Pre GE2025 Wapinzani wa Tanzania wasaidiwe kuachana na siasa za kufikirika!

Pre GE2025 Wapinzani wa Tanzania wasaidiwe kuachana na siasa za kufikirika!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe la Leo.
View attachment 3246218
Kiukweli kabisa, upinzani Tanzania una hali mbaya sana, uko dholfu bin taaban kwa kukosa watu wa mikakati, hivyo kuendelea kufanya siasa za kiharakati kwa kutumia utopian politics!, badala ya kufanya siasa za kimikakati, matokeo yake ni kushindwa vibaya, na ni kwa zaidi ya miaka 30, upinzani umeshindwa kushika dola, upinzani huu unatakiwa kusaidiwa, bila kusaidiwa, uchaguzi wa 2025, unakwenda kuwa kama uchaguzi wa 2020, Bunge la 2025 litakosa tena kambi rasmi ya upinzani Bungeni, matokeo yake ni hasara wote, CCM, Nchi na Watanzania kwa ujumla.

Kukosekana kwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, kumepelekea kuwa na Bunge legelege, lisilo na uwezo wa kuisimamia serikali kikamilifu!. Bunge hili limekuwa linapitisha kitutusa, kila linacholetewa na serikali!.

Tungekuwa na wapinzani makini mule Bungeni, yale baadhi ya madudu ya ajabu.ajabu yaliyopitishwa na Bunge letu, kama kama ule Mkataba batili, kisha kuletewa muswada batili wa sheria mpya ya uchaguzi na kutunga kuwa sheria huku inakwenda kinyume na katiba yetu, yasingepita kabisa kirahisi ki vile!.

Leo nazungumzia umuhimu wa Tanzania kuwa na upinzani makini, upinzani imara na upinzani wa kweli kwa maendeleo ya taifa, bila kuwepo kwa upinzani imara, upinzani makini, hakutakuwa na CCM imara!, kwasababu imethibitishwa pasipo shaka, nchi zenye upinzani legelege, hupelekea vyama tawala kubweteka kwa kukosa changamoto, hivyo upinzani makini, imara na wa ukweli ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Hili limethibishwa na hili Bunge ambalo ni kama Bunge Rubber Stempu, linapitisha kila kitu hata madudu ya ajabu ajabu, hivyo kukosa msisimko, ili Bunge lichangamke, lazima baadhi ya wapinzani makini waingie Bungeni, Bunge lijalo liwe na kambi rasmi ya upinzani. Wapinzani wasiposaidiwa, uchaguzi wa 2025, utakuwa kama uchaguzi wa 2020!.

Kazi ya upinzani makini na upinzani wa kweli ni kupinga kwa kutumia hoja mbadala, na sio kupinga tuu ili mradi unapinga, upinzani makini unapinga kwa kutumia nguvu ya hoja na sio hoja za nguvu, unapinga kwa hoja kwa kupangua hoja kwa hoja na wakati huo huo unaweka hoja mbadala ili kutoa changamoto kwa chama tawala kuwa tunakuangalia, ukishindwa unaondolewa!.

Upinzani wetu hapa Tanzania, una tatizo kwa wapinzani karibu wote, hawana hoja mbadala za kushindanisha na hoja za serikali, hivyo kuonekana kama upinzani wa kupiga tu kelele nawapinzani wengine karibu wote ni wapinzani wa kupinga tuu kila kitu bila kuwa na hoja mbadala, matokeo yake ni tuna upinzani uchwara usiotimiza majukumu ya upinzani makini, matokeo yake CCM kuutumia udhaifu wa upinzani wa aina hii kujiimarisha, uchaguzi mkuu wa 2025 upinzani usiposaidiwa, uchaguzi huu ni CCM tena!.

Kwa kuanzia kwanza tujifunze upinzani makini na wa kweli ni nini, unatakiwa kufanya nini, na upinzani legelege na uchwara ni nini, unafanya nini, kwanini Tanzania hatuna upinzani makini?

Tanzania tuna vyama 21 vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

Lengo kuu la vyama vyote vya siasa, ni kushika dola na kuongoza serikali yaani kutawala. Kila chama kinaandaa ilani yake ya uchaguzi kwa kueleza iwapo kitapewa ridhaa ya kutawala na wananchi, kupitia uchaguzi huru, na wa haki, kitafanya hivi na vile katika maeneo haya na yale.

Kazi ya chama tawala ni kuongoza serikali kwa kutumia ilani yake ya uchaguzi. Baada ya uchaguzi, kazi ya upinzani makini duniani kote ni kupinga sera za chama tawala kwa hoja mbadala na sio kupinga tuu alimradi kupinga.

Hii imeifanya Tanzania kuwa na chama kimoja kikuu chenye nguvu, CCM ambacho ni kama dola, na vyama utitiri vya upinzani vinavyofanya siasa za uchwala, hali inayopelekea hakuna serious people wenye kutaka mabadiliko ya kweli, wanaweza kuviaminia kuvikabidhi nchi kutokana na kujikita kwenye siasa uchwara za matukio na kupinga tuu kila kitu badala ya kujikita kwenye siasa za kujenga hoja.

