WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Siku hizi wanasema sio dunia tu bali hata galaxies na kwa kifupi ulimwengu (universe) wote ambao hata mwisho wake na wapi ni katikati haijajulikana.
Hahahaha...

Sasa nimeanza kuelewa kwanini ile sala ya Mwanakondoo..tumedili kutoka "aondoae dhambi za dunia kuwa dhambi za ulimwengu"
 
Huko kote umenena vyema kabisa, ndiyo maana nimeondoa. Lakini katika hili la mwisho, naomba kuuliza kama unamfahamu Pengo.

Namfahamu sana. Rafiki yangu niliye kua naye shule alikua Askofu msaidizi wake. Na ninajua nini swali baada ya hili. Pengo siyo mropokaji kama wengine. Pengo ana wakati wake anauona muafaka anakuja na lungu lake. Sijui umri wako huko nyuma Pengo aliwasema CCM waziwazi.

Unakumbuka alipowaambia CCM na serikali yake kuwa "Hittler alichaguliwa na wananchi wa ujerumani ki demokrasia na wala hakupindua nchi. Watu walichoka na muelekeo wa serikali ya wakati huo ya Ujerumani ikaamua kumuweka Hitller madarakani.

Ningeoba sana ninyi watawala muangalie upya jinsi mnavyoendesha serikali isiye ya udhalimu tukaja tukamuweka Hitller wetu hapa Tanzania. Maana watu wakiwachoka na mambo yenu watampigia kura yeyote yule ili mradi wabadilishe uongozi.

Hivyo msitukwaze" huyo alikua Pengo. Miaka ya 90 wakati serikali ilikua inapiga virungu mpaka wanafunzi migomo mingi ya madaktari n.k. Hivyo wengi humu ndani JF wamezaliwa juzi juzi hawamjui kabisa Pengo. Pengo alikua mwiba kwa CCM wakati huo hakuna vyama vingi.
 
Kwanza akatubu ndipo mambo mengine yafuatie!

Sijui Kwanini Yule askofu mkubwa wa kanisa anashindwa kumshauri Swahiba wake atubu!
.msimamo wa TEC sometimes huwa unatofautiana na msimamo wa kanisa!
"Msimamo wa TEC sometimes unatofautuana na msimamo wa kanisa"!!!! Huku ndiko kulewa kwa mvinyo mpya au mbege grade one?. Hivi unajua kanisa ni nini na TEC ni nini?. Kanisa linaanzia level ya dunia (pope) kisha level ya majimbo ( jimbo moja moja) kuna msemo wa kanisa unasema hivi penye askofu kanisa limekamilika. Askofu ni mchungaji Mkuu wa kanisa level ya jimbo. Sasa wanapokutana maaskofu wote Tanzania maana yake kanisa katoliki Tanzania limekutana na kujadiliana na kuafikiana kisha maafikiano hayo huandikwa ili jumuia ya waamini wasome na kuelewa kinachosemwa na kanisa. Kwahiyo kusema Msimamo wa TEC sometimes unakwenda kinyume na kanisa ni kwamba hujui TEC ni nini na kanisa ni nini.
 
Masemaji wa kanisa ni Papa.
Na papa Ana balozi wake hapa......
Huo waraka siyo kauli ya kanisa.....ni mawazo tu ya maaskofu kama watz wengine......
 
Unajua mkuu kuna watu wanajifanya wanalijua kanisa katoliki kwa kusoma vitabu vya kusadikika vya kina Yericko. Wao hawajui kabisa miongozo ya kanisa lakini ukiona wakiandika apa utadani wanalijua kwelikweli ila kwa wsiojua wanaamini hizi habari za kusadikika wanazoandikiwa na kina Yericko ambao wanatoa vijarida kujaza matumbo yao. Hata kirefu ca TEC (Tanzania Episcopal Conference) labda hawakijui.
 
Masemaji wa kanisa ni Papa.
Na papa Ana balozi wake hapa......
Huo waraka siyo kauli ya kanisa.....ni mawazo tu ya maaskofu kama watz wengine......
Yaani mkuu maaskofu wa Katoliki ni kama watanzania wengine? Naona unawashusha.
 

