Pre GE2025 Wapinzani wa Tanzania wasaidiwe kuachana na siasa za kufikirika!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Motivational speaker hebu kaa kimya, huu ushauri wako mpelekee Zito ndio alijifanya anafanya siasa za hoja, ila ppl akiingia kwenye uchaguzi wenzake wanakuja na mabox ya kura huku polisi na maafisa wa tume wakishuhudia hilo. Unaita ccm ni chama imara, kisha vyombo vya dola ndio vinatumika kuilinda ccm kubaki madarakani kwa shuruti! Anzisha chama uchukue hiyo fursa na ufanye hizo siasa za hoja, kisha ikifika uchaguzi uone kura zinazoletwa kwa mabox ni ngapoli.
 
😄

Multiparty imetushinda

Hamas Walikuwa Chama Cha Upinzani huko Palestine

Zelenesky ni Rais kutoka Chama Cha Upinzani huko Ukraine

Labda ndio sababu watanzania hawapendelei Vyama kama CUF
kwa ulaya hawana mifumo ya chama kimoja kuhodhi madaraka , ko ndan ya ulaya kila mtu ni mpinzani , angalia hatua waliyopo. ila rudi Afrika ni disaster
 
Mbona alishasema na inajulikana! Jinsi ya kuokoa hii nchi ni kuruhusu mgombea binafsi. Ili kujiondoa katika makucha ya vyama vya siasa
 
ama kweli nyani haoni kundule..yaani umekaa kuandika andiko refu hivi kuwananga vyama vya upinzani..eti ooh hawako serious kushika dola,ooh hawana hoja,ooh upinzani hakuna watu wa maana kupewa nchi..yanini ww kujitoa ufahamu hali ya kuwa mfumo mzima wa uchaguzi unaufahamu upo upande gani kuanzia tume ya uchaguzi na viongozi wake wanavyopatikana,wasimamizi na watangaza matokeo pia sheria na kanuni za uchaguzi wenyewe ikiwemo matumizi ya polisi..haya yote unayajua na mabaya mengine mengi tu..na ww unajua maovu yoote ya mfumo wa uchaguzi na yanayofanywa nyuma ya pazia na chama dola na serikali yake ila ww unajidai huyaoni ila unawananga wapinzani eti hawana nia kuingia ikulu au kufanya siasa serious wakati wakijaribu kufanya hizo siasa za ukweli mnawatumia polisi waliovaa kivita utegemee maajabu gani toka kwao.. wekeni uwanja sawa na haki wa uchaguzi muone..ila mm nimekuelewa sana kwani watu dizaini yako pascal kuwa mnatumiwa na mifumo dhalimu kufanya spinning ili kunufaisha kikundi fulani..ningekuwa sikujui kwa kukuona kwenye TV ww mzee ninge kutukana kwa hili andiko lako lililojaa unafiki..
 
Chama cha mapinduzi hakishindi uchaguzi wowote, na hakitashinda, kinatumia nguvu ya dola na rasilimali za umma na sheria mbovu walizotunga wenyewe na kujitangazia ushindi usio halali.
 
Yote uliyoandika yanataka watu! Kama wakala wako anapewa elfu 10 ajanywe soda anaachia fisi bucha unataka suluhisho gani? 2020 uchaguzi uliibiwa kwa uzembe uzembe wa mezani. Vyama havilipi mawakala, vyama haviandai watu makini wa kusimamia zoezi la kujaza fomu tumeyaona hayo kwenye serikali za mitaa!

Mi nilidhani mtu kama Lissu alivyokua akitokwa povu atakua na suluhisho ya Yale aliyolaumu wenzake kushindwa ndo mmepata suluhisho la No Reform No Election? Haya Leo anasema bila bunduki hamuwezi iondoa CCM kwahyo atanunua bunduki?
 