Upinzani makini unatakiwa kupinga hoja za serikali kwa hoja mbadala zenye mashiko, kwa upinzani huu wa kupinga tuu bila mbadala, nani atawaaminia wapinzani na kuwapa ridhaa?.

Nimemsikiliza TAL kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV kuhusu falsafa yake ya No Reforms No Election.

Japo hakuna ubishi kuhusu umahiri wa TAL kama mwanasheria, mwanasiasa, mbunge, mnadhimu mkuu wa upinzani, M/Mwenyekiti wa Chadema, lakini TAL kama Mwenyekiti wa Chadema, ana strengths zake, (umahiri), ila pia ana madhaifu yake ambayo anahitaji msaada mkubwa kusaidiwa na watu wenye uwezo wa kusaidia, ili Tundu Lissu, Chadema na wapinzani wengine, waweze kubadilika na kuachana na siasa za kiunaharakati na badala yake kufanya siasa za kimikakati ya kujiandaa kutawala.

Hivyo vibwagizo vya kiuanaharakati, kama “no reforms no election” vibwagiza hadaa (utopian politics) visivyotekelezeka!. Chadema na wapinzani wote, lazima wajikite kwenye kufanya siasa za ukweli, (real politics) ambazo ni siasa za mikakati, (politics of engagement), vinginevyo uchaguzi wa 2025, mambo ya 2020 yanakwenda kujirudia, na itakuwa ni CCM tena!.

Hivyo natoa wito, kwa Watanzania wowote wazalendo wa kweli wa nchi hii, na wenye mapenzi mema na nchi yetu, wenye uwezo, wa kuwasaidia wapinzani, na kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL ili aweze, na kuisaidia Chadema ili iweze na pia kuwasaidia wapinzani wengine wote kufanya siasa za ukweli za kutaka kushika dola.

Kwenye kipindi hicho, TAL alipoulizwa maandalizi ya uchaguzi, amesema Chadema haifanyi maandalizi yoyote bila reforms ni no election!. Hizi ni utopian politics, sii TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi Mkuu usifanyike!.

Natoa wito, kwa watu wowote, wenye uwezo, kutoka popote hata wana CCM, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, kwa kuishauri kuwa uchaguzi mkuu wa 2025, Chadema ina fursa!, hii ni fursa adhimu na fursa adimu kwa Chadema kuichangamkia, muda uliobaki kabla ya uchaguzi, sio rafiki kufanya siasa za kiharakati, huu ni muda wa kufanya siasa za kimikakati ya ushindi, tena namshauri TAL na Chadama wakumbatie falsafa ya pragmatism politics, wawe pragmatic and do what is possible!.

TAL na Chadema na wapinzani wengine wote, wasaidiwe waachane na utopian politics, wafanye real politics, the time is almost too little too short!, hakuna muda wa kupoteza!.

Paskali.
Huwezi kushindana na mwizi kwa kukesha ili asikuibie.P wafikishie wezi ujumbe huu wakisha upata ujumbe,mada yako itajivika uhusika na uzito wake ipasavyo.
 
Lissu anafikiria vitu kutoka kichwani kwake bila ya kuelewa wapo hatua gani ya uelewa. Watanzania wengi hawajui kama wao ndio wenye na wafanyakazi wa serikali ni waajiri wao. Sasa utamshawishi mtu vipi kudai mabadiliko hata elimu ya haki haijui. Mbaya zaidi haki zake zipo kwenye katiba ambayo kila siku mnaiita mbovu as if kila kitu kibaya.

Story ni ndefu ila Lissu sio mwanasiasa na upinzani bara bado; Zanzibar tayari.

Lissu ni ‘demagogue’ wanna be lakini hana rhetoric ya kuongea na watanzania kwa kuwaelewa kwanza, hana political strategy ya muda mrefu. Yeye anadhani kilichopo kichwani kwa either unakubaliana nae au, basi na watanzania wote wenye shida wanatakiwa kuwa na mtazamo huo-huo. Hizo siasa anazohubiri muda wake Tanzania bado, yupo lala land.

Wewe unasema ‘No reforms, no election’, huko ndani ya CCM kauli hiyo wanaitafsiri kama ‘kuvuja kwa pakacha, nafuu kwa mchuuzi’.

CDM ni useless
Mkuu Meya Kwimbi Mayor Quimby ,watu kama wewe ni watu muhimu sana,hili bandiko linakuhusu!,unatakiwa kujitolea kusaidia,Asante kwa mchango huu,TAL anatakiwa asome hapa!

P
 
Bro ..
Rejea Uchaguz wa 2020(uchaguzi mkuu) na 2024 (serikal za mitaa),yaliyotendeka..
Ungeshari strategy ipi hapo tuwe na uchaguz huru na haki?

Mbona hauzungumzii mapunguf ya kikatiba na tume ya uchaguzi?

Mbona hauzungumzii kata kata ya wagombea wa upanzani tu na sio wa Ccm?

