanzania wapi unawasemea? Watanzania wako binafsi hako nyumbani kwako? au watanzania wote ambao wameamka wanajua uovu na uonevu wote wa CCM?
 
Jenga hoja acha kututoa kwenye Reli tukaja na Lugha ya kukuudhi ukasirike bure
Habari ya kupigwa risasi Tundu Lissu inaingia vipi? Maana Dk Mollel alishatoa majibu kuwa Chadema mnahusika. Sasa analeta habari gani?
 
Kwa nini ushiriki uchaguzi wakati hata yule unaepambana nae unamkubali kuwa anauwezo wa kufanya kazi kiutendaji kuliko wewe? Angalia mtu kama Nyalandu body language inaonyesha anamkubali JPM 100%.
Ndiyo mfumo wetu wa uchaguzi ulivyo na huu mfumo uko kikatiba/kisheria. Lakini pia kibinadamu, mtu hawezi kupata 100% bila kufanya mtihani kwa kufikiri tu kuwa fulani ni mwanafunzi bora. Kufanya mtihani na kushinda kwa kupata mfano 100% kunaongeza confidence kwa mwanafunzi aliyefanya mtihani. Hata kwenye upigaji kura ni hivyo, mgombea anayeshiriki uchaguzi na kupigiwa kura kwa zaidi ya 50% na wapiga kura ina maana huyo atayechaguliwa anakuwa na confidence kwamba wapiga kura wengi (kitakwimu) wana imani naye, kuliko anayepitishwa bila kujua ame'perform' kwa kiasi gani kwenye uchaguzi.

Mpiga kura anayeshiriki uchaguzi na akaona mgombea aliyempigia ameshinda anapata confidence ya kushiriki zaidi kwenye chaguzi nyingine zijazo. Lakini pia kwa mgombea ambaye anashiriki uchaguzi na kupoteza inampa confidence namna ya kujijenga zaidi. Anaweza akaona sehemu ambayo alizembea ili arekebishe na kufanya vizuri zaidi kwa chaguzi nyingine zijazo. Na ndivyo pia ilivyo kwa wapiga kura ambao mgombea wanayempigia ameshindwa, wataendelea kushiriki wakitumaini kwamba siku moja mgombea wao anaweza kushinda pia. Yaani ndivyo tunavyowapata viongozi wetu katika ngazi mbalimbali. Kama kuna watu wawili: mmoja akipita bila kupingwa na kufanywa kuwa kiongozi wa nchi bila kupiga kura na mgombea mwingine kushiriki mchakato na kuibuka mshindi, unadhani psychologically nani atapata faraja zaidi moyoni mwake? Yule ambaye hana hata takwimu za kujua alishinda kwa kiwango gani au yule anayejua jinsi alivyopambana na hata hivyo akaibuka mshindi?
 
Watanzania wapi unawasemea? Watanzania wako binafsi hako nyumbani kwako? au watanzania wote ambao wameamka wanajua uovu na uonevu wote wa CCM?
Chama kinachoonea wananchi hakiwezi kufanya maendeleo mkubwa kama haya. Angalia umeme vijini 85%. Mtu anapata kwa 27000 tu.
 
Yule anayepita bila kupingwa lakini ni mchapakazi na mtu anayetekeleza bora asipingwe. Ni kupoteza muda na pesa kupambana na kiongozi kama huyu. Msiwakariri wazungu.
 
Du Kuna thread zingine, no wonder hata mwanakijiji siku hizi haandiki Tena makala hapa maana. Tumeacha kutumia akili badala take tunatumia mikia kuwaza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…