Uchaguzi 2020 Wapinzani mnatambua kabisa Rais Magufuli ni mtendaji, mchapa kazi na mtekelezaji mzuri. Bado hamuoni aibu kuchukua fomu za urais!

Kitendawili cha nani anakatisha haki ya baadhi ya watanzania kuishi kikitenguliwa nitakubaliana au kukukatalia assertion yako
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana. Badala ya kujiandaa kwa raha utakayopata Magufuli akiwashinda wapinzani kwa 100% katika sanduku la kura, unataka kuikimbia burdani hiyo?

Wenzako Yanga huwa wanakesha kwa matarajio tu ya kutoka sare na Simba wakasakate kigodoro usiku kucha, wewe umepania kuweka mpira kwapani? Acha mchecheto; acha Magufuli aonje kibano cha kura, kabla ya kutangazwa mshindi kama ilivyokuwa 2015. Acha hizo SGR, JNHPP, dreamlinerz ziongee zenyewe.[emoji44]
 
Mnafahamu kuwa JPM ni jembe na linatekeleza maendeleo kwa ajili ya watanzania na hao wagombea wenu hawana sifa za kupambana na JPM. Hamuoni aibu kufanya huo mchakato?
Hata angekuwa koleo kupingwa muhimu, hata kama tume ni hii inayoongozwa na mgombea acha muone hisia za wananchi .

Pili hakuna la maana alilofanya kiasi asilinganishwe na watu wengine. Nimeacha kuemo humu siku mbili nimekuta umetupia utumbo huu !! Daahh [emoji87]
 
Kitendawili cha nani anakatisha haki ya baadhi ya watanzania kuishi kikitenguliwa nitakubaliana au kukukatalia assertion yako
Kama kuna extrajudicial killings hapa Tanzania mbona wewe na ukoo wenu mpo mnapeta?
 
Jaduong najua mambo mazuri aliyofanya unayakubali kimoyomoyo. Ngoja baada ya mradi wa JNHPP kukamilika uanze kufurahia matunda.
Hao wagombea wenu wanapoteza muda tu.
 
Jaduong najua mambo mazuri aliyofanya unayakubali kimoyomoyo. Ngoja baada ya mradi wa JNHPP kukamilika uanze kufurahia matunda.
Hao wagombea wenu wanapoteza muda tu.
Ndiyo democracy, acha wapoteze muda. Kuacha kuweka mgombea ni usaliti kwa ma democrat . Ingekuwa hivyo akina Trump na wengine wasingepingwa
 
Ndiyo democracy, acha wapoteze muda. Kuacha kuweka mgombea ni usaliti kwa ma democrat . Ingekuwa hivyo akina Trump na wengine wasingepingwa
Na hapo watanzania wengi wanapokosea. Kufananisha siasa za Tanzania na Ulaya au Usa.
Hapa Tanzania Ccm ni chama cha watanzania wanyonge sio chama cha matajiri kama Republican. Ndio maana upinzani unaangukia pua.
 
Onghwise, mimi Ccm nimeanza nayo 1975 nikiwa mwana Tanu youth League na baadaye chipikizi wa chama kipya cha Ccm 1977. Hicho cha zamani kilikuwa cha wananchi. Na watu hawakulazimishwa kukipenda. Kila mtu alijiona mwana Ccm. Lakini hii ya leo ina wenyewe, na kama siyo mwana Ccm hata kinafki unahujumiwa kwa kila kitu. Kwa Nyerere hatukuwa hivi.

Swala la upinzani kutokuwa na uwezo ni maoni yako. Na huwawakilishi WaTz kwa ujumla wao. Acha Maghufuli apingwe hata kama system italazimisha kura kutokutosha.
 
Acha mpambano uendelee we shida yako Nini?Kama undhani amefanyia Mambo mzuri nchi.wapiga kura wataamu.by the way si amepitishwa peke yake huko ccm?
Kama angekuwa amefanya mengi mazuri, CCM isingempitisha peke yake wangeruhusiwa na wanachama wengine wachukue Fomu ili wakatupwe mbali na vikao vya juu Kama ilivyo kawaida. Hiyo ingemuimarisha dhidi ya wapinzani lakini kwa kuwa miaka 5 amefanya madudu tu, Chama chake kimeogopa atatupwa nje na wanachama wenzake kabla hata ya kufikia kuteuliwa kuwakilisha Chama. Kufukuzwa Membe ni thibitisho la uoga huo.
 
Unaumwa kichwani, na hauko sawa, kapime labda una kisonono kilichoathiri mpaka ubongo wako.
 
Jaduong Ccm ipo makini inapofanya makosa inajirekebisha. Hii Ccm ya sasa ni kama ya mwl JKN haina mwenye chama au tajiri wa kuimiliki. Na kusema wananchi wanalazimishwa kuipenda sio kweli.Maana matokeo chanya ndio yanawafanya waipende. Kama hospital ya mkoa wa Mara imekaa zaidi ya miaka 30 haijakamilika. Leo hii Ccm wameikamilisha kwa nini watu wa huko kwenu wasiikubali!
 
Nonsense.
 
Mbona wewe huoni aibu kupost uzi kama huu,wakati unaona utendaji wa yesu wenu unafaa.
 
Mara ina matatizo mengi sana kuwadanganya na peremende ya hospital na ambayo ipo mkoani, na mkoa wenyewe ukiwa umetawanyika ni kama tone la maji masafi ndani ya bahari iliyojaa matatizo.

After all kuyafanya yote hayo ni wajibu wa wanaoshikilia dola. Kwani ni kazi walioiomba. Na wanalipwa kwa kazi hiyo . Na hii haimfanyi asipingwe
 
Jaduong kushikilia dola na kuwatumikia wananchi ni swala jingine. Kuna Marais wanahamisha pesa na kupeleka Uswiss. Lakini JPM amejitoa watu wa mara mpate hospital ya rufaa ya mkoa. Kuliko kusafiri mpaka Mwanza. Mnatakiwa mkubali JPM anatekeleza.
 
C

Kumkubali ni issue nyingine na haiondoi ukweli kuwa lazima vyama vingine viweke wagombea . Kitu kizuri huchaguliwa miongoni mwa vingine. Asin'gang'anie kuonekana kuwa kafanya maajabu yasiyopingwa
 
CKumkubali ni issue nyingine na haiondoi ukweli kuwa lazima vyama vingine viweke wagombea . Kitu kizuri huchaguliwa miongoni mwa vingine. Asin'gang'anie kuonekana kuwa kafanya maajabu yasiyopingwa
Hivyo vingine viko wapi miongoni mwa vitu vizuri? Hajafanya maajabu bali ametekeleza kile wananchi wanataka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…