Kwakuwa wewe pia ni mtanzania na naamini umepita darasani na una nia njema kabisa na chi yako,embu walau tupe briefly baadhi ya "Strategy" za kufanya au kuingia kwenye chaguzi ilihali katiba na tume ya uchaguzi ziko au zinabaki kama zilivyo..

Utakuwa umeitendea haki elimu yako, nchi na familia yako.
Mlamba asali hawezi ona hayo mapungufu kapigwa upofu chezea njuruku wewe
 
View attachment 3246603

Apple ndio kampuni iliyozindua first ever modern tablet mwaka 1993 ikiitwa ‘Apple Newton’ ilikuwa touch screen computer na inaweza text.

IBM wakaenda mbele zaidi wakaja na first ever touch screen mobile phone 1994 ikiitwa ‘IBM Simons’.

Hizo bidhaa zote mbili zilifeli vibaya sana sokoni miaka ya 90 kwa sababu technology ilikuwa mbele ya muda. Apple ilifisika kabisa kwa sababu walitumia hela nyingi kwenye research ya hiyo PDA, ikabidi ‘Bill Gates’ awape mkopo kwa sababu aliamini uwepo wa kama washindani utachochea technology innovation.

Hizo bidhaa za Apple na IBM zilizo fail miaka ya 90, leo technology hiyo hiyo tunaita smart technology na ndio dominant sokoni.

Somo ni nini elewa wananchi wanataka nini na wako wapi (marketing research) kwanza kabla ya kutengeneza bidhaa. Changes za kitu kigeni zinataka baby steps, kufikia ukileta kitu kipya kabisa kinaenda fail hata kama ni bora.

Lissu anafikiria vitu kutoka kichwani kwake bila ya kuelewa raia wapo hatua gani ya uelewa. Watanzania wengi hawajui kama wao ndio wenye nchi na wafanyakazi wa serikali ni waajiriwa wao. Sasa utamshawishi mtu vipi kudai mabadiliko hata elimu ya haki yake haijui. Mbaya zaidi haki zake zipo kwenye katiba ambayo kila siku mnaiita mbovu as if kila kitu kibaya.

Story ni ndefu ila Lissu sio mwanasiasa na upinzani bara bado; Zanzibar tayari.

Lissu ni ‘demagogue’ wanna be lakini hana rhetoric ya kuongea na watanzania kwa kuwaelewa kwanza, hana political strategy ya muda mrefu. Yeye anadhani kilichopo kichwani kwake either unakubaliana nae au, basi na watanzania wote wenye shida wanatakiwa kuwa na mtazamo huo-huo. Hizo siasa anazohubiri muda wake Tanzania bado, yupo lala land.

Wewe unasema ‘No reforms, no election’, huko ndani ya CCM kauli hiyo wanaitafsiri kama ‘kuvuja kwa pakacha, nafuu kwa mchuuzi’.

CDM ni useless
Nawewe usikae mno kwenye nadharia za mambo bila kujua wapi panafaa ku-apply hizo nadharia. Hivi wewe mtoto wako utamwacha ale mavi kwasababu unasema bado ni mtoto kwasasa hana akili, mpe atakacho?! Lissu anafanya kazi nzuri kuwaelimisha wanachi, kuwazindua, kuwatoa kwenye ujinga, wajielewe wapi wapo. Badala na yeye kuendelea kuwatafuna wananchi mpaka hapo watakapozinduka (panya hufanya hivyo), yeye anawazindua. Huo ndio ujinga wa CHADEMA ama huo ni ujinga wako wewe na CCM?
 
sawa mke wangu kwa kunipangia niwe mwanachama wa chama kipi kesho naomba unipangie nguo za kazini pia uninyooshee tumeelewana mke wangu
Si unaona ulivyo. Watu kama wewe mnatakiwa mkae kimya muongozwe wapi pa kwenda au sio?
 
Kwani Tanzania sasahivi Kuna kampeni na vyama vimeshapitisha manifesto?

Nafikiri wewe ndiye mtoto Kama sio mtoto niwekee hapa manifesto ya ccm 2025!!
Umesharukia huku tena hapo kinajadiliwa nini nawewe ulisema nini? Hapa sasahivi unaongea nini? Kuna chama kinaingia kwenye chaguzi bila manifesto? Hapa tunazungumzia manifesto? Una akili za kima wewe
 
Nawewe usikae mno kwenye nadharia za mambo bila kujua wapi panafaa ku-apply hizo nadharia. Hivi wewe mtoto wako utamwacha ale mavi kwasababu unasema bado ni mtoto kwasasa hana akili, mpe atakacho?! Lissu anafanya kazi nzuri kuwaelimisha wanachi, kuwazindua, kuwatoa kwenye ujinga, wajielewe wapi wapo. Badala na yeye kuendelea kuwatafuna wananchi mpaka hapo watakapozinduka (panya hufanya hivyo), yeye anawazindua. Huo ndio ujinga wa CHADEMA ama huo ni ujinga wako wewe na CCM?
Mkitoka hapo mnaanza kulaumu Simba na Yanga sijui inapumbaza wananchi. Mara bongo flavour ni tatizo ndio maana wananchi hawafuatulii siasa. Badala ya kukubali tatizo ni kukosa mbinu za siasa.

