Sidhani kama Serikali itakuwa na haraka sana kuanza ligi na Kanisa Katoliki. ni kitu kimoja kumhoji uraia Askofu NiweMugizi, au kukagua mpaka nguo za ndani za mke wa Askofu Kakobe, lakini ni kitu kingine kabisa kuanzisha ligi na Kanisa Katoliki lenyewe.Ngoja tuone kama watatumiwa TRA maana katoliki wana miradi mingi
Pengo la Pinda [emoji23] [emoji23] [emoji23]Namsubiri "rafiki" wa pinda atie neno maana hakawii kusema alikua Vatican hahusiki na "tamko"
Mmenikosha maaskofu wangu. Nadhani Maaskofu wa DRC wamewapa somo. Sasa naahidi kuongeza mchango wa Tegemeza Jimbo kwa mwaka huu mpaka laki moja. Nilishaacha kuchangia kabisa kwa sababu ya Pengo!
Uongozi wa nchi yetu hauna utaratibu wa kujibu waraka.Ingekuwa hivyo ingebidi kuwe na mtu maalum wa kujibu nyaraka za kanisa maana ni nyingi mno na ni za kila wakati.Wametoa mawazo yao tunawadhukuru lakini nchi inasonga mbele kwa taratibu za kinchi na sio za kanisa.Kanisani tuonane hukohuko na ni lazima tuje kusali kwani tuna muhitaji Mungu vilevile.
Jumapili ijayo nitawahi deski mbele St peters
Hahahaha...
Sasa nimeanza kuelewa kwanini ile sala ya Mwanakondoo..tumedili kutoka "aondoae dhambi za dunia kuwa dhambi za ulimwengu"
Hahahaha...
Sasa nimeanza kuelewa kwanini ile sala ya Mwanakondoo..tumedili kutoka "aondoae dhambi za dunia kuwa dhambi za ulimwengu"
Masemaji wa kanisa ni Papa.
Na papa Ana balozi wake hapa......
Huo waraka siyo kauli ya kanisa.....ni mawazo tu ya maaskofu kama watz wengine......
Tamko hili limewatarget zaidi watawala wakatoliki ili waelewe wanachofanya pamoja na kanisa kukaa kimya lakini wanaona na hivyo wabadili matendo yao.
Ilikuwa Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu, chini ya Askofu Mkuu Paulo Ruzoka. Ni kweli Rais wa TEC ndiye msemaji wa Kanisa Katoliki Tanzania. ndiyo maana siyo rahisi Kardinali Pengo kuukana waraka huu. itamletea matatizo makubwa sana.
Ipo tofauti. Zile Nyaraka za 2010 za Kanisa Katoliki kama kaulimbiu ya kuwaandaa waumini kwa uchaguzi mkuu, na hata ule wa karibuni zaidi ambao Kardinali Pengo aliukana, zilitolewa na kamati za Baraza la Maaskofu. tofauti ni kwamba ile inakuwa imeidhinishwa na askofu mhusika wa kamati. hapo utaona jina la Askofu mmoja tu ambaye ndiye mkuu wa Kamati husika. na pia Waraka unakuwa na nguvu ya kushauri tu, si wa kimamlaka kwa nchi nzima. ndio maana Pengo aliukana bila kuwa na wasiwasi.
Huu wa sasa umetolewa na Baraza lenyewe la Maaskofu na wameusaini Maaskofu wote wa nchi nzima. hapo sasa waraka huu una nguvu za kutumika kama nyenzo ya uinjilishaji kwa taifa zima. Ni kauli rasmi ya Kanisa Katoliki Tanzania na Maaskofu wote kwa kweli wanalazimika kuuheshimu. Ni tofauti kubwa sana na Historia imeandikwa.
Mkuu,
usiache kuchangia kanisa kwa ajili ya Pengo na D'Salaam yake. Wakikuudhi changia jimbo lolote achana na D'Salaam ya Pengo.
By the way Pengo ataondoka na kuiacha D'Salaam kwa askofu mwingine anayekidhi kama tatizo la Rulenge lilivyodhibitiwa kwa kumleta NiweMugizi kuisambaratisha Jumuiya ya Mshikamano.[/QUO
Mwache kwanza amsambaratishe MangeMara paap ....sheikh wa BAKWATA anawajibu.
Unajuwa Sugu amewekwa jela kwa kesi bailable kwa tuhuma gani?Hiki kifungu kwenye waraka wa hawa jamaa kina mantiki; "Kufungiwa huku kwa vyombo vya habari kumeenda sambamba na kuminya uhuru wa Mahakama na Bunge kwa njia ya kuminya haki wabunge na kutowapa nafasi ya mikutano ya hadhara kama haki yao ya msingi ya kikatiba.” Ni kweli kwamba wabunge wamezuiwa kufanya mikutano kwenye majimbo yao? Hii inadhihirisha kwamba hawa watu hawajui kinachoendelea na badala yake wameandika kile walichoambiwa na hao waliotaka habari hii iandikwe kwa namna ya kizushi na sio kiuahalisisa!