Imebidi nikakinunue kitabu kabla hakijaisha.
 
Reactions: BAK
Mindi Ngoja tuone Bakwata kama watatia neno!huo waraka ungetolewa na Sheikh Ponda pangekua pameshawaka moto saa hii
 
Namshangaa saana Mh Rais anavyozidi kuwachekea hawa maaskofu
Badala ya kuendelea na kazi zao za kidini wanaingilia ingilia siasa
Hawa maaskofu wanatakiwa waadhibiwe adhabu kali hasa,ili wawe mfano kwa maaskofu wengine[emoji1321]
 
Namshangaa saana Mh Rais anavyozidi kuwachekea hawa maaskofu
Badala ya kuendelea na kazi zao za kidini wanaingilia ingilia siasa
Hawa maaskofu wanatakiwa waadhibiwe adhabu kali hasa,ili wawe mfano kwa maaskofu wengine[emoji1321]


Nenda kamwambie akatubu huko acha kuropoka hapa
 
mume sema kweli tupu ila wakuyafanyia Kazi maneno haya ndohayupo nadhani mungemshauri turudi kwenye mfumo wa chama kimoja
 
Masemaji wa kanisa ni Papa.
Na papa Ana balozi wake hapa......
Huo waraka siyo kauli ya kanisa.....ni mawazo tu ya maaskofu kama watz wengine......


Duh mkuu na wewe ni Mkatoliki? kama wewe ni mkatoliki basi hujapata hata mafundisho ya awali ya komunio ya kwanza. Yaani wewe unajua msemaji wa kanisa ni pope?. Lini pope kawa msemaji wa kanisa? Pope ni kiongozi wa kanisa na mara nyingi maamuzi hutolewa na vyombo vya maamuzi vya kanisa level ya dunia. Halafu nani alikwambia balozi wa pope ni msemaji wa kanisa? Hebu kabla hujachangia uwe unajifunza kwanza. Balozi wa pope hajawahi wala hatakaa awe msemaji wa kanisa. Eti huo waraka siyo kauli ya kanisa bali ni mawazo ya maaskofu wa tanzania , sasa mkuu KANISA ni nini?. Naomba nikufunze kidogo, kanisa huanzia level ya dunia (kiongozi wake ni pope) halafu inaenda moja kwa moja kwenye level ya jimbo (kiongozi wake ni askofu wa jimbo) penye askofu kanisa linakamilika kabisa. Lakini maaskofu wanapokutana wote hapo KANISA limekamilika kabisa. kwahiyo ndg huo waraka ni ni kauli halisi na halali ya kanisa na haliwezi kupingwa hata na pope wala balozi wake, kingine mawazo ya maaskofu tanzania ndiyo mawazo ya kanisa. Kama hujui uwe unauliza upewe mwanga.
 
Dalili za kupungua kwa sadaka ziko wazi!wapambane na hali yao![emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Wataanza kutozwa kodi shauri zao,au kuchunguzwa uraia wako.wangekuwa na ubavu huo si wangewatenga na kuwafukuza ushiriki wale wote wasababishi wa waliyoyaandika kwenye waraka wao.

Duh aisee muwe mnjifunza utaratibu wa kanisa kwa undani kabla ya kuzungumza!, kanisa linaweza kumfungia mtu ushiriki wake kwenye kanisa ila hiyo hatua ili ichukuliwe ni lazima labda uwe umeasi au umefanya kosa kubwa sana dhidi ya imani ya kanisa. Na sababu ni kwamba hata Yesu na mitume wake hawakuwahi kuwafungia watu kwenye mambo ya imani huko ni kuhukumu.
 
Mwaka gani alitamka haya?
 
Kumfahamu mtu haihitaji uwe umri sawa naye, haihitaji umzidi au uwe mdogo kwake, haihitaji muwe mmesoma nsye au uwe umemfundisha. Rekodi zinaongea. Aonekanavyo ndivyo alivyo. Ni kama Prof Kabudi wa Tume ya Warioba na Prof Kabudi waziri, ni watu tofauti wenye misimamo na kauli tofauti.
Unaweza uka highlight kwa majina ni watawala gani wa hapa nchini ambao Pengo aliwakemea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…