Hivi unadhani huko kwenye dunia ya watu walioendelea kwanini wanaajiri reputable marketing firms kama ‘Saatchi & Saatchi, Cambridge Analytica and the likes na kuwalipa mamillioni kwenye uchaguzi ili kuwapa wanasiasa mbinu za kufikisha ujumbe wao.

Tanzania kila kitu rahisi.

Hakuna anaempangia Lissu cha kufanya, lakini hiyo ni failed mission kabla ya kuanza.
 
Mkitoka hapo mnaanza kulaumu Simba na Yanga sijui inapumbaza wananchi. Mara bongo flavour ni tatizo ndio maana wananchi hawafuatulii siasa. Badala ya kukubali tatizo ni kukosa mbinu za siasa.

Hivi unadhani huko kwenye dunia ya watu walioendelea kwanini wanaajiri reputable marketing firms kama ‘Saatchi & Saatchi’ and likes na kuwalipa mamillioni kwenye uchaguzi ili kuwapa wanasiasa mbinu za kufikisha ujumbe wao.

Tanzania kila kitu rahisi.

Hakuna anaempangia Lissu cha kufanya, lakini hiyo ni failed mission kabla ya kuanza.
Ila huwaga una ujinga mwingi sana

Serikali haikubali tume huru alafu unawalaumu wapinzani

Polisi wanaingiza kura feki kwenye vituo vya kupiga kura alafu unawalaumu wapinzania

Unajua hakuna mtu wa hovyo hapa duniani kama waafrika

Uchaguzi wa mwaka 2020 kuna wagombea wa upinzani walipigwa, waliteswa na kutupwa porini kosa lao ni kutumiza haki yao ya kikatiba alafu unawalaumu wapinzani tena
 
Hakuna anaebishia hayo malalamiko.

Kinachozungumziwa ni mbinu za kufikirika katika harakati za kutafuta fairness.

Ukisusa wenzako wanaendelea na Lissu hana ushawishi wa kuingiza hata 1% ya watanzania barabarani kwa akili za watanzania wa leo. Sasa sio kwamba wanafurahishwa na mazingira yao ya shida.

Vita mbinu, sio kwenda kichwa kichwa tu kama Lissu.
 
Wanabodi,
Hii ni makala yangu kwenye Gazeti la Nipashe la Leo.
View attachment 3246218
Kiukweli kabisa, upinzani Tanzania una hali mbaya sana, uko dholfu bin taaban kwa kukosa watu wa mikakati, hivyo kuendelea kufanya siasa za kiharakati kwa kutumia utopian politics!, badala ya kufanya siasa za kimikakati, matokeo yake ni kushindwa vibaya, na ni kwa zaidi ya miaka 30, upinzani umeshindwa kushika dola, upinzani huu unatakiwa kusaidiwa, bila kusaidiwa, uchaguzi wa 2025, unakwenda kuwa kama uchaguzi wa 2020, Bunge la 2025 litakosa tena kambi rasmi ya upinzani Bungeni, matokeo yake ni hasara wote, CCM, Nchi na Watanzania kwa ujumla.

Kukosekana kwa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, kumepelekea kuwa na Bunge legelege, lisilo na uwezo wa kuisimamia serikali kikamilifu!. Bunge hili limekuwa linapitisha kitutusa, kila linacholetewa na serikali!.

Tungekuwa na wapinzani makini mule Bungeni, yale baadhi ya madudu ya ajabu.ajabu yaliyopitishwa na Bunge letu, kama kama ule Mkataba batili, kisha kuletewa muswada batili wa sheria mpya ya uchaguzi na kutunga kuwa sheria huku inakwenda kinyume na katiba yetu, yasingepita kabisa kirahisi ki vile!.

Leo nazungumzia umuhimu wa Tanzania kuwa na upinzani makini, upinzani imara na upinzani wa kweli kwa maendeleo ya taifa, bila kuwepo kwa upinzani imara, upinzani makini, hakutakuwa na CCM imara!, kwasababu imethibitishwa pasipo shaka, nchi zenye upinzani legelege, hupelekea vyama tawala kubweteka kwa kukosa changamoto, hivyo upinzani makini, imara na wa ukweli ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.

Hili limethibishwa na hili Bunge ambalo ni kama Bunge Rubber Stempu, linapitisha kila kitu hata madudu ya ajabu ajabu, hivyo kukosa msisimko, ili Bunge lichangamke, lazima baadhi ya wapinzani makini waingie Bungeni, Bunge lijalo liwe na kambi rasmi ya upinzani. Wapinzani wasiposaidiwa, uchaguzi wa 2025, utakuwa kama uchaguzi wa 2020!.

Kazi ya upinzani makini na upinzani wa kweli ni kupinga kwa kutumia hoja mbadala, na sio kupinga tuu ili mradi unapinga, upinzani makini unapinga kwa kutumia nguvu ya hoja na sio hoja za nguvu, unapinga kwa hoja kwa kupangua hoja kwa hoja na wakati huo huo unaweka hoja mbadala ili kutoa changamoto kwa chama tawala kuwa tunakuangalia, ukishindwa unaondolewa!.

