Wapinzani wangeliungana na Hayati Magufuli hakika tungelikuwa tushapata Tanzania Mpya, tatizo ni maslahi binafsi

Wapinzani wangeliungana na Hayati Magufuli hakika tungelikuwa tushapata Tanzania Mpya, tatizo ni maslahi binafsi

Mkuu kumpenda Magufuli haina tatizo kabisa - kwa waliompenda, kumuelewa na kuwa wafuasi na mashabiki wake. Ni haki yao.

LAKINI kutarajia kuwa wapinzani nao walitakiwa kumuunga mkono na hivyo KUACHA KABISA KUIKOSOA SERIKALI ni kudharau sana intelligence na integrity ya wapinzani.

Na sio tu wapinzani walioko kwenye vyama vya upinzani (opposition) bali pamoja na wote wasio wanachama wa vyama, wanaharakati, na hata walio ndani ya chama tawala. Natumaini utanielewa.

That is my point.

Hakuna sehemu nimeongelea “mapenzi Kwa Magufuli, hata nukta.

Nimeongelea wao kumkataa kumuunga mkono katika mambo yale yale waliyokua wakiyapigia kelele wao wenyewe (upinzani)+ wananchi wengi…

Eti integrity ya wapinzani? Kwenye nini labda maana hata credibility tu ni ndoto kuipata Kwa wanasiasa wa Tanzania, both CCM na Upinzani.
 
Mambo gani hayo?

Halafu, ni Magufuli ndiye mwanasiasa pekee aliyekuwa na integrity na credibility nchini? Ndio mahaba yenyewe hayo uliyo nayo kwa mwendazake! Au utadai pia kuwa Magufuli hakuwa mwanasiasa.
 
Binafsi naamini Tanzania Mpya itatengenezwa kwa kuudhoofisha mfumo imara wa CCM na kupata katiba Mpya.

Hayati Magufuli alijaribu mpaka wana CCM wengi wakamchukia, wapinzani hawakumuelewa na yeye akaamua kuwabadilikia .

Laiti kama Upinzani ungezungumza lugha Moja na Magufuli ndani ya kipindi kifupi tungepata Tanzania Mpya, Tatizo vyama vyetu kuna viongozi maslahi.

Hayati Magufuli alihitaji sana uungwaji mkono na wapinzani na ndio maana hata watu aliyowachukua Upinzani walikuwa ni imara na watendaji wazuri .

Huyo Magufuli kama asingekuwa na Maslahi Binafsi kwa nini aliiba Chaguzi ....!!?
 
Binafsi naamini Tanzania Mpya itatengenezwa kwa kuudhoofisha mfumo imara wa CCM na kupata katiba Mpya.

Hayati Magufuli alijaribu mpaka wana CCM wengi wakamchukia, wapinzani hawakumuelewa na yeye akaamua kuwabadilikia .

Laiti kama Upinzani ungezungumza lugha Moja na Magufuli ndani ya kipindi kifupi tungepata Tanzania Mpya, Tatizo vyama vyetu kuna viongozi maslahi.

Hayati Magufuli alihitaji sana uungwaji mkono na wapinzani na ndio maana hata watu aliyowachukua Upinzani walikuwa ni imara na watendaji wazuri .
Magufuli yupi angeleta Tanzania mpya wakati alikuwa anafilisi biashara za matajiri?

Mungu mwenyewe alijuwa kuwa akina Kikwette na CCM wamebugi big time kumpa kichaa uRais, ndipo akamtoa. Bado nyie machawa sijui tuwaite misukule mnamuota!!

Amekufa na hatorudi tena, jitahidi uzoee hali hii
 
Mradi wa umeme ulipingwa na wataalamu ww mazingira tena kwa riport rasmi ya kitaalamu, wakati huo January Makamba akiwa waziri. Mimi ni mmojawapo wa aliyepinga mradi wa umeme wa hilo bwawa, tena nikiwa na sababu za msingi. Kabla ya 2015 tuliimbishwa kama watoto wadogo kuhusu umeme wa gas na bomba limefika hapa Dar, kumbuka tulikopa 2T kwa ajili ya mradi wa umeme wa gas. Na matatizo ya wakati ule kuhusu umeme wa maji ilikuwa ni mabadiliko ya tabia nchi. Wakati tukilishwa haya, Magufuli alikuwa kimya huko kwenye chama chake akilinda cheo.