🤣🤣🤣!😭😭😭 ivi Tz upzani miaka yote bdo awajui wanaitaji nn wameshndwa kuwa na sera makini, kuwa na watu wenye nguvu ya ushawishi kwa mfano ili kukubalika popote pale lazma ufanye zaidi ya mwezako kuwa na sera inayo mgusa mwananch mmoja baada ya mwngne kuangalia uzaifu wa ccm maana ccm n zaifu sana ila upzani aupo sriaz
 
Nadhani ulipokuwa unaandika Makala hii Nafsi Yako ilikuwa inakusuta! Deep down in your heart unajuawa kati ya chama tawala na Chadema nani ni dhaifu na muoga. Njaa mbaya sana!
 
Mayala hauna hoja. Eti miaka 30 upinzani umeshindwa kushika dola!? Kuna uchaguzi wa haki unafanyika Tanzania kwanza ili uweze kutoa hizo lawama zako. Je, ccm na serikali sio kitu kimoja!? Vimewahi kutengenishwa!? Hapo bado wapinzani wanaambiwa wamekosea kujaza fomu. Na wengine wanatekwa kipindi wanaenda kurudisha fomu. Mayalla ni afadhali ukae kimya. Unazeeka vibaya Aisee!
 
JPm anawaambia wakurugenzi, nakuteua mimi, nakulioa mshahara halafu umtangaze mpinzani!? Je hapo kuna uchaguzi!? Sometimes mpumguze kujitoa akili.
 
Kama wanaiba ruzuku JPM na roho yake mbaya dhidi ya wapinzani mbona hakuwafunga magerezani kwa kutumia vyombo vyake vya Takukuri na polisi!? Acha porojo!
 
Umeandika kama mgeni kwenye nchi hii! Yaani ni kama Mkenya aliyekuja kututembelea siku 2 na kuona jinsi tunavyongea kuhusu vyama vingi vya siasa au kuhusu CHADEMA! Wewe kama mcha-mbuzi wa maswala ya kisiasa ungeenda mbali zaidi kujadili mfumo wa upigaji na Usimamizi wa kura hapa kwetu jinsi ulivyo! Hayo yote uliyoandika hayasaidii katika kuhesabu kura! Ligeuze andiko lako liwe CCM inahitaji kusaidiwa katika kusimamia uchaguzi hapa nchini! Hebu waweke wasimamizi huru wa uchaguzi au waombe US ije isaidie kusimamia uchaguzi na mwezi ujao uitishwe uchaguzi bila hata kampeni uone kama CCM itaambulia kitu! Wako pale kwa kusaidiwa na mapolisi yasiyojitambua!
 
Ntapinga mpaka mwisho mtu anayesema vyama vya siasa vya upinzani haviaminiki kwa umma wa Tanzania, ukweli ni kwamba umma wa Tanzania haujapatiwa haki ya kuwa huru kuchagua na kupewa matokeo kwa vipindi kadhaa vya uchaguzi toka mfumo wa vyama vingi uanze
 
Ni kero kubwa pale ambapo watu wazima na werevu wanapoamua kufanya unafiki makusudi.

Inajulikana wazi kuwa ccm haishindi uchaguzi kwa box la kura bali kwa wizi?!

Hizi propaganda zinazofanywa na machawa wa ccm zinastahili kupuuzwa na umma wa Watanzania.

Kama wapinzani ni dhaifu kweli acheni uchaguzi uwe huru na haki washindwe kihalali..


View: https://x.com/Nipashetz/status/1746897669929292081?t=sCKgMQBF86NDG5E9Jma40w&s=19
 
Kama upinzani ni dhaifu ni kwanini polisi wanawekwa katika vituo vya kupiga kura?
Ni kwanini anaetangazwa na tume kuwa ni mshindi ndiye mshindi hata kama amepata 20% ya kura zote na kesi hawezi kupingwa mahakamani?
Hapo ng'wanangwa ameandika kama amekatwa kichwa! Sana sana anaandika huku anapulizia kwa kuvizia uteyuzi! Tuna wachambuzi wa hovyo kabisa nchi hii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…