Upinzani wetu hapa Tanzania, una tatizo kwa wapinzani karibu wote, hawana hoja mbadala za kushindanisha na hoja za serikali, hivyo kuonekana kama upinzani wa kupiga tu kelele nawapinzani wengine karibu wote ni wapinzani wa kupinga tuu kila kitu bila kuwa na hoja mbadala, matokeo yake ni tuna upinzani uchwara usiotimiza majukumu ya upinzani makini, matokeo yake CCM kuutumia udhaifu wa upinzani wa aina hii kujiimarisha, uchaguzi mkuu wa 2025 upinzani usiposaidiwa, uchaguzi huu ni CCM tena!.

Kwa kuanzia kwanza tujifunze upinzani makini na wa kweli ni nini, unatakiwa kufanya nini, na upinzani legelege na uchwara ni nini, unafanya nini, kwanini Tanzania hatuna upinzani makini?

Tanzania tuna vyama 21 vya siasa vyenye usajili wa kudumu.

Lengo kuu la vyama vyote vya siasa, ni kushika dola na kuongoza serikali yaani kutawala. Kila chama kinaandaa ilani yake ya uchaguzi kwa kueleza iwapo kitapewa ridhaa ya kutawala na wananchi, kupitia uchaguzi huru, na wa haki, kitafanya hivi na vile katika maeneo haya na yale.

Kazi ya chama tawala ni kuongoza serikali kwa kutumia ilani yake ya uchaguzi. Baada ya uchaguzi, kazi ya upinzani makini duniani kote ni kupinga sera za chama tawala kwa hoja mbadala na sio kupinga tuu alimradi kupinga.

Hii imeifanya Tanzania kuwa na chama kimoja kikuu chenye nguvu, CCM ambacho ni kama dola, na vyama utitiri vya upinzani vinavyofanya siasa za uchwala, hali inayopelekea hakuna serious people wenye kutaka mabadiliko ya kweli, wanaweza kuviaminia kuvikabidhi nchi kutokana na kujikita kwenye siasa uchwara za matukio na kupinga tuu kila kitu badala ya kujikita kwenye siasa za kujenga hoja.

Upinzani makini unatakiwa kupinga hoja za serikali kwa hoja mbadala zenye mashiko, kwa upinzani huu wa kupinga tuu bila mbadala, nani atawaaminia wapinzani na kuwapa ridhaa?.

Nimemsikiliza TAL kwenye kipindi cha dakika 45 cha ITV kuhusu falsafa yake ya No Reforms No Election.

Japo hakuna ubishi kuhusu umahiri wa TAL kama mwanasheria, mwanasiasa, mbunge, mnadhimu mkuu wa upinzani, M/Mwenyekiti wa Chadema, lakini TAL kama Mwenyekiti wa Chadema, ana strengths zake, (umahiri), ila pia ana madhaifu yake ambayo anahitaji msaada mkubwa kusaidiwa na watu wenye uwezo wa kusaidia, ili Tundu Lissu, Chadema na wapinzani wengine, waweze kubadilika na kuachana na siasa za kiunaharakati na badala yake kufanya siasa za kimikakati ya kujiandaa kutawala.

Hivyo vibwagizo vya kiuanaharakati, kama “no reforms no election” vibwagiza hadaa (utopian politics) visivyotekelezeka!. Chadema na wapinzani wote, lazima wajikite kwenye kufanya siasa za ukweli, (real politics) ambazo ni siasa za mikakati, (politics of engagement), vinginevyo uchaguzi wa 2025, mambo ya 2020 yanakwenda kujirudia, na itakuwa ni CCM tena!.

Hivyo natoa wito, kwa Watanzania wowote wazalendo wa kweli wa nchi hii, na wenye mapenzi mema na nchi yetu, wenye uwezo, wa kuwasaidia wapinzani, na kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL ili aweze, na kuisaidia Chadema ili iweze na pia kuwasaidia wapinzani wengine wote kufanya siasa za ukweli za kutaka kushika dola.

Kwenye kipindi hicho, TAL alipoulizwa maandalizi ya uchaguzi, amesema Chadema haifanyi maandalizi yoyote bila reforms ni no election!. Hizi ni utopian politics, sii TAL wala Chadema wana uwezo wa kuzuia uchaguzi Mkuu usifanyike!.

Natoa wito, kwa watu wowote, wenye uwezo, kutoka popote hata wana CCM, tujitokeze tujitolee kumsaidia TAL na kuisaidia Chadema, kwa kuishauri kuwa uchaguzi mkuu wa 2025, Chadema ina fursa!, hii ni fursa adhimu na fursa adimu kwa Chadema kuichangamkia, muda uliobaki kabla ya uchaguzi, sio rafiki kufanya siasa za kiharakati, huu ni muda wa kufanya siasa za kimikakati ya ushindi, tena namshauri TAL na Chadama wakumbatie falsafa ya pragmatism politics, wawe pragmatic and do what is possible!.

TAL na Chadema na wapinzani wengine wote, wasaidiwe waachane na utopian politics, wafanye real politics, the time is almost too little too short!, hakuna muda wa kupoteza!.