Hadithi za umeme wa gas ilikuwa ni kupata 5,000m mpaka yeye anaingia madarakani kulikuwa 500m tayari za umeme wa gas, huku umeme wa Magufuli ikiwa 2,115m kwa 7t. Sasa kwa akili ya kawaida kwanini, tungeweka 3T tusingeweza kupata hizo 2,115m za kwenye umeme wa maji, tukaacha mazingira salama, na hizo 4T nyingine tuwekeze kwenye kilimo ama viwanda? Sasa nikuulize ww unayedhani kila mtu aliibeba hoja ile kwa mtazamo wa kipropaganda.
  1. Je kuna mabadiliko ya tabia nchi ama hakuna?
  2. Ni kwanini tuliwekeza 7T kwenye umeme wa maji ambao tuliambiwa tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi, tukaacha kuwekeza hela chini ya 7T kupata umeme zaidi ya 2,115m?
Ukitoa ufafanuzi wa hayo mawili, nitahamia kwenye hayo mengine uliyorukia kichwakichwa bila kujiuliza.
maswali yako ni mazito na ya msingi sana mkuu, mimi siwezi kuyatolea ufafanuzi kwa usahii kabisa kama ipasavyo, other wise ningekuwa kwenye system ndo ningejua kwa undani zaidi kwamba ni nini kilipelekea magufuli kuepuka mradi wa umeme wa gas. Nadhan nyie ambao mko kwenye system mnaweza kutujuza.

Naomba nikuulize, mpaka sasa bado unaamin kuwa magufuli hakuwa sahihi kufanya mradi ule wa umeme?
 
Yuko sahihi kutupatia umeme, lakini pesa imekuwa nyingi sana kwenye mradi wa maji, nadhani nusu ya pesa hiyo ingeweza kutupatia Mega hizo za kwenye gas, na nyingine ingeingia kwenye shughuli nyingine.

Kwahiyo uelewe hatukupinga kila kitu bila hoja za msingi. Ila ww ulitekwa na maelezo ya kipropaganda kiasi kwamba ukapata upofu wa kuona hoja mbadala.
 
Binafsi naamini Tanzania Mpya itatengenezwa kwa kuudhoofisha mfumo imara wa CCM na kupata katiba Mpya.

Hayati Magufuli alijaribu mpaka wana CCM wengi wakamchukia, wapinzani hawakumuelewa na yeye akaamua kuwabadilikia .

Laiti kama Upinzani ungezungumza lugha Moja na Magufuli ndani ya kipindi kifupi tungepata Tanzania Mpya, Tatizo vyama vyetu kuna viongozi maslahi.

Hayati Magufuli alihitaji sana uungwaji mkono na wapinzani na ndio maana hata watu aliyowachukua Upinzani walikuwa ni imara na watendaji wazuri .
Magufuli alikuwa na upeo mfupi wa kuona mambo na alikuwa anapenda kusifiwa hata anapofanya makosa. Watu wa shule za kata mna shida sana. Jaribuni kujifunza lugha ya kiingereza ili mpanue upeo wenu wa kuona mambo na kuijua dunia.
 
Binafsi naamini Tanzania Mpya itatengenezwa kwa kuudhoofisha mfumo imara wa CCM na kupata katiba Mpya.

Hayati Magufuli alijaribu mpaka wana CCM wengi wakamchukia, wapinzani hawakumuelewa na yeye akaamua kuwabadilikia .

Laiti kama Upinzani ungezungumza lugha Moja na Magufuli ndani ya kipindi kifupi tungepata Tanzania Mpya, Tatizo vyama vyetu kuna viongozi maslahi.

Hayati Magufuli alihitaji sana uungwaji mkono na wapinzani na ndio maana hata watu aliyowachukua Upinzani walikuwa ni imara na watendaji wazuri .
Huwezi ungana na dikteta
 
