WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

WARAKA: Maaskofu Katoliki waonya uminywaji wa demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari nchini

Siku hizi wanasema sio dunia tu bali hata galaxies na kwa kifupi ulimwengu (universe) wote ambao hata mwisho wake na wapi ni katikati haijajulikana.
Hahahaha...

Sasa nimeanza kuelewa kwanini ile sala ya Mwanakondoo..tumedili kutoka "aondoae dhambi za dunia kuwa dhambi za ulimwengu"
 
Huko kote umenena vyema kabisa, ndiyo maana nimeondoa. Lakini katika hili la mwisho, naomba kuuliza kama unamfahamu Pengo.

Namfahamu sana. Rafiki yangu niliye kua naye shule alikua Askofu msaidizi wake. Na ninajua nini swali baada ya hili. Pengo siyo mropokaji kama wengine. Pengo ana wakati wake anauona muafaka anakuja na lungu lake. Sijui umri wako huko nyuma Pengo aliwasema CCM waziwazi.

Unakumbuka alipowaambia CCM na serikali yake kuwa "Hittler alichaguliwa na wananchi wa ujerumani ki demokrasia na wala hakupindua nchi. Watu walichoka na muelekeo wa serikali ya wakati huo ya Ujerumani ikaamua kumuweka Hitller madarakani.

Ningeoba sana ninyi watawala muangalie upya jinsi mnavyoendesha serikali isiye ya udhalimu tukaja tukamuweka Hitller wetu hapa Tanzania. Maana watu wakiwachoka na mambo yenu watampigia kura yeyote yule ili mradi wabadilishe uongozi.

Hivyo msitukwaze" huyo alikua Pengo. Miaka ya 90 wakati serikali ilikua inapiga virungu mpaka wanafunzi migomo mingi ya madaktari n.k. Hivyo wengi humu ndani JF wamezaliwa juzi juzi hawamjui kabisa Pengo. Pengo alikua mwiba kwa CCM wakati huo hakuna vyama vingi.
 
Kwanza akatubu ndipo mambo mengine yafuatie!

Sijui Kwanini Yule askofu mkubwa wa kanisa anashindwa kumshauri Swahiba wake atubu!
.msimamo wa TEC sometimes huwa unatofautiana na msimamo wa kanisa!
"Msimamo wa TEC sometimes unatofautuana na msimamo wa kanisa"!!!! Huku ndiko kulewa kwa mvinyo mpya au mbege grade one?. Hivi unajua kanisa ni nini na TEC ni nini?. Kanisa linaanzia level ya dunia (pope) kisha level ya majimbo ( jimbo moja moja) kuna msemo wa kanisa unasema hivi penye askofu kanisa limekamilika. Askofu ni mchungaji Mkuu wa kanisa level ya jimbo. Sasa wanapokutana maaskofu wote Tanzania maana yake kanisa katoliki Tanzania limekutana na kujadiliana na kuafikiana kisha maafikiano hayo huandikwa ili jumuia ya waamini wasome na kuelewa kinachosemwa na kanisa. Kwahiyo kusema Msimamo wa TEC sometimes unakwenda kinyume na kanisa ni kwamba hujui TEC ni nini na kanisa ni nini.
 
Masemaji wa kanisa ni Papa.
Na papa Ana balozi wake hapa......
Huo waraka siyo kauli ya kanisa.....ni mawazo tu ya maaskofu kama watz wengine......
 
Unajua mkuu kuna watu wanajifanya wanalijua kanisa katoliki kwa kusoma vitabu vya kusadikika vya kina Yericko. Wao hawajui kabisa miongozo ya kanisa lakini ukiona wakiandika apa utadani wanalijua kwelikweli ila kwa wsiojua wanaamini hizi habari za kusadikika wanazoandikiwa na kina Yericko ambao wanatoa vijarida kujaza matumbo yao. Hata kirefu ca TEC (Tanzania Episcopal Conference) labda hawakijui.
 
Masemaji wa kanisa ni Papa.
Na papa Ana balozi wake hapa......
Huo waraka siyo kauli ya kanisa.....ni mawazo tu ya maaskofu kama watz wengine......
Yaani mkuu maaskofu wa Katoliki ni kama watanzania wengine? Naona unawashusha.
 