Paskali.

Nyuma ya serikali ya nchi nyingi za kiafrika kuna kundi dogo la wahuni ,mafisadi na wauaji .Hawa hawahitaji mtu yeyote wala serikali wala chama makini kishike dola.

CCM ya Magufuli kwa nini iwe tofauti na CCM hii isiyo na watu wala mtu hata mmoja lakini.

Unaitaja vipi CCM iliyowaweka pembeni watu kama Prof. Kabudi.
Unaitaja CCM gani iliyowaweka pembeni akina Lukuvi na kumchukua Mlarushwa na mtoa rushwa aliyewahi kupigwa marufuku kugombea kutokana na Rushwa .

Unaitaja CCM gani inayowaweka pembeni akina Paulo Makonda kutoka uenezi uliokua unawavutia vijana wa nchi hii kuiunga mkono CCM ?
Ni CCM gani inayojitenga na akina Polepole ,Januari makamba mtoto wa Kada wa CCM na aliyeshika nafasi ya juu kwenye kinyang'anyiro cha urais ndani ya CCM.?
Ni CCM ipi nje ya Nape Nnauye ?

Ni CCM ipi ipi hii ya Mwenyekiti asiyejua hata katiba ya chama chake mpaka aulize wazee ? Mtu asiyejua kakatiba ka chama anaweza vipi kujua katiba ya nchi,katiba ya Afrika Mashariki ,Katiba ya AU ,katiba na maagano na matamko ya UN, Maagano ya Kimataifa ya Haki za binadamu , Kanuni na sheria za kimataifa juu ya haki za kisiasa n.k. ?

Kama tuna tawaliwa na kiongozi amekua na uwezo wa kuzipambanua kanuni za uchaguzi ndani ya chama chake kama mwenyekiti wa chama basi tunatawaliwa na Dikteta kamili.
Bora Dikteta maana anajua kanuni na miiko ya kijeshi linapokuja suala la kupambana na raia wasio na silaha . Huyu anayefurahia watu kutekwa hadharani na kusema eti watu wasio na silaha wameota mikia . !!

Utaingiaje kwenye uchaguzi utegemee kushindana na mtu aliyefanikiwa kutumia idara zake kuwanyamazisha washindani wake ndani ya CCM. Samia hana tofauti na Kagame linapokuja suala la Madaraka tofauti na Kagame ni uzalendo . Kagame anapigania maslahi ya Rwanda kufa na kupona lakini mambo mengine yote hana tofauti na Kagame kisiasa .

Hivi Pascal kwa nini wasomi wa Tanzania mnakua machawa msiofanya hata utafiti mkaona jinsi hata zoezi la uandikishaji wa wapiga kura lilivyofanyika ?
Zoezi la kuandikisha wapigakura zaidi ya mil 40 unalifanyaje ndani ya siku tano. ?
Zoezi la kuandikisha na kuhakiki wapigakura limetulia mabilioni ya pesa kwa ajili ya kupata wapigakura wa CCM wasiozidi mil. 5 tu tena wengi ni wale wazee wenye makazi ya kudumu wa vijijini na marehemu ambao kwa miaka zaidi ya 20 hakujafanyika uhakiki wa kujua nani yupo hai na nani ni marehemu.
Mabilioni ya pesa yanatumika kufanya Hadaa ya uchaguzi halafu tunawatwisha lawama wapinzani .
Huu uhujumu uchumi wa kupoteza fedha za umma kwa uchaguzi feki unamnufaisha nani ?

Mpaka leo karibu mwaka wa Kumi na nne kitambulisho cha NIDA kinakua kizungumkuti kukipata lakini eti wiki moja inatosha kuandikisha wapiga kura zaidi ya mil.40 . Huu ni utapeli wa kisiasa .
Haya ndiyo mambo ya muhimu kwa wasomi wetu mahiri wa kukariri na Machawa walitakiwa wahoji kabla ya kurukia uchaguzi maana hakuna uchaguzi kama mtu hajajiandikisha . Kuigawa mitungi ya gesi na pikipiki na baiskeli na pesa ni lazima utegemee kura za watu waliojiandikisha . Je ni akina nani wanapewa hizo rushwa ?
Je, ni watanzania wote au kuna mahesabu yamefanywa kujua wale watakaowachagua .?

Je ,mitungi ya gesi inatosha ni kwa wote wasio nazo au ni baadhi kwa ajili ya kura ?
Bila shaka uandikishaji wa wapiga kura kwa wiki moja ulikua unalenga watu wahache tu na kubakisha marehemu na wanafunzi wa shule amba wakati wa kupiga kura watapewa likizo .

Chama chochote chenye watu wenye akili timamu hakiwezi kupoteza muda wake kuingia kwenye uchaguzi wa kipumbavu kama unaofanyika Tanganyika kwa sasa.
Tundu Lisu ni Binadamu mwenye akili kubwa sana na maono ya mbali sana iliyojaliwa na Mungu aliyeumba asili ya kila kitu na ndiye muamuzi wa Kila kitu duniani na hata ahera .
CCM ni chama kilichowekwa na watu waovu kwa hiyo huwezi ukashindana na mtu muovu labda uwe muovu kuliko yeye.