Ulicho andika ni cha kweli ila wenye akili ndogo ni vigumu kuelewa ...waulize wapinzani ni kwanini JPM alikuwa anatamka sana haya maneno ....(ngojeni kwanza ni nyoshe nchi) kuna elimu kubwa sana na akili kubwa sana kwenye haya maneno kwa watu tulio jaliwa akili timamu ...muulizeni mbowe au tundu lissu au zitto hayo maneno yalikuwa na maana gani? Ndiyo utajua kuwa tanzania tunaongozwa na wapumbavu wengi sana..kamwe mbowe lisu na zito awawezi kuelewa hekima ya hayo maneno .....pia JPM alikuwa ni Rais mkweli tofauti na huyu muhuni ambaye wapinzani walimtukuza kwa kumwamini ...yaana unashindwa kumwamini Rais mkweli unakuja kumwamini Rais muhuni...vyama vya upinzani tanzania vimechanganyikiwa kabisa ni upumbavu ulio tukuka....kwa sasa wapinzani walituaminisha kuwa mtu wa kushirikiana naye ni Samia lakini kinacho wakuta wanajuta na wataendelea kujuta zaidi ...kipindi cha JPM ilikuwa ukishirikiana naye yupo piss sana anakuingiza kujenga nchi na kupambania taifa kikweli kweli .....WAPINZANI TANZANIA KUTOKANA NA AKILI ZAO MBOVU WAKA UNDERESTIMATE THE STUPIDITY OF THE STUPID PEOPLE .....SAMIA NI DEATH TRAP...SIYO DEATH KWA UPINZANI TU BALI NA KWA TAIFA PIA...niliwaambia wapinzani ilikuwa rahisi kupata katiba mpya na nzuri na ya haki chini ya mzalendo JPM kuliko huyu muhuni tuliye naye sasa walinipingakwenye huo ukweli vibaya sana na sababu za kunipinga ni ....(walishindwa kufumbua fumbo la magufuli la ngojeni kwanza ninyoshe nchi)

Acha kumlinganisha Lissu na vitu vya kijinga. Magufuli na Samiah wote ni mashetani. Hawana la maana.
 
Alisemaga hivyo baada ya kuona hawakuwa wakimuunga mkono kwa yale aliyokuwa akiyafanya japo yalikuwa ndio yale yale waliyokuwa wakiyahubiri wapinzani siku zote kabla ya JPM kushika madaraka !

Wapinzani walivyoona Jiwe anashangiliwa sana na Wananchi wakasema huyo Jiwe anafuata sera zetu !
Lakini wakaendelea kumpinga na kumponda badala ya kumuunga mkono !

Ndipo alipoona kumbe na hawa wapinzani ndio kama hao hao aliokuwa akipambana nao huko Serikalini na Chamani kwake !
Akaamua sasa ajitengenezee sapoti kutoka kwa Wananchi na kutoka kwa baadhi ya wale aliowainua kutoka Chamani kwake na upinzani !

Ukweli ni kwamba JPM alikuwa na nia ya kuibadilisha Nchi kabisa lakini alihitaji sana sapoti ya kutoka Upinzani ili aweze kuyatimiza yale aliyokuwa ameyakusudia !
Bahati mbaya Wapinzani walishindwa kumuelewa hata alipokuwa akiwashughulikia kweri kweri wa Chamani kwake lakini Wapinzani walishindwa kabisa kuusoma mchezo !
Wao wakaendelea na pinga pinga Jazz Band yao ndipo Ngosha akabadili ubao 😳🙄 !

Wamuunge mkono kwa lipi?. Tanzania ni nchi ya vyama vingi kwanini ulazimishe upinzani umuunge mkono?.

Halafu alitoa kauli hiyo mwanzoni baada ya kuchaguliwa. Alikuwa na hasira ya kupata Asilimia 57 ya kura zote.
 
Binafsi naamini Tanzania Mpya itatengenezwa kwa kuudhoofisha mfumo imara wa CCM na kupata katiba Mpya.

Hayati Magufuli alijaribu mpaka wana CCM wengi wakamchukia, wapinzani hawakumuelewa na yeye akaamua kuwabadilikia .

Laiti kama Upinzani ungezungumza lugha Moja na Magufuli ndani ya kipindi kifupi tungepata Tanzania Mpya, Tatizo vyama vyetu kuna viongozi maslahi.

Hayati Magufuli alihitaji sana uungwaji mkono na wapinzani na ndio maana hata watu aliyowachukua Upinzani walikuwa ni imara na watendaji wazuri .
Nadhani hoja ingekuwa hivi:
Magufuli asingewapiga vita wapinzani na kuwatumia kupata taarifa mbalimbali angeweza kuvunja kabisa mtandao wabkifisadi. Sasa yeye kadanganywa kuwa wapinzani ndio watamchelewesha.
 
Back
Top Bottom