Inatia moyo sana kuona Baraza la Maaskofu nchini limeanza kulaani na kukemea huu UdU wa kutisha unaoendelea nchini katika awamu hii.

Waliokuwa wanaikosoa Serikali hii dhalimu walitusiwa majina mbali mbali ikiwemo wasaliti, majizi, wapiga madili na matusi mengine chungu nzima.

Sasa hata Baraza hili la Maaskofu limechoka kuendelea kukaa kimya huku UdU nchini ukizidi kushamiri kwa kasi ya kutisha na hivyo kutishia amani ya nchi yetu.

DU apingwe kwa nguvu zote za Watanzania wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu ili aheshimu katiba, Bunge, mahakama, sheria za nchi, sheria za manunuzi ya Serikali, sheria za kutoa fedha hazina etc.

Naendelea kusema huyu jamaa ni janga kubwa sana la Taifa letu na ni mtu hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu.

Nzi Elli Tetty Sky Eclat Salary Slip zitto junior MENGELENI KWETU tindo Saint Ivuga Erythrocyte lusungo Retired

Imebidi nikakinunue kitabu kabla hakijaisha.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mindi Ngoja tuone Bakwata kama watatia neno!huo waraka ungetolewa na Sheikh Ponda pangekua pameshawaka moto saa hii
 
Namshangaa saana Mh Rais anavyozidi kuwachekea hawa maaskofu
Badala ya kuendelea na kazi zao za kidini wanaingilia ingilia siasa
Hawa maaskofu wanatakiwa waadhibiwe adhabu kali hasa,ili wawe mfano kwa maaskofu wengine[emoji1321]
 
Nenda kamwambie akatubu huko acha kuropoka hapa
 
Page 12
"Kikatiba, nchi yetu inafuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katiba na Sheria mbalimbali zimeainisha utaratibu wa kazi na shughuli za vylma vya siasa. Ili kuhakikisha hvamba ka'"'ina shughuli z vyamavya siasa zinakuwa endelevu, vyama vyenye kukidhi vlgezo hupewa ruzuku kupitia Bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania. Hata hivyo, shughuli za, sirsa bado zinaendelea kuzuiwa kwa kutumia vyombo vya dola. Maana yake ni kwamba shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa, kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani, ambayo ni haki ya kila rua, zimekoma mpaka uchaguzi mwingine. Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na Sheria za nchi.

Vile vile baadhi ya vyombo vya habari vimefungiwa au kusimamishwa kwa muda, na hivyo kupunguza uwigo wa uhuru wa wananchi wa kupata habari, maoni na wa kujieleza. Kufungiwa huku kwa vyombo vya habari kumeenda sambaba na kuminya uhuru wa mahakama na bunge kwa njia ya kuminya haki wabunge na kutowapa nafasi ya mikutano ya hadhara kama haki yao ya msingi ya Kikatiba.

Katika mazingira haya ni rahisi kwa jamii kufarakana na hata kujenga chuki kiasi cha kuhatarisha amani, usalama na hadhi ya uhai wa binadamu. Kumekuwapo pia hali ya vurugu katika chaguzi mbalimbali. Chaguzi hizi zinaacha nyuma uchungu, hasira, tamaa ya kulipa kisasi na hata kususia chaguzi nyingine. Hali hii ni hatari kwa mustakabali wa Taifa letu. Tukiiachia hali hii izoeleke tushishangae huko mbeleni kujikuta katika mifarakano mikubwa zaidi itakayobomoa misingi ya amani na umoja wa kitaifa."
mume sema kweli tupu ila wakuyafanyia Kazi maneno haya ndohayupo nadhani mungemshauri turudi kwenye mfumo wa chama kimoja
 
Masemaji wa kanisa ni Papa.
Na papa Ana balozi wake hapa......
Huo waraka siyo kauli ya kanisa.....ni mawazo tu ya maaskofu kama watz wengine......

Duh mkuu na wewe ni Mkatoliki? kama wewe ni mkatoliki basi hujapata hata mafundisho ya awali ya komunio ya kwanza. Yaani wewe unajua msemaji wa kanisa ni pope?. Lini pope kawa msemaji wa kanisa? Pope ni kiongozi wa kanisa na mara nyingi maamuzi hutolewa na vyombo vya maamuzi vya kanisa level ya dunia. Halafu nani alikwambia balozi wa pope ni msemaji wa kanisa? Hebu kabla hujachangia uwe unajifunza kwanza. Balozi wa pope hajawahi wala hatakaa awe msemaji wa kanisa. Eti huo waraka siyo kauli ya kanisa bali ni mawazo ya maaskofu wa tanzania , sasa mkuu KANISA ni nini?. Naomba nikufunze kidogo, kanisa huanzia level ya dunia (kiongozi wake ni pope) halafu inaenda moja kwa moja kwenye level ya jimbo (kiongozi wake ni askofu wa jimbo) penye askofu kanisa linakamilika kabisa. Lakini maaskofu wanapokutana wote hapo KANISA limekamilika kabisa. kwahiyo ndg huo waraka ni ni kauli halisi na halali ya kanisa na haliwezi kupingwa hata na pope wala balozi wake, kingine mawazo ya maaskofu tanzania ndiyo mawazo ya kanisa. Kama hujui uwe unauliza upewe mwanga.
 
Dalili za kupungua kwa sadaka ziko wazi!wapambane na hali yao![emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
Wataanza kutozwa kodi shauri zao,au kuchunguzwa uraia wako.wangekuwa na ubavu huo si wangewatenga na kuwafukuza ushiriki wale wote wasababishi wa waliyoyaandika kwenye waraka wao.

Duh aisee muwe mnjifunza utaratibu wa kanisa kwa undani kabla ya kuzungumza!, kanisa linaweza kumfungia mtu ushiriki wake kwenye kanisa ila hiyo hatua ili ichukuliwe ni lazima labda uwe umeasi au umefanya kosa kubwa sana dhidi ya imani ya kanisa. Na sababu ni kwamba hata Yesu na mitume wake hawakuwahi kuwafungia watu kwenye mambo ya imani huko ni kuhukumu.
 
Namfahamu sana. Rafiki yangu niliye kua naye shule alikua Askofu msaidizi wake. Na ninajua nini swali baada ya hili. Pengo siyo mropokaji kama wengine. Pengo ana wakati wake anauona muafaka anakuja na lungu lake. Sijui umri wako huko nyuma Pengo aliwasema CCM waziwazi. Unakumbuka alipowaambia CCM na serikali yake kuwa "Hittler alichaguliwa na wananchi wa ujerumani ki demokrasia na wala hakupindua nchi. Watu walichoka na muelekeo wa serikali ya wakati huo ya Ujerumani ikaamua kumuweka Hitller madarakani. Ningeoba sana ninyi watawala muangalie upya jinsi mnavyoendesha serikali isiye ya udhalimu tukaja tukamuweka Hitller wetu hapa Tanzania. Maana watu wakiwachoka na mambo yenu watampigia kura yeyote yule ili mradi wabadilishe uongozi. Hivyo msitukwaze" huyo alikua Pengo. Miaka ya 90 wakati serikali ilikua inapiga virungu mpaka wanafunzi migomo mingi ya madaktari n.k. Hivyo wengi humu ndani JF wamezaliwa juzi juzi hawamjui kabisa Pengo. Pengo alikua mwiba kwa CCM wakati huo hakuna vyama vingi.
Mwaka gani alitamka haya?
 
Kumfahamu mtu haihitaji uwe umri sawa naye, haihitaji umzidi au uwe mdogo kwake, haihitaji muwe mmesoma nsye au uwe umemfundisha. Rekodi zinaongea. Aonekanavyo ndivyo alivyo. Ni kama Prof Kabudi wa Tume ya Warioba na Prof Kabudi waziri, ni watu tofauti wenye misimamo na kauli tofauti.
Unaweza uka highlight kwa majina ni watawala gani wa hapa nchini ambao Pengo aliwakemea?
 
Back
Top Bottom