Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Waraka: Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) latoa tahadhari kuhusu ugonjwa wa Corona nchini

Afadhali sasa sauti zinaanza kupazwa toka kila kona, tuache kuishi kwa kudanganyana kama watoto, kila mmoja popote alipo achukue tahadhari kwa kujilinda yeye na awapendao, Corona ipo na inaua.

Inawezekana kifo cha Padre huko Kagera ndio kimewasukuma TEC kutoa hili tamko, wameona ukimya ungezidi kutuangamiza.
Na Dar es salaam nako padri karudisha file
 
Ngoja nikufungue macho kidogo, siku zote ukiona kanisa katoliki linatoa kauli ujue hiyo imepita, kwasababu wao ndiyo wanao control mambo mengi hao ni zaidi ya kanisa. Hakuna kiongozi wa kiserekali anaweza kushindana nao.
Wanasema Roma Locuta causa finite
 
Wao ni Idara ya afya? Wanasemaje pia kuhusu Malaria?
Kuna taasisi ya kidini yenye hospitali nyingi tanzania kama roman catholic?..... huo ndio usemi wao kuhusu malaria na waraka wao unalenga taifa la Mungu yaani waumini wao inawezekana wewe huko exempted
 
Hivi mpaka padri au sista afe ndio tamko litoke,tunatakiwa kuwa makini na kuthamin utu wa watu wote,hata barua yao hao walioiandika haitaji waamini pale juu ila inawataja wao wenyewe barua iko kibaguzi ni kama waamini sio watu.Au nasema uongo ndugu zangu.
 
Hizi dini za kuletewa bhana. Mbona hili kanisa halisaidii watu wenye kukosa kazi, chakula. Tuendelee na utamaduni wetu wa asili. Tule mimea yetu. Dawa za asili tuuu. Wao wale chanjo zao. Yule anayetuletea ajipige yeye. Tanzania hamna korona.
 
Nashukuru mleta hoja umesema kumbe tangu korona iingie Tz sasa ni mwaka unaisha. Pia umesema kuwa wenzetu walichukua tahadhari mapema (mwaka sasa) lakini sisi hatukuchukua tahadhari zao za kujifungia (Lockdown).
Swali ni Je, kama hatukujifungia sasa huu ni mwaka, kuna mtu amebaki tena Tz kweli? Waliojifungia mbona wamekufa ka panzi huku kwetu hao wafu wanaliwa au?? Mbona hatujaona haswa mimi sijawahi ona jirani yangu hata mmoja tu. Ila nimezika wengi wa ajali za baharini na ziwani, ajali za kuungua moto Moro, ajali za kufunikwa udongo machimboni etc. Hao wa korona mnawala?
Acheni kututisha, hameni Tz muende huko wanakovaa barakoa tuone kama hamtakufa. B/up sana mh Rais wetu kwa kututoa hofu. Kihoro cha hofu kingetumaliza. Mnaotaka Lockdown mna zenyu agenda na hapa kwetu hampati nafasi ng'o!!!!!
 
Waraka unasema kuwa mwaka jana tulifanikiwa katika mapambano dhidi ya corona,sasa kama ni hivyo sijajua ni kwanini watu wamekuwa na wasiwasi na kulaumu serikali katika hili wimbi la pili ikiwa wimbi la kwanza serikali ilishinda mapambano?
 
Nashukuru mleta hoja umesema kumbe tangu korona iingie Tz sasa ni mwaka unaisha. Pia umesema kuwa wenzetu walichukua tahadhari mapema (mwaka sasa) lakini sisi hatukuchukua tahadhari zao za kujifungia (Lockdown).
Swali ni Je, kama hatukujifungia sasa huu ni mwaka, kuna mtu amebaki tena Tz kweli? Waliojifungia mbona wamekufa ka panzi huku kwetu hao wafu wanaliwa au?? Mbona hatujaona haswa mimi sijawahi ona jirani yangu hata mmoja tu. Ila nimezika wengi wa ajali za baharini na ziwani, ajali za kuungua moto Moro, ajali za kufunikwa udongo machimboni etc. Hao wa korona mnawala?
Acheni kututisha, hameni Tz muende huko wanakovaa barakoa tuone kama hamtakufa. B/up sana mh Rais wetu kwa kututoa hofu. Kihoro cha hofu kingetumaliza. Mnaotaka Lockdown mna zenyu agenda na hapa kwetu hampati nafasi ng'o!!!!!
Kaka ukilinganisha nchi tafadhali uelewe tofauti iliyopo:
TZ tumeweza kuishi bila tahadhari kubwa kwa sababu idadi ya wazee ni ndogo. Wazee juu ya miaka 65 ni asilimia 2.6 hivi, jumla kidogo juu ya milioni moja. Nchi kama Italia ina idadi hiyohiyo ya watu kama TZ, lakini wazee ni zaidi ya milioni 13. Kimataifa ni hao wanaoendelea kuonyesha dalili kali na kufa. Hata Ulaya au Marekani vijana au watu wenye umri wa wastani hawafariki dunia "kama panzi". Kote Duniani karibu vijana wote wenye COVID wanakohoa kidogo na kupona, wanaokufa ni wachache.

Kilicholinda Tanzania si miujiza au kufukiza, ni umri wa wananchi, pamoja na hali ya maisha katika nyumba bila madirisha yanayozuia hewa, hivyo hatari ya aerosol (matone madogo katika pumzi yanayosambaza virusi) kuongezeka ndani ya chumba si kali kama ktk nchi za kaskazini.

Ila Covid ipo, ingesaidia kama viongozi wasingerudia "hakuna Corona", maana watu wengi mno wanaiamini na kuacha kila tahadhari. Hali inayosababisha vifo visivyo vya lazima.
Hakuna haja ya lockdown,lakini sharti kujitahadhari .
 
Nawa mikono, epuka mikusanyiko, vaa mask kila wakati uwapo matembezini, tumia sanitizer baada ya kushikana na mtu, fanya mazoezi, kula vizuri hasa matunda, mboga mboga, kunywa maji ya kutosha, usisahau kuwa pamoja na familia yako pia baada ya kazi mental health inaanzia nyumbani kwako.
 
.
masoudkipanya-20210125-0001.jpeg
 
Back
Top Bottom