Masihi Yeshua Aliwahi kusema msishindane na mtu muovu . Mtu akikupiga shavu moja mgeuzie na la pili . Na akikunyanganya koti lako mwachie na Kanzu yako. Akikulazimisha umsindokize kilometa tano basi msindikize kumi . Akasema hapo ndipo mtakapokuwa wana wa baba yenu aliye mbinguni . Yaani akimaanisha kuwa hapo ndipo mtakapoona nguvu za Mungu (aliyemuita baba ). Kwa falsafa ya Yesu CCM inalazimisha uchaguzi ili ionekane inakubalika na kushinda kwa kishindo basi ni bora kuwaachia washinde kwa asilimia 100.

CCM ikishinda kwa asilimia mia moja bila upinzani itakua ni ushindi mkubwa kwa Upinzani makini kwa sababu 2030 Samia atakua amechokwa na kuchukiwa na kila Mtanganyika Mzalendo ndani na nje ya CCM jambo litakaloamsha roho ya uzalendo ndani na nje ya CCM . Upinzani ndani ya CCM utaibuka kwa hasira kubwa ambayo haijawahi kutokea tangu kuundwa kwa TAA.
Hapo ndipo Upinzani hasa Chadema utakapoingia madarakani na CCM kufa kabisa.

Lakini kama Chadema kitashiriki uchaguzi kitakua kimejiua chenyewe kwa sababu hakitapata kura hata asilimia kumi maana uandikishaji wa wapiga kura umefanyika kisanii haijawahi kutokea na chama chochote hapa Tanganyika kitakachoshiriki uchaguzi kitapigwa kipigo cha mbwa koko.

ACT iweke mgombea Zanzibar maana Zanzibar kuna maridhiano ya kikatiba na angalau katiba bora na tume kidogo huru kwa maana ya upatikanaji wa wajumbe wake .
Kwa hiyo nguvu kubwa ya ACT waipeleke Zanzibar lakini sio Tanaganyika .

Kama wajumbe wa serikali za mitaa wa CCM na serikali yake ambao hawalipwi mishahara walitumia mbinu zote chafu za kupiga kura duniani ili washinde itakuaje kwenye udiwani,ubunge na Urais wenye maslahi makubwa ?
Yeshua Masihi aliwahi kusema kama wanautendea mti mbichi namna hii itakuaje kwa mti mkavu ?

Bila shaka kwa wabunge na madiwani wa CCM waliohongwa kiasi hicho uchaguzi kwao utakua ni kufa na kupona . Hakuna ztakayekubali kushinda iwe kwa kuua ,kuteka ,kununua wagombea au vinginevyo ?

Uchaguzi wa Serikali za mitaa tulishauri sana Wapinzani wasishiriki ili CCM wakose sababu ya kujisifia kubwa wamechaguliwa kwa kura za kishindo .Kilichotokea hakitasahaulika na wapenda haki na demokrasia duniani.

Hakuna namna ya kushiriki kwenye uchaguzi wa mateso namna hii . Kwa nini uchaguzi uwe vita wakati wanaogombea wote ni ndugu zetu ?
Kwa nini Polisi watuwe na mgombea mmoja kuumiza wagombea wengine na wapiga kura wao katika nchi isiyo na ubaguzi wa kidini ,kikabila wala rangi ?
Kwa nini polisi waaminishwe kuwa kuna Wanzania wasiotakiwa kuchaguliwa na watanzania wanzao ili kuongiza dola ?

Kwa nini uchaguzi ukiisha ubakize vilio badala vya kupoteza watu ,kuua watu ,kuteka watu ,kufunga wetu,kufilisi watu ,kufukuza watu kwenye maeneo yao na kazi zao kwa sababu tu ya watu wasiozidi hata mia tano wanaotaka madaraka ya ubunge na urais ili wakashibishe familia zao na marafiki zao.

Kushindwa kwenye uchaguzi ni jambo la kawaidi kwani hata Mbowe ameshindwa pamoja na Henje.
Mpaka sasa mbowe na kundi lake wanahuzuni ya kupoteza nafsi zao kwenye sanduku la kura .
Hiyo ndiyo demokrasia .Hawahuzuniki kwa kupoteza watu wao kwa kutekwa ,kuuawa ,kufungwa ,kupigwa ,kubambikiwa kesi ,kupigwa mabomu kufilisiwa, kufukuzwa kazi kwa sababu ya uchaguzi bali wanahuzunika kidogo tu kwa sababu ya kushindwa uchaguzi ndio maana hata Aliyeshinda anaonekana kuwa na furaha maana hajashinda kwa damu za watu bali ni mbinu tu za kisiasa katika nchi zote zenye demokrasia ya kweli .
Lakini jambo la hovyo na baya sana ni watu kuuawa na kuteswa na kuumizwa kwa sababu ya uchaguzi .

Hivi nani anayeweza kuingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi na Mtu muovu kama Dr.Kasheku Musukuma ?.
Mtu ambaye anajua wazi kuwa akikosa ubunge hawezi kuteuliwa kuwa DC wala Mkurugenzi wala balozi kulingana na elimu yake ya ngumbaru .
Mtu yule ana pesa nyingi za kuhonga na kununua wagombea ,pili anauwezo wa kutuma majambazi yasiyojulikana yakamtoa mtu roho mchana kweupe na asifanywe chochote kwa maana ya chochote .
Sasa nani anaweza kurski maisha yake eti kuna fursa kwa wapinzani .Fursa, Damn shit!!!

Wakurugenzi wote wanafanya ufisadi wa kutisha wa fedha za halmashauri hilo halina ubishi.
Ni mkurugenzi yupi anataka kuwa na madiwani wa vyama vya upinzani watakaotoa siri za ufisadi ndani ya Halmashauri ?

TAL ana maono toka kwa Mungu sina shaka na hilo kabisa . Kwa Mwanzo huu Watamshinda kwa hila lakini hawatashinda kusudi la Mungu kuwapa watanzania viongozi wenye kusimamia haki na usawa katika rasilimali za umma . Mabadiliko ya kweli ya kijamii ,kisiasa ,kidemokrasia ,kiuchumi na maendeleo ya kweli na sheria za haki yote yataletwa na TAL kwa sababu Mungu anafanya kazi na watu Jasiri wasio na woga .

Wapinzani kugombea ni kuwapa majukwaa wahuni kwenye kampeni .

Hakuna upinzani hata wasanii wa muziki wanaotumiwa na CCM kuhamashisha maadili mabovu watakua hawana maana kwenye majukwaa. Akina Msingwa watakua hawana cha kuongea wala kupinga hoja maana watabaki kubwabwaja wenyewe majukwaani na mwisho wataona wamepita bila kupingwa na rushwa hazitatoka . Wajumbe watakosa kazi za kununua kadi na pesa za kugawa .
Uchaguzi utadoda na CCM itashinyaa na kuzubaa mapema na kuishi kwenye mzubao huo Kuelekea 2030 wenye chama halisi watakapodai chama chao na kuanda kuvurugana . Samia atakua amestaafu na CCM yao na Kikwete ataeeeka na CCM yake itakua imezeeka na kuchoka vibaya sana .

No Reforms No Election ni kauli ya Haki .
Haki huinua Taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote (pamoja na Paskali Mayalla )
 
View attachment 3246603

Apple ndio kampuni iliyozindua first ever modern tablet mwaka 1993 ikiitwa ‘Apple Newton’ ilikuwa touch screen computer na inaweza text.

IBM wakaenda mbele zaidi wakaja na first ever touch screen mobile phone 1994 ikiitwa ‘IBM Simons’.

Hizo bidhaa zote mbili zilifeli vibaya sana sokoni miaka ya 90 kwa sababu technology ilikuwa mbele ya muda. Apple ilifisika kabisa kwa sababu walitumia hela nyingi kwenye research ya hiyo PDA, ikabidi ‘Bill Gates’ awape mkopo kwa sababu aliamini uwepo wa kama washindani utachochea technology innovation.

Hizo bidhaa za Apple na IBM zilizo fail miaka ya 90, leo technology hiyo hiyo tunaita smart technology na ndio dominant sokoni.

Somo ni nini elewa wananchi wanataka nini na wako wapi (marketing research) kwanza kabla ya kutengeneza bidhaa. Changes za kitu kigeni zinataka baby steps, kufikia ukileta kitu kipya kabisa kinaenda fail hata kama ni bora.

Lissu anafikiria vitu kutoka kichwani kwake bila ya kuelewa raia wapo hatua gani ya uelewa. Watanzania wengi hawajui kama wao ndio wenye nchi na wafanyakazi wa serikali ni waajiriwa wao. Sasa utamshawishi mtu vipi kudai mabadiliko hata elimu ya haki yake haijui. Mbaya zaidi haki zake zipo kwenye katiba ambayo kila siku mnaiita mbovu as if kila kitu kibaya.

Story ni ndefu ila Lissu sio mwanasiasa na upinzani bara bado; Zanzibar tayari.

Lissu ni ‘demagogue’ wanna be lakini hana rhetoric ya kuongea na watanzania kwa kuwaelewa kwanza, hana political strategy ya muda mrefu. Yeye anadhani kilichopo kichwani kwake either unakubaliana nae au, basi na watanzania wote wenye shida wanatakiwa kuwa na mtazamo huo-huo. Hizo siasa anazohubiri muda wake Tanzania bado, yupo lala land.

Wewe unasema ‘No reforms, no election’, huko ndani ya CCM kauli hiyo wanaitafsiri kama ‘kuvuja kwa pakacha, nafuu kwa mchuuzi’.

CDM ni useless
We usiwadharau wananchi kiivyo,!!!,mtu hata kama hana elimu usemayo,lkn kwa akili nyepesi tu,wengi walijionea uchaguzi ulopita,hivi nani asojua kilichofanyika??,,the same 2020, kweli wasijue kusoma,lkn washindwe kujua kilichofanyika?
 
Back
Top Bottom