Wapinzani pelekeni hoja nzito kwa wananchi, sio blaa blaa za Bandari

Wapinzani pelekeni hoja nzito kwa wananchi, sio blaa blaa za Bandari

Haa haa just haa haa.! Mmeshindwa kutetea LIMKATABA LIBOVU mnataka sasa na sisi tunao upinga tunyamaze. Halafu maisha yaendelee. Hili la kuuza bandari si sawa na la kuuza madini. Hakuna mwenye akili timamu atanyamazia hili. Mkataba ni MBOVU, UFUTWE. Ni LAZIMA UFUTWE.
#OkoaBandariZetu
Hakuna demokrasia kwa watu maskini kama sisi. Demokrasia inamruhusu mtu kuwachochea watu maskini waichukie serikali yao maskini isiyokuwa na fedha za kuwahudumia kikamilifu. Kama Kuna Rais wa nchi maskini ataikumbatia sana demokrasia kiongozi huyo lazima ataanguka, na hata yule atakaemuangusha pia Hana Cha maana atakachowafanyia wananchi kwakuwa shida sio kiongozi bali mifumo mibaya ya fedha na biashara ya dunia.
 
Peleka wewe hzo hoja , kama rasilimali zinagawiwa hovyo Kwa watu wengine hayo maji utayapataje we kiazi
Ona Sasa akina Halima na wenzake wamewabwanga kihalali kambisa. Ukijamba kwa hasira utajinyea.
 
Acha kudanganya watu wewe wapi umeona kuna ubadhilifu, wapi kuna ukosefu wa pembejeo kwa wakulima, wapi kuna ukosefu wa maji mpaka wapinzani waandamane kupinga vitu hivyo? Hii nchi hakuna shida chini ya utawala wa CCM🤣🤣🤣🤣🤣
Kuna ukweli fulani kwenye hilo. Watanzania shida yao kubwa sio CCM bali mfumo wa uchumi wa dunia usiotoa nafuu hata kidogo kwa nchi za Afrika. mali za Afrika zinaibiwa na ni lazima ziibwe bila kujali ni chama gani kinatawala. ndio maana hata nchi zilizobadilisha vyama bado zimesalia palepale na vilevile na hivyohivyo, tena wakati mwingine wananchi wanaweza kuhisi ni heri wangebakia na chama walichokiangusha. Wanchi wa Liberia walidhani wakimchangua Mtu maarufu kama George Weah kuwa Rais wataogelea kwenye dimbwi la raha na nafuu, lakini cha ajabu hata mpira wao haukunyanyuka. Ruto hivyohivyo, Chikwera kule malawi hivyohivyo, na kwingine hali yao imebaki ileile au chini zaidi.

Waafrika tusidanganyane kuhusu demokrasia, shida yetu kuu sio ukosefu wa demokrasia bali wizi wa maliasili zetu, ukosefu wa mitaji na technologia vinavyosababisha tuwe tegemezi, ombaomba wa misaada na wakopaji wakuu. tukae chini sote tuangalie tutafanye. Labda vyama vyetu vya siasa kwenye kampeni na ilani zao vishindane tu namna bora ya kukusanya kodi na kuongeza mapato, kuzuia rushwa, kuzuia wizi wa mali za umma na namna ya kutumia fedha za mikopo na kupunguza matumizi tu basi; kwakuwa hakuna serikali ambayo haitakopa, ni uongo kuwaambia watu kuwa wakikuchagua wewe hautakopa, ni kudanganya wananchi.
 
Back
Top Bottom