Hayati JPM alikuwa na mapungufu yake ila pia alikuwa na mambo mazuri.
Sisi wapinzani huwa tunakosoa kwa kuangalia shilingi upande mmoja tu
Sasa tokea amefariki huyu hayati JPM wamachinga ni watu wa kuumizwa tu. Kuhamishwa hovyo bila hata mikakati, masoko yao kuungua huku wengine wakila virungu.
Wapinzani tujipange kuwatetea na hii hoja tuikomalie 2025.
Hatuwezi kuendesha nchi kwa kutumia same level of thinking.
Machinga ni wasaliti wakubwa wa upinzani hapa nchini kwetu, hawajawahi kusimamia hoja zao na kutafuta a permanent political side itakayowasemea matatizo yao.
Machinga wamejibrand kama wao ndio wenye nchi na kama eti wao ndio walipakodi ingali masikini kote hakuna anayetaka risiti ya EFD Wala huku mabarabarani.
Machinga wamevamiwa na viongozi wao wanaojivika kuwasemea machinga ingali hao watu ni vibaraka wa CCM.
Machinga amegeuzwa mtaji wa kisiasa wa CCM. Wanatulizwa wakati wa uchaguzi na uzuri wake nao wamekuwa kama bendera kufuata upepo.
Machinga akipewa elfu tano wakajazwa kwenye malori kama nyanya wanazouza na kupelekwa kwenye mikutano ya CCM wao huwa wamemaliza kura yao pale na kuuza utu wao.
Machinga haaminiki sababu ya kuwaza kutetea tumbo na sio kutetea hali halisi ya ugumu wanaokutana nao kwenye maisha ya kila siku na kusaidia vizazi vijavyo.
Machinga hafahamu kwamba, anayekuja kukurubuni kwa elfu tano hajawahi kuwa machinga hivyo hajui adha ya umachinga na mahitaji ya machinga ili kubadilisha hali waliyonayo kwa sasa kuanzia mitaji, masoko mpaka muundo wa Kodi na tozo wanazopaswa kulipia.
Hivyo binafsi siwaonei huruma Hawa watu sababu wengi wapo CCM na wanaform vijiwe vya CCM wanaweka Tawi kwa kupandishwa bendera ili wapate CCM protection na wakishatimuliwa ndio huwa wanakuja kulalamika kutafuta sympathy kwa wananchi tunapambana kweli kutafuta haki na usawa.
Machinga ni mtaji wa CCM mie nilishawaweka kwenye group la